Dr. Slaa: Kikwete mmiliki wa DOWANS...

Kinachonishangaza, kunisikitisha na kunifadhaisha ni kuwa bado kuna watu miongoni mwetu Watanzania wenye ujasiri wa kumtetea Jakaya Mrisho Kikwete ! Duh !
Wengi wa type ya DSM hawaoni madudu ya mtu yeyote, ilimradi tu ni wa deen yao! Majuha hawa na si wazalendo
 
Mwisho wao umekaribia. Tena ni baada ya kuanza bunge vinginevyo mshauri wake asome majira ya nyakati.
 
Soma vizuri anachoongea Slaa, usitake ligi hujaelewa bado. Tatizo ukishakuwa shabiki wa CCM, akili ya kufikiri kidogo tu inakosekana.
 

- Wananchi wamewaongeza wabunge wengi Upinzani, lakini bado wakachagua majority wabunge wa CCM, ni FACT it has nothing to do na anything na ni wabunge wa CCM ambao ni majority bungeni, ndio wenye kauli ya mwisho kuhusu ishu zote muhimu za taifa na ndio Demokrasia yenyewe.

William.
 

Dr Slaa anajua 'kuua nyani hakuna kuangalia usoni'
'Nyani wote' wanaolifilisi taifa kama shamba la bibi, lazima Dr Slaa kuwawahi kabla ya shamba la wananchi kuachwa tuvune mabua badala ya mavuno ambayo 'nyani' wamekuwa wakijigawia kwa uozo wa mikataba feki ya kifisadi na hila.

Tunaomba kama JK mwanaume wa kweli, ajitokeze akanushe kuwa sio kinara wa DOWANS na 'mzazi' wake yaani Richmond-uli.

Tukumbuke kuwa kukubalika wa Richmond - kulingana na Tume ya Mwakyembe na kuthibitishwa na Lowassa mwenyewe pamoja na Mkuu wa TIC -Ole Naiko wa kituo cha uwekezaji, ni kuwa ilikuwa 'order toka juu' kwa Lowassa kwa 'kimemo' alichomwamuru Ole Naiko -kwa ajili ya 'dharura iliyokuwepo' aruhusu Richmond 'ikabidhiwe kazi' kuondoa tatizo la umeme.

ANGALIZO: Tukumbuke yafuatayo:
* Lowassa alipotoa order alikuwa ikulu - kwa Waziri Mkuu, na Rais ni uzio mmoja wa ikulu na hivyo maamuzi hayo yalikuwa ni ya JK mwenyewe kupitia Lowassa. Jibu liko wazi hapa.

* JK alishasema EL ni mtendaji wake makini na hadi leo anasikitika kumkos alipojiuzulu. Jibu tunalipata tena hapa.

* Tuliambiwa ktk Tume, wahusika ktk kuileta Richmond ni RA na Jamaa anaitwa N. Gire. Na kiukweli JK, EL na RA ni partners na marafiki wa kufa mtu. Jibu hapa tunalo.

* Tukumbuke mbali na shida zote ambazo Richmond na Dowans yameleta kwa Watanzania, wakati wa kampeni JK alipoenda kumnadi ELalisema tena kuwa EL ni mtendaji mahiri ambaye amekumbwa tu na bahati mbaya na JK anamjutia kumkosa ktk utawala wake. Jibu lipo wazi hapa.

Hivyo kwa kujumuisha hayo yote na msururu wa mengine ambayo hatuwezi ku-list hapa, tunapata jibu moja la hakika (formula) kuwa EL + RA + JK = Richmond & Dowans.

....for Gods sake, iokoe nchi yetu na 'ukungu' huu ee Mwenyezi.
 

Unauhakika gani kuwa riport zao zinafanyiwa kazi? inawezekana kabisa wanayempelekia taarifa na ushauri wao ni MR know it all. Hapo utawalaumu wao vipi?
 
Katiba si iko juu ya mihimili yote. Ukiamua kutumia tu bunge hutawakilisha mawazo ya Watanzania wote. Hata ukiangalia idadi ya waliopiga kura ni Watanzania wachache sana. Nadhani Dr Slaa yu sahihi kabisa.

