mchillo
JF-Expert Member
- Oct 13, 2010
- 500
- 224
Asante sana Rutabashubanyuma kwa nyundo ulizoshusha. Ukweli ndio huo kwani tusipokuwa makini watanzania tutaingizwa mjini na Rais huyu ambaye mara kadhaa vitendo vyake vimethibitisha kuwa mpungufu wa umakini. Laiti kama angekuwa makini kidogo tu nchi isingeingizwa kwenye janga kama hili linalotukabili, yaani lakuwalipa matapeli kina RA, EL, NM, na wenzao wa hapahapa nchini mabilioni ya fedha za wavuja jasho.Tuhuma hizi za Dr. Slaa dhidi ya JK inaziunga mkono kwa asilimia mia.........kwa sababu zifuatazo:-
a) Uteuzi wa Dr. Idrissa Rashid kuongoza Tanesco ulijaa mizengwe ambayo ushahidi mwingi ulibainisha ya kuwa JK ndiye aliyeshinikiza Dr. Idrissa kuwa kibosile pale......................................Dr. Rashid mwenyewe alikwisha diriki kusema ya kuwa hakuiomba hiyo nafasi ila aliombwa kuliongoza Tanesco katika mazingira yanayothibitisha ya kuwa kuna ukiukwaji mkubwa wa maadili ya kitaifa unaongozwa na JK mwenyewe...................Ilikuwaje Dr. Rashid apewe nafasi hiyo wakati waombaji wengi wa nafasi hiyo maombi yao yalitupwa ili kufanikisha mianya ya ufisadi ambayo JK alikuwa tayari ameiandaa..........................................
b) Aidha uamuzi wa Dr. Rashid kuizuia mitambo ya DOWANS huku akielewa wao na DOWANS hawana mgogoro wowote ulikuwa mpango kamambe wa kuliingiza taifa hili mkenge na kulifanya liingie hasara kubwa ya mabilioni yanayokadiriwa 185 kwa kuvunja mkataba bila sababu za kimsingi..................Mkataba ambao tayari ulikuwa umekwisha hivyo haukupaswa kuuvunja kwa kuzuia mitambo isiyomilikiwa na Tanesco.......Bilioni hizo 185 zinazidi maradufu hata thamani ya hiyo mitambo hata kama leo ingelinunuliwa kuwa mipya...................
c) Kwa uongozi makini, DOWANS isingeruhusiwa kurithi mkataba wa RICHMOND kampuni hewa na hivyo kulisababishia taifa maumivu makali ya kuendeleza mkataba ambao tayari ulikuwa una nuksi.......................kuanzia awali...................Kama RICHMOND ni kampuni hewa basi mktaba wake iliyourithisha kwa DOWANS nao ni hewa na hivyo hatukupaswa kuuheshimu ila ni ufisadi tu unamwongoza JK kuhalalisha upuuzi huu unaolishushia taifa heshima humu duniani........
d) JK alikuwa ni Waziri wa Nishati kwenye serikali ya Mwinyi na hivyo alihusika moja kwa zote katika ujio wa IPTL ambayo bei zake za kuiuzia umeme TANESCO zimechangia kwa kiasi kikubwa katika kulifilisi shirika hilo la umma na kuliingiza taifa gizani........................vile vile wakati wa utawala wa JK hapo Wizara ya Nishati ndipo kazi ya uagizaji wa mitambo ya umeme wa dharura iliposhika kasi kama ile mitambo ya Ubungo ambayo uendeshaji wake na bei zake za kuinunulia zilikuwa ni ufisadi mtupu......................
