Elections 2010 Dr Slaa ITV Live sasa

Elections 2010 Dr Slaa ITV Live sasa

Hivi hakuna uwezekano wa kuwa na kipind maalumu kwa kweny ITV kila siku katika siku zilizobaki kumpa rais wetu mtarajiwa awe anamwaga vitu hapo wakuu au sheria hairuhusu?
 
Padres.JPG
Hivi wasomi wote hao mpaka tuongozwe na Padre?
 
People Poweeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeerrr!!!!!!!!!!!!!!!
 
Kaka asante kwa kutushtua ni kweli jamaa anaongea kwa uchungu sana..

Tukijitahiti kushawishi watu kumi kwa kila mpenda mabadiliko.. JK nje..
 
Niliangalia mahojiano hayo.....mimi hayakunifumbua macho maana Dr Slaa namjua alivyo mweledi na makini. Leo asubuhi nakutana na wana CCm wa mtaani kwetu, baadhi nikawapa lift kwenda ofisini......kweli hayo mahojiano yameleta impact kubwa!....jamaa hawa ni pure kijani na njano lakini walikiri kwamba Dr Slaa anastahili kuwa rais wetu! Ningependa mahojiano kama haya yafanyike mara nyingi iwezekanavyo ili watu wengi waweze kufumbuliwa macho....watu wako gizani jamani! Hii kijani na njano pia na nyundo juu.....inampofusha mtanzania. Mungu isaidie Tanzania...watu wajue lipi jema na lipi baya...tufanye uamuzi sahihi Octoba 31. Amina.
 
kwa sasa jk anajipya anachofanya nikuahidi kila kukicha ameona maji yana mfika shingoni
 
Jaman huku kwetu umeme uli katwa jana usiku! Hvi kipindi kita rudiwa lini? Anaye jua atuhabarishe ili tuweke screan ztu nje waone wengi huku kijijini.
 
nilibahatika kumsikiliza Dr slaa jana, kwa kweli jamaa alishuku vilivyo - aliongelea sera za CHADEMA kuhusu huduma za jamii kama afya, elimu na makazi huku akitoa mifano ambayo mtu wa kawaida kabisa lazima atamuelewa.. Huyu ndiye anafaa kabisa kuwa Rais wetu kwani anaelewa fika kiini cha matatatizo yetu na ufumbuzi wake.

Majibu mazuri sana kuhusu muungano wetu na masuala mengine ya usalama wa taifa. Hakuna ubishi CHADEMA imejipanga vilivyo kuaddress hizi kero kuu endapo watapewa ridhaa ya kuongoza nchi hii.
 
Jana nilisuuzika moyo wangu mno. Alizungumza points mpaka nikajikuta natamani aendelee kuongea tu. Wadau hebu tuendelee kuchangia chadema ili kuwezesha hizi advocacy japo kwa muda uliobaki. Andika SLAA au CHADEMA na tuma 15710. Ujumbe mmoja unakuwa umechangia sh. 350, tuma jumbe nyingi kadri uwezavyo. Changia mabadiliko Tanzania. Kweli ndio maana wanakuogopa Dr. Slaa na wanatumia nguvu kubwa ya kuweka mabango. Hivi hayo mabango ukiyaunganisha si itakuwa ni line ndefu sana ya nguzo za umeme? Hivi bei ya bango moja na ile ya nguzo ya umeme ipi kubwa? Lack of common sense. shiiiiiiiiiiiit. Halafu huko vijijini hakuna umeme, miaka nenda uje halafu bado wanapigia Chama Cha Majambazi.
 
kwa sasa jk anajipya anachofanya nikuahidi kila kukicha ameona maji yana mfika shingoni

Ha ha ha mkuu, eti kaahidi fly overs na maji tele DSM? Tangu lini Dar iwe na maji ya uhakika wakati Rufuji inamwaga maji kila siku? Tena kipindi cha kiangazi maji ni tone, ndiyo maana nyumba zetu nzuri unakuta zimetundikwa tanki za maji zinaharibu mandhari kabisa. Yaani kila kukicha masim-tank kila nyumba. Hivi kampeni za 2005 si aliahidi maji yatafurika DAR na atachukulia vyanzo vingine kama Rufiji River? Nisaidieni hapa Wakuu. Tumechoshwa na Siasa za maji taka, za danganya toto. Asifikiri ataendelea kutupa pipi kifua kama anavyowagawia watoto ambao anakutana nao njiani wakiwa na nguo za kuchanika hakuna hata katambuga mguuni na shule hawaendi. Je pipi ni chakula, elimu, vituo vya afya na madawa/wataalam?
 
