- Mkuu unajua sisi watu wa mjini matusi ni kawaida sana kwanza hapa hujatukana, na siwezi kushuka hiyo level hapana, however ninakukaribisha kurudi kwenye mada anytime ukimaliza matusi yako, ha! ha! ha!
William.
Bwana Malecela Jr. Humu ndani itakuja kurukwa na akili. Sasa wewe utakuwa mtu mmoja unapingana na dunia nzima. Uwezo huo hauna kitu cha kwanza. Unajua ubishi wako ni wa kitoto usiyokuwa na maana.
1. Fedha za watanzania walipa kodi zinaibiwa, unataka wafanyeje?
2. Serikali iliyo madarakani ya Kikwete na babako ndo wezi, hiyo unasemaje?
3. Wewe baba yako amefanyiwa kitu kibaya bado unaitetea CCM akili iko wapi?
4. Unataka kuniambia kwamba hakuna kitu kama DOWANS, kwa hiyo watanzania wasiulize au ni haki ya hao majambazi kuwaibia watanzania?
Nadhani ungetafakari kilio cha walio wengi ukatumia busara kuangalia unakotoka na unakokwenda. Naona umeamua kutumia jina lako ili kundi la kikwete wakusome, sawa watakusoma. Ila watu wenyewe wamelewa wewe watakusaidia nini? Miaka yote CCM ikiwa madarakani na baba yako akiwa kinara ni kitu gani ulichokifaidi? Mkuu humu tuna machungu sana. Nchi yetu inaharibika watu kama wewe ndo wale ambao watatufukuza kuingia porini na kurudi kama wanyama wa kweli kuing'oa CCM na Kikwete.
Mimi nimezaliwa ndani ya CCM. Baba yangu bado yupo ndani ya CCM, mwenye bado ni mwana CCM tena mwenye kadi tangu 1989 ila naamua kuipinga serikali ya Kikwte iondoke madarakani. Tumechoka. Tutembelee uone ucungu wetu siyo kukaa na ndoto zako za abunuwasi.
http://ufisaditanzania.blogspot.com[/QUOTE]
Mkuu naungana na wewe kabisa. Matusi na lugha chafu vinatokana na frustrations, hakuna nayekubaliana na hili hata kama mtu anasema ni way of life ya watu wa mjini. Sisi watu wa vijijini hatukubaliani na that way of life, ni bira tufukuzane na kupiga kelele na ng'ombe wetu kuliko kuongea lugha chafu.
Ukweli ni kwamba, si kila mwanaCCM ni mwizi na si kila mwana CCM ni mpumbavu. Ukiangalia kwa undani unaona wazi kabisa kuwa issue nzima ya umeme, ni watu wachache sana wanaofaidi, hata kama inainufaisha CCM ambacho ni chama chetu, si CCM yote ni kundi dogo sana la watu ambao hata hawafiki 100. Hivi ukianza kuwatetea wanaotufanya watanzania tuishi maisha duni, utakuwa unatumia kigezo gani?
Pamoja na nguvu zote alizopewa kikatiba na nguvu zote za kiuchumi tulizonazo Tanzania nzima, is it conceivable that mpaka leo tunaendelea kuwa na tatizo la umeme, toka JK aingine madarakani umeme ni tatizo na linaendelea kuwepo tu na hayuko serious kulishughulikia. Kwanini?? Kama Slaa akisema JK ndio mmilikiwa Dowans, japo hatuna ushahidi, kwanini tusimuamini? ushahidi wa kimazingira unaonesha wazi kabisa kuwa anayosema Slaa yana mashiko.
Kuna wakati nakuwa na hasira sana na baadhi ya watoto wa Viongozi wa zamani. Mzee Malecela katika uongozi wake (pamoja na upungufu wake kama binadamu wengine) alikuwa mstari wa mbele kupigania maslahi ya anaowaongoza, hakuwa mstari wa mbele kuwalinda wanaoihujumu CCM na wanaoihujumu Tanzania, hata kwenye issue hii najua anaumia.
tatizo la umeme linafanya watanzania wote tuonekane kama watoto, it is even shame to discuss it in 2011. haya yalikuwa ni mambo ya kuzungumzia mwaka 1960.