e) JK baada ya kuona moto wa Katiba Mpya hawezi kuuzima hasa ukizingatia yeye mwenyewe amepoteza uhalali wa kuliongoza taifa hili baada ya kuchakachua matokeo ya Uraisi kupitia NEC na TISS akaamua kuiteka hoja tajwa na kuibinafsisha kupitia Tume yake mwenyewe atakayoiteua ambayo ni marudio ya michakato ya siku za nyuma ya iliyozaa viraka 15 katika katiba yetu.......na ambayo imeshindwa kukidhi mahitaji ya watanzania wa karne hii ya 21.................haya siyo mageuzi hata kidogo na hayashibishi kiu ya mabadiliko katika katiba yetu................................Katiba Mpya itapimwa kama Bunge litapitisha sheria ya kuainisha mchakato huo shirikishi na ambao una nguvu ya kisheria.....................Siyo Tume ya Raisi ambayo haina nguvu ya kisheria na inaundwa na CCM pekee yake badala ya kuwapa nafasi watanzania wenye sifa kujitokeza na kupimwa na kamati maalumu ya Bunge.............kama wana sifa za kuwa kwenye TUME HURU ya kukusanya na kuainisha matakwa ya watanzania juu ya katiba mpya....................Zipo Tume nyingi za Raisi ambazo matunda yake hakuna anayoyafahamu...........Tume ya Nyalali, WHITE PAPER, Tume ya kukusanya maoni ya muundo wa Afrika ya Mashariki ............n.k..................
Tatizo ni kuwa zimeundwa na Raisi pekee yake ili kuzima uhaja wa mabadiliko nchini na hazina nguvu ya kisheria na hivyo kujifanyia kazi kwa matashi ya yule aliyeziteua.......................UTANi UTANI HUU TUSIURUHUSU KUJITOKEZA KWENYE mchakato wa kuandika KATIBA MPYA...........
Rais Kikwete ni balaa kwa taifa hili na miaka mitano hii ya mwisho ya utawala wake inaweza kuleta maafa yatakayodumu miango kadhaa ijayo. Binafsi sikumpa kura yangu mwaka 2005 kama nilivyofanya mwaka 2010 na sababu iliyonishawishi kutompakura yangu wakati ule ilikuwa hii ya yeye kuhusika kwenye mkataba uliokuwa kichomi kwa taifa; mkataba wa IPTL ambao hata Mkapa alifurukuta kuusitisha aliishia patupu. Niliongozwa na nasaha za Hayati Baba wa Taifa aliposema Rais mla rushwa kamwe hataweza kupambana na rushwa na kweli ikawa hivyo baada ya kugundulika "Madudu" kibao kwenye EPA, Richmond na ile hatua ya ikulu ku -extend mkataba ovyo wa TICTS ambao wabunge walijaribu kuuchachamalia na kuishia patupu baada ya kuambiwa ongezeko la mkataba ule lililofanyika kiholela lilikuwa na baraka za ikulu.
Tukirudi kwenye suala la katiba naungana na wale wenye kuitilia shaka dhamira ya kiongozi huyu aliyepora madaraka kwa hila kwa kusaidiwa na vyombo vilivyopaswa kuuzuia uhalifu ule yaani majeshi, polisi na usalama wa taifa. Huyu ni rais aliyepora madaraka kwa kuupindua uamuzi wetu wananchi wa kumchagua tumpendaye. Huyu ndiye Rais aliyeingia katika awamu ya pili ya madaraka kupitia mapinduzi. Ni mhaini asiyeaminika aliyebadilika kuwa kondoo kwa kasi ya kutisha kwani juzijuzi tu wapambe wake walikuwa wakiimba " Katiba iliyoko ni nzuri wala hakuna haja ya kuiandika upya" Hakuwakemea wala kuwapinga na leo anaahidi kuteua Tume ya kuratibu maoni ya wananchi kuhusu katiba mpya! Wapo waliopiga vigelegele na makofi lakini mimi simwamini hata kidogo mpaka nitakapoona utekelezaji wa hili.
Huu ni wakati watanzania kuwa makini kwa kila kauli za Rais aliyethibitisha mara kadhaa kuwa anayoyasema hadharani ni tofauti na yaliyo moyoni mwake.