Dr. Slaa: Kikwete mmiliki wa DOWANS...

Asante sana Rutabashubanyuma kwa nyundo ulizoshusha. Ukweli ndio huo kwani tusipokuwa makini watanzania tutaingizwa mjini na Rais huyu ambaye mara kadhaa vitendo vyake vimethibitisha kuwa mpungufu wa umakini. Laiti kama angekuwa makini kidogo tu nchi isingeingizwa kwenye janga kama hili linalotukabili, yaani lakuwalipa matapeli kina RA, EL, NM, na wenzao wa hapahapa nchini mabilioni ya fedha za wavuja jasho.

Rais Kikwete ni balaa kwa taifa hili na miaka mitano hii ya mwisho ya utawala wake inaweza kuleta maafa yatakayodumu miango kadhaa ijayo. Binafsi sikumpa kura yangu mwaka 2005 kama nilivyofanya mwaka 2010 na sababu iliyonishawishi kutompakura yangu wakati ule ilikuwa hii ya yeye kuhusika kwenye mkataba uliokuwa kichomi kwa taifa; mkataba wa IPTL ambao hata Mkapa alifurukuta kuusitisha aliishia patupu. Niliongozwa na nasaha za Hayati Baba wa Taifa aliposema Rais mla rushwa kamwe hataweza kupambana na rushwa na kweli ikawa hivyo baada ya kugundulika "Madudu" kibao kwenye EPA, Richmond na ile hatua ya ikulu ku -extend mkataba ovyo wa TICTS ambao wabunge walijaribu kuuchachamalia na kuishia patupu baada ya kuambiwa ongezeko la mkataba ule lililofanyika kiholela lilikuwa na baraka za ikulu.

Tukirudi kwenye suala la katiba naungana na wale wenye kuitilia shaka dhamira ya kiongozi huyu aliyepora madaraka kwa hila kwa kusaidiwa na vyombo vilivyopaswa kuuzuia uhalifu ule yaani majeshi, polisi na usalama wa taifa. Huyu ni rais aliyepora madaraka kwa kuupindua uamuzi wetu wananchi wa kumchagua tumpendaye. Huyu ndiye Rais aliyeingia katika awamu ya pili ya madaraka kupitia mapinduzi. Ni mhaini asiyeaminika aliyebadilika kuwa kondoo kwa kasi ya kutisha kwani juzijuzi tu wapambe wake walikuwa wakiimba " Katiba iliyoko ni nzuri wala hakuna haja ya kuiandika upya" Hakuwakemea wala kuwapinga na leo anaahidi kuteua Tume ya kuratibu maoni ya wananchi kuhusu katiba mpya! Wapo waliopiga vigelegele na makofi lakini mimi simwamini hata kidogo mpaka nitakapoona utekelezaji wa hili.

Huu ni wakati watanzania kuwa makini kwa kila kauli za Rais aliyethibitisha mara kadhaa kuwa anayoyasema hadharani ni tofauti na yaliyo moyoni mwake.
 
Kama Kawaida yake Salva Rweyemamu ameamua kujipaka kinyesi kwa kujibu kijuha tuhuma za Dr Slaa. Huyu inatikiwa aanzishiwa thread yake ili watu wamchambue kisawasawa
 
Malecela kinachokusumbua ni unafki,hata hao wananchi unawataja kuwakejeli tuu, kwako wewe wananchi ni kina makamba, kingunge, John Malecela, Ridhiwan na wengine wanaofanana na, si yule mama anaetegemea kwenda kusaga mahindi watoto wale ugali wa kubahatisha ambao leo umeme unapopandishwa ndo kiama chao! si wale wanafunzi wakijijini wanaosubiri kutembea umbali mrefu kufuata umeme ili wajisomee usiku.

Na wala si mafundi mchundo na wakaanga samaki unaowaongelea.

Ukiona mada imelenga maslahi ya jamaa zako kaa kimya si lazima kuchangia, kwani hata wananchi wa Tanzania huwajui wewe.