- Katiba inasema waliopiga kura wanatosha kuwakilisha wananchi wote wa Tanzania, na kwenye uchaguzi ulioisha wapiga kura wameongeza wabunge wengi wa Upinzani bungeni, lakini wamechagua majority kuwa CCM, until katiba itakapobadilishwa kuhusu udadi ya wapiga kura uchaguzi ulioisha ni valid kwa mujibu wa katiba ya sasa.

William.
 
Kinachonishangaza, kunisikitisha na kunifadhaisha ni kuwa bado kuna watu miongoni mwetu Watanzania wenye ujasiri wa kumtetea Jakaya Mrisho Kikwete ! Duh !

- Tunatetea principle na haki ya wananchi wengi walioichagua CCM as majority bungeni, hatetewi Rais hapo.

William.
 

- Mkuu tujadili mada iliyoko mbele yetu ya kwetu binafsi hayana nafasi hapa, vipi huna hoja kuhusu mada?

William.
 
W. J Malecela, je, kila wanachopitisha Wabunge wa CCM Bungeni ndio matakwa/maoni/mapenzi ya wananchi kwa kuwa tu wamechaguliwa katika uchaguzi wa vyama vingi unaoendeshwa kwa Demokrasia ya Kiliberali? Kwa mfano, je, maamuzi yote kuhusu Richmond na Dowans yaliyofanywa na Bunge baada ya Dkt Mwakyembe kuwasilisha hotuba ya Kamati yake kwa mbwembwe nyingi zilizopelekea kujiuzulu kwa Lowassa ndio maamuzi ya Watanzania wanaotesekana na mgawo wa umeme? Na, je, una maoni gani kuhusu 'Tyranny of the Majority', yaani, 'Udikteta wa Walio Wengi'?
 
 

- Mkuu rudi nyuma ukaone nilipoanzia, nimesema hivi wabunge wengi wa CCM wamechaguliwa na wananchi wengi kwa hiyo kama kuna ishus za katiba zitaenda kuwa approved bungeni, then CCM itakua na the upperhand ya kuamua kwa sababu ina wabunge wengi waliochaguliwa na wananchi wengi hivyo wanawakilisha mawazo ya wananchi wengi, I hope umenielewa hapo mkuu!

William.
 

Wewe ndiye unayetuaacha hoi yawezekana hujui nini matwakwa ya wananchi walio wengini wa tanzania na hasa walalahoi, acha mafisadi ambao pengine wewe ndio unawasemea kama si mmoja wao.
 

Lakini mabadiliko ya Kikatiba hufanywa na Bunge Maalumu (Constitutional Assembly) ama?
 
Wewe ndiye unayetuaacha hoi yawezekana hujui nini matwakwa ya wananchi walio wengini wa tanzania na hasa walalahoi, acha mafisadi ambao pengine wewe ndio unawasemea kama si mmoja wao.

- Nje ya mada mkuu, na sina muda wa kupoteza!, halafu ni heshima tu kwa Dr. Slaa ndio maana sikuichambua post nzima., otherwise rudi kwenye mada kama unaweza tuelimishane!

William.
 

Huwezi kujustify ushindi wowote walioupata wagombea wa CCM, kote ktk Urais, Ubunge na hadi Udiwani ni wizi mtupu. Hata Makongoro jana amewaambia vijana na ktk mkesha kuwa vijana wameiadhibu CCM, imekwama kila mahali na hata pale iliposhinda 'ilipita kwa mbinde'. Hili ni jibu kwako unafikiri kila wakati kuwa CCM ilishinda kihalali! La hasha. Ni wizi + NEC + UWT + Ufisadi, ndio unapata CCM na wewe unapoteza nguvu kutetea hili eti wabunge CCM ni 'majority'? You must have somethg wrong kichwani hapo!
Badilika, tetea wananchi na taifa ili likuenzi. Acha kutetea utupu na nonsense majority! Pole sana.
 

- Unajua ni muda sasa unatumia sana matusi na lugha chafu kujaribu kuninyamazisha mtu ambaye unaamini kichwa changu hakiko sawa, sasa wenye vichwa sawa watapata taabu sana kuamini mwenye kichwa sawa kama wewe akipoteza muda mwingi kushindana na mwenye kichwa kisicho sawa kama changu, ha! ha! ha!

- Well, lets say kichwