Ng'azagala
JF-Expert Member
- Jun 7, 2008
- 1,288
- 222
CHADEMA wasilaumiwe mambo hayawezi kukaa vizuri mara moja;
Ni mchakato wa muda mrefu. Nafikiri CHADEMA ni vema wakazingatia ushauri.
Don't be biased Geza Ulole ame hit kabisa post yako labda yuko negative na mawazo yako, kasema si lazima Mwenyekiti awe mgombea urais nilitegemea haya maneno uliyomwambia GU utamwambia Nyani Ngabu ambaye yuko off topic kabisa linganisha hizi posts nani yuko off,usome kilichoandikwa usisome unachofikiria kimeandikwa.
si lazima wabadilishe mwenyekiti; yaani mwenyekiti anaendelea kuwa Mwenyekiti lakini uongozi wa chama kimtazamo na mwelekeo unatolewa na mgombea wa Urais. Kwa hiyo hawahitaji kubadili Katiba ni makubaliano ya kimantiki tu.
Don't be biased Geza Ulole ame hit kabisa post yako labda yuko negative na mawazo yako, kasema si lazima Mwenyekiti awe mgombea urais nilitegemea haya maneno uliyomwambia GU utamwambia Nyani Ngabu ambaye yuko off topic kabisa linganisha hizi posts nani yuko off,
Baada ya kusema hayo mimi nafikiri huu sio muda mwafaka kwa chama kilicho kwenye kampeni kuanza kuzungumzia vyeo hata mwenyekiti wa Chadema Mbowe alishawahi kutamka hayo.
Pili naungana na Geza Ulole kuwa mgombea urais si lazima awe Mwenyekiti na si chadema pekee waliofanya hivyo TLP NRA NCCR havijaweka wenyeviti wao kuwa wagombea, hata Obama hakuwa Mwenyekiti wala kiongozi mkuu wa Democrats kama unavyosema.
Kuhusu kiongozi mkuu wa chama hilo linategemea na katiba inasemaje kila chama kina utaratibu wake wa uongozi. Hata CCM unayoisema mgombea wake ndiye m/kiti ina mpango wa kuachama na mtindo huo kwa vile haumpi muda wa kutosha rais kupumzika, yeye aongoze chama yeye huyo huyo awe amiri jeshi na kiongozi wa serikali ni mzigo mzito.
Vile vile si busara kwa mtu mmoja kulundikiwa vyeo kama vile chama hakina watu wengine wenye uwezo. Kwa kufanya hivyo tutakuwa tunarudi kwenye enzi za zidumu fikra za m/kiti.
You are right mawazo ya wengi yamejikita kwenye kampeni team yanasahau majukumu ya mwenyekiti ambaye ni kiongozi mkuu wa chama wherther kuna uchaguzi au hakuna, mwenyekiti wa chama anabaki na madaraka yake hanyang'anywi na mgombea yayote, hiyo ndiyo misingi ya chama.Tatizo hapa ni kufikiri campaign team + manager= Mwenyekiti
Kuna thread zingine hata zingekuwa na malengo mazuri kiasi gani timing yake inakuwa suspect. Tayari Mwanakijiji kwa kuanzisha hii mada anapanda mbegu kwenye mioyo ya wadandiaji fulani fulani kuwa kuna mgongano katika uongozi wa Chadema, kati ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu au kati ya mgombea Uraisi na mgombea Ubunge - hogwash !
Sikusikia hii wakati Mwinyi anafanya Kampeni Mwenyekiti wake akiwa Mwalimu Nyerere, sikusikia hii Mkapa akifanya kampeni huku Mwenyekiti wake akiwa Mwinyi na sikusikia mgongano wakati Kikwete anapiga kampeni Mwenyekiti wa CCM akiwa Mkapa. Hizi controversies zinazoanzishwa kuhusu Chadema at this time zina malengo gani kama si kuidhoofisha Chadema wakati uhai wa chama chochote cha siasa kwa wakati huu unategemea mshikamano na si vyeo ?
Chedema hawawezi kuongoza nchi. Wanaubinafsi na uroho wa madaraka. Mwaka huu wataanguka zaidi hata kuliko 2005.
