Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 21,470
- 40,593
Kuna tetesi kwamba kuna majadiliano yanaendelea kati ya marafiki wa Slaa walioko CCM na Slaa kuhusu uwezekano wa mwanasiasa huyo kuwa Katibu Mkuu wa CCM baada ya Katibu Mkuu wa sasa Abdulrahman Kinana kumaliza muda wake.
Marafiki hao ndani ya CCM wanadai kwamba "Style" ya Mwenyekiti wao John Pombe Magufuli inaendana na Slaa na wanaamini kwamba wawili hao watakiimarisha sana chama chao. Pia inadhaniwa kuwepo kwa Slaa kutakuwa ni mwiba mkali sana kwa chama chake cha zamani CHADEMA.
Slaa alikuwa ni mwanachama wa CCM kabla ya kujiunga na CHADEMA mwaka 1995 kutokana na kutopewa nafasi ya kugombea Ubunge jimbo la Karatu kupitia CCM. Kuna wakati CCM walidai kuwa Slaa alikuwa bado analipia kadi yake na Slaa mwenyewe alikiri kwamba kadi yake ya CCM bado anayo.