Hivi wasomi wote hao mpaka tuongozwe na Padre?

Kwani Padre siyo msomi?!!

Asante mkuu kwa kumweleza. Kwa kifupi mapadre wamesoma sana!! Kwa ufupi, kuna 6 years secondary (O and A Levels), ongeza miaka mitatu, Theology, ongeza miaka mitano Phylosophy!! Phylosophy na Theology ni zaidi ya Masters/PhD. Mapadre ni vichwa acha kabisa. Halafu Dr. Alisoma kabisa PhD in Phylosophy!!! Ambayo hata wewe na mimi tunaweza enda kusoma. Je ile ya Mkwere ni degree ipi tena, looo B.A (Econiomics)? Pia inategemea degree yako ni First class, Upper Second, Lower Second, or what, tena with Hons au kavu tu? Utakuta mtu kila mwaka Supplementary, degree kahemea halafu naye anajidai?
 
JK anaahidi kama kachanganyikiwa - eti Hospitali za rufaa kila jimbo, Maching Complex kila Mkoa - ha ha ha this is more than too much. Hata mtoto wa miaka 10 ulimnyambulishia kwa lugha nyepesi yote aliyoahidi miaka 5 iliyopita na utekelezaji wake na haya ya sasa atashtuka.

Na kila ahadi utasikia, Wenzetu wa uchina wanatusaidia, mara wenzetu wa India, Japan, Marekani tumeingia nao mkataba. ina maana ahadi zote hizi ni za ombaomba? Kikwetu nyumba inayo ombaomba hadi unga wa ugali huwa haina heshima kabisa mbele ya Jamii. sasa JK usiifanye Tanzania nchi ya kwanza duniani kwa kuomba omba hatutaki aibu zaidi ya hii.
 
Hivi wasomi wote hao mpaka tuongozwe na Padre?


Kweli CCM imeishiwa sera, yaani mpaka wanajichanganya sasa, hivi wewe unajua kuwa Slaa ana PHD? unajua kanisa lina system yake ya elimu ambayo ushindani wake si viwango vya kawaida (na uhakika na hilo kwakuwa nimesoma huko na pia nimesoma UDSM). John10, nasikitika kukwambia kuwa - you are too late!
 
Sielewi ni kwa nini CCM wamekazana na dhana ya kwamba elimu bure kuanzia darasa la saba hadi kidato cha sita bure ni dhana isiyowezekana, labda wanataka tukubaliane na iledhana ya Dr. Slaa ya kwamba ndiyo wamefikia mwisho wa uwezo wao wa kufikiri.
Ni aibu kwa Sita kubwabwaja ati elimu bure ni ndoto wakati fedha alizotumia kujenga ofisi ya jimbo tu ingeweza somesha wanafuzi wote wa mkoa wa Tabora kati ya darasa la saba hadi form six bure kwa miaka zaidi ya mitano!
Nafarijika na ufahamu wa wananchi unaoongezeka kila kukicha kwamba CCM aliyoiacha Nyerere si hii bali iliyoko ni nembo juu ya box alilofungiwa nunda mla watu ndiyo CCM.
Mbona kwa miaka mingi sasa, Halmashauri zinazoongozwa na CHADEMA zimekuwa zikitoa elimu hiyo bure tena kwa makusanyo ya kodi za Halmashauri tu bila ya kuihusisha serikali kuu?
Watanzania wenzangu, habu turejee maneno ya mwanaharakati mmojawapo nchini Christofa Mtikila kuwa saa ya Ukombozi ni sasa. Tusikubali kuipoteza fursa hii ya kulipa kisasi cha udhalilishaji mkubwa na ujambazi uliofanywa na CCM kwa raia wa nchi hii.
Tanzania bila CCM, Kikwete, Makamba na Msekwa inawezekana.
Hukumu ya CCM ni Oktoba 31, usisahau kufoleni na silaha yako, ndiyo kadi ya kupigia kura itakayoiweka madarakani CHADEMA na wagombea wake. Kura ya kwanza mpe Dr. Slaa, ya pili Mbunge wa CHADEMA na ya tatu Diwani wa CHADEMA ili CCM waambulie majivuno yao. Mungu ibariki Tanzania.
 

Attachments

  • Image001.jpg
    Image001.jpg
    79.9 KB · Views: 25
Back
Top Bottom