Watu wanataka yawe mazuri over a night Chadema iwe na uongozi mzuri kesho, ifike vijiji vyote kesho, ishinde urais kesho, ibadili uongozi kesho, wasipofanya hivyo hawafai kupewa uongozi. Hawaelewi kuwa hayo yote yanahitaji time, resources na watu, na watu wenyewe ndio sisi hatutegemei waje toka Norway au Zambia.CHADEMA wasilaumiwe mambo hayawezi kukaa vizuri mara moja;
Ni mchakato wa muda mrefu. Nafikiri CHADEMA ni vema wakazingatia ushauri.
Mkuu LuteniWatu wanataka yawe mazuri over a night Chadema iwe na uongozi mzuri kesho, ifike vijiji vyote kesho, ishinde urais kesho, ibadili uongozi kesho, wasipofanya hivyo hawafai kupewa uongozi. Hawalewi kuwa hayo yote yanahitaji time, resources na watu, na watu wenyewe ndio sisi hatutegemei waje toka Norway au Zambia.
Wakati tunataka kitu tujaribu kuangalia reality, mfano tunalaumu Chadema haijaweka wagombea kwenye majimbo yote. Hatujiulizi kwa nini, kwani chadema haitaki wabunge, kuna constraints ambazo tunaacha kuzizingatia sijui kwa ni kwa makusudi au.
Angalia wagombea wangapi wa Chadema wamewekewa pingamizi za ajabu ajabu na wasimamizi wa NEC wamezikubali, mfano Mwanza mjini eti si raia, chukulia MO waliwekeana pingamizi yake ikapita angalia uraia wa Bashe na wa Kigwanagala. Kama wewe si mshabiki vitu kama hivi ni vya kuangalia lakini tukiwa tunajadili huku tukitawaliwa na ushabiki vitu vya msingi hatuwezi kuviona.
Utakuta mtu anasema Chadema hakifai kupewa nchi au CCM wameshindwa kuongoza, na si uongo wote tunazama humo matokeo yake tunajaza page bila ku gain chochote.
Kama hadi leo hujui kwa nini huwaoni kwenye TV hutawaona milele.unamaanisha nini??? tarehe 31 october si mbali,
mpaka sasa hatuwaoni kwenye TV waki campaign
The Democratic National Committee provides national leadership for the Democratic Party of the United States. It is responsible for promoting the Democratic political platform, as well as coordinating fundraising and election strategy. Shortly after his inauguration, Barack Obama transferred his Obama For America organization to the DNC
Mwanakijiji,
Mimi ni mwanafunzi wa historia. Naamini kabisa kuwa Dr. Slaa atakapokuwa rais atakuwa ndiye "main spokesman" wa CHADEMA. Tuachane for a minute na culture ya CCM ambapo Mwenyekiti wa chama alikuwa/ndiye rais wa nchi.
Tunaweza kutumia altenative ya Marekani ambapo flag bearer katika uchaguzi anakuwa automatic party leader.
Licha ya ushabiki wangu kwa Zitto au Mbowe, sasa hivi our flag bearer ni Dr. Slaa. Nitaendelea kuwaheshimu Mbowe/Zitto kama viongozi wetu lakini tunajua anayebeba bendera yetu ni Dr. Slaa. Na ikitokea hivyo CHADEMA will be writing a new page in our history kwamba siyo lazima uwe mwenyekiti wa chama kuwa flag bearer. Ni dalili njema.
Chama kitampa mwongozo wake na watasimama nyuma yake na siio chama kusimama mbele ya Dr. Slaa ktk maswala ya uchaguzi na hata kuunda serikali. Ifahamike tu huu ndio mwanzo wa kutafuta Urais, madaraka makubwa ya chama yanpokwenda nje ya chama ndio mwanzo wa chama kumchagulia rais watu ktk nafasi za Uongozi wa nchi.. Rais mtarajiwa ndiye anayetakiwa kuchagua watakao ongoza kampeni yake na sio lazima yeye awe Mwenyekiti wa Kampeni ya Uchaguzi na sio kabisa awe mwenyekiti wa chama, ila kama atapenda kuwa mwenyekiti wa kampeni ya uchaguzi basi chama hakina sababu ya kukataa.