Umeishi maghorofani unawajua wapi maskini wa Tanzania? Hao wabunge wa CCM unafikiri wote wanapenda unafiki wa hicho chama? Kwanini mnapokusanya maoni yao bungeni mnawapa karatasi zenye namba? Ili muwabaini wasiopenda unafiki wenu.
 
yaani mimi huwa unanifurahisha tu jinsi unavyowazaga na kukurupuka kama katibu wenu mkuu bila hata kufikiria hata kidogo.
Pengine ndio yeye mwenyewe
 
I absolutely echo Dr. Slaa remark "Kikwete Kikwete mmiliki wa DOWANS" as long as Kikwete doesn't come out and tell the wananch the rightful owner of Dowans.
 
WE NYAU JIMMY>>>>>> ona hayo maandishi yaliyokuzwa jinsi yanavyokuumbua.kwa hiyo mashaka yako yamethibitishwa na kauli ya SLAA???
hivi slaa akikwambia kuwa alitembea na mama yako ukazaliwa wewe hivyo JOSEPHINE MUSHUMBUZI ni mama yako wa kufikia utaamini????
pole kwa kuamini wanasiasa na kuacha akili afanye kazi kwa remote control
 
Nadhani anamaanisha by implication hana evidence. It is a political game

I thank the person who posted this important post. I also ridicule Chifmtz that Dr Slaa does not in any case speak without evidence. There is time and space for everything. The time will tell; everything will be set open. Usiongee tu kwa sababu ni haki ya kikatiba. By the way what is the meaning of political game.:sad:
 


endelea kutumia piriton
 
The reality is now open. DR. SLAA NI MUONGO WA KARNE. i hate to have such political leaders. They are dangerous to Tanzanians.
 
The reality is now open. DR. SLAA NI MUONGO WA KARNE. i hate to have such political leaders. They are dangerous to Tanzanians.
Kwa nini unadhani JK ndio mkweli? Dr Slaa ni Mkweli sana tu kuliko wanasiasa wengi tu. Kusimamia kwake ukweli hasa kwa maslahi na mustakabali mwema wa NCHI yetu ndiko kumempambanua na wanasiasa wote Tanzania.
 
Ni jambo la kushangaza kusikia kuwa rais hajui na wala haifahamu Dowans. Haiingii akilini kabisa, hivi kweli rais atashindwa kuelewa kitu kinachofanyika ndani ya nchi yake? Anasimamia nini sasa kama haelewi kinachoendelea ndani ya nchi yake. Huu ni usanii mwingine,mwenye kaya anasimamia yote, haiwezekani kitu kifanyike au kiingizwe ndani bila yeye kujua. Kwa mtindo huu inaonekana kuna vitu vingi havijui, na hii si kweli, ipo namna hapo. Watanzania tuelezwe ukweli, kama Dowans haipo basi kwa nini tunaendelea kuumiza kichwa, rais haijui kwa hiyo tusilipe deni kwa kitu ambacho hata mkuu wa nchi hakijui.
 
The reality is now open. DR. SLAA NI MUONGO WA KARNE. i hate to have such political leaders. They are dangerous to Tanzanians.

Mtalia sana mwaka huu.

Mtakabwa mpaka penati mkose pa kutokea. CCM is collapsing slowly.
 

Pamoja na ulaku wa fisi, hata kama atakufa kwa njaa kamwe hawezi kula mguu/mkono wake. Kukataa kata kata kwa JK kuwa hauijui DOWANS na wamiliki wake ndicho kinachoonyesha hoja ya Dr. Slaa kuwa JK anaimiliki "by implication". Sasa atawafahamu vipi? si sawa na fisi aliyezidiwa na kuhamua kula mkono?
 
Kweli mambo ni magumu sana... Ccm wameanza kuchakachua watoto kwa pilau na juici ya azam..

Jk anaongea pumba badala ya kuweka wazi kuwa ameshashindwa nchi na anachohitaji ni mawazo ya jinsi ya kutengeneza nchi mpya..
 
JK kutokujua mmiliki wa Dowans anajaribu kumlaghai nani? Hii ni hatari!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…