Dr.Slaa: Atakayekiuka UKAWA tutamshughulikia

Dr.Slaa: Atakayekiuka UKAWA tutamshughulikia

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
53,868
Reaction score
121,001
Wakuu Katibu Mkuu wa CHADEMA ametoa angalizo hilo kwa mbunge wake atakeenda bungeni kusaliti wananchi.Hii imeripotiwa magazetini asubui.Pia imeripotiwa wabunge wa Ukawa wamerejea bungeni,huu ni upotoshaji,mbunge aliyerejea ni mmoja tu sio kama CCM wanavyopotosha
 
Mtanzania wameripoti aliye rejea BMK ni Leticia Nyerere na John chibuda. Hatua kali ni muhimu zichukuliwe
 
Ukawa vipande vipande
WABUNGE WA UKAWA WAANZA KUREJEA BUNGENI, LETISIA NYERERE WA CHADEMA AHUDHURIA VIKAO
Mbunge wa Viti Maalum, Leticia Nyerere (CHADEMA) ajisajili leo katika Bunge Maalum la Katiba
Chanzo.tarifa ya habari ya ITV leo
****************************** *******************
By Alexandry Nemesi
Mbunge wa Viti maalum kupitia CHADEMA Mh.Leticia Nyerere kwa mujibu wa ITV habari usiku huu ameonyeshwa na amesaini kitabu cha Mahudhurio ndani ya Bunge maalum La Katiba ikiwa ni kinyume na Msimamo wa CHADEMA kwa wajumbe wake kutohudhuria vikao hvyo.
Ni dhahiri sasa Leticia ameonyesha sura yake halisi kutokana na matendo yake ndani ya Chama kwa kutoheshimu maamuzi ya Vikao halali vya chama.
Ni wakati sasa wa Chama kumchukulia hatua kali za kinidhamu ikiwemo kuvuliwa uanachama.
By ifweero
Mbunge wa viti maalum chadema na mujumbe wa bunge maalum la katiba ( mjumbe wa ukawa) amerudi bungeni kuendelea na vikao vya bunge maalum tupate katiba mpya. Hongera sana leticia. Taifa kwanza, vyama baadae
source: itv habari
 
Ukawa waliopo bungeni ni leticia nyerere, hamad rashid mohamed, said arf, na john shibuda
 
Ukawa waliopo bungeni ni leticia nyerere, hamad rashid mohamed, said arf, na john shibuda

Ahmad Rashid na zzk,hao ni wabunge wa mahakama hawapo Ukawa,aliyepo Ukawa ni Leticia Nyerere ambaye tayari mh Halima Mdee alishamuonya juu ya undumila kuwili wake kwa ccm,na Shibuda ni Mbunge wa ccm kupitia chadema
 
Wakuu Katibu Mkuu wa CHADEMA ametoa angalizo hilo kwa mbunge wake atakeenda bungeni kusaliti wananchi.Hii imeripotiwa magazetini asubui.Pia imeripotiwa wabunge wa Ukawa wamerejea bungeni,huu ni upotoshaji,mbunge aliyerejea ni mmoja tu sio kama CCM wanavyopotosha
The ideal of free human beings enjoying civil and political freedom.
 
wako wabunge wengi wanataman kurejea ila unafiki na kutojiamini vinawasumbua
 
chadema inaendekeza utawala wa kibabe na kimabavu, chadema ni chama cha kidikteta,, leticia ni haki yake kikatiba kwenda bungeni,, babu slaa atuonyeshe katiba ya ukawa inayokataza wasiende bungen
 
ukawa hawana lolote wanalotetea wananchi. ukawa wanatetea matumbo yao
 
wako wabunge wengi wanataman kurejea ila unafiki na kutojiamini vinawasumbua

Wanalinda heshima yao kwa wananchi na huo ni ushujaa wa hali ya juu kuamua kuacha posho na kukaa nje ili sauti ya nguvu ya umma isikike kupitia wananchi.
 
Ahmad Rashid na zzk,hao ni wabunge wa mahakama hawapo Ukawa,aliyepo Ukawa ni Leticia Nyerere ambaye tayari mh Halima Mdee alishamuonya juu ya undumila kuwili wake kwa ccm,na Shibuda ni Mbunge wa ccm kupitia chadema

tafadhali nieleweshe maana ya mbunge wa mahakama na mbunge wa ccm kupitia chadema.
 
Back
Top Bottom