Sielewi ni kwa nini CCM wamekazana na dhana ya kwamba elimu bure kuanzia darasa la saba hadi kidato cha sita bure ni dhana isiyowezekana, labda wanataka tukubaliane na iledhana ya Dr. Slaa ya kwamba ndiyo wamefikia mwisho wa uwezo wao wa kufikiri.
Ni aibu kwa Sita kubwabwaja ati elimu bure ni ndoto wakati fedha alizotumia kujenga ofisi ya jimbo tu ingeweza somesha wanafuzi wote wa mkoa wa Tabora kati ya darasa la saba hadi form six bure kwa miaka zaidi ya mitano!
Nafarijika na ufahamu wa wananchi unaoongezeka kila kukicha kwamba CCM aliyoiacha Nyerere si hii bali iliyoko ni nembo juu ya box alilofungiwa nunda mla watu ndiyo CCM.
Mbona kwa miaka mingi sasa, Halmashauri zinazoongozwa na CHADEMA zimekuwa zikitoa elimu hiyo bure tena kwa makusanyo ya kodi za Halmashauri tu bila ya kuihusisha serikali kuu?
Watanzania wenzangu, habu turejee maneno ya mwanaharakati mmojawapo nchini Christofa Mtikila kuwa saa ya Ukombozi ni sasa. Tusikubali kuipoteza fursa hii ya kulipa kisasi cha udhalilishaji mkubwa na ujambazi uliofanywa na CCM kwa raia wa nchi hii.
Tanzania bila CCM, Kikwete, Makamba na Msekwa inawezekana.
Hukumu ya CCM ni Oktoba 31, usisahau kufoleni na silaha yako, ndiyo kadi ya kupigia kura itakayoiweka madarakani CHADEMA na wagombea wake. Kura ya kwanza mpe Dr. Slaa, ya pili Mbunge wa CHADEMA na ya tatu Diwani wa CHADEMA ili CCM waambulie majivuno yao. Mungu ibariki Tanzania.