Watu wanataka yawe mazuri over a night Chadema iwe na uongozi mzuri kesho, ifike vijiji vyote kesho, ishinde urais kesho, ibadili uongozi kesho, wasipofanya hivyo hawafai kupewa uongozi. Hawalewi kuwa hayo yote yanahitaji time, resources na watu, na watu wenyewe ndio sisi hatutegemei waje toka Norway au Zambia.
Wakati tunataka kitu tujaribu kuangalia reality, mfano tunalaumu Chadema haijaweka wagombea kwenye majimbo yote. Hatujiulizi kwa nini, kwani chadema haitaki wabunge, kuna constraints ambazo tunaacha kuzizingatia sijui kwa ni kwa makusudi au.
Angalia wagombea wangapi wa Chadema wamewekewa pingamizi za ajabu ajabu na wasimamizi wa NEC wamezikubali, mfano Mwanza mjini eti si raia, chukulia MO waliwekeana pingamizi yake ikapita angalia uraia wa Bashe na wa Kigwanagala. Kama wewe si mshabiki vitu kama hivi ni vya kuangalia lakini tukiwa tunajadili huku tukitawaliwa na ushabiki vitu vya msingi hatuwezi kuviona.
Utakuta mtu anasema Chadema hakifai kupewa nchi au CCM wameshindwa kuongoza, na si uongo wote tunazama humo matokeo yake tunajaza page bila ku gain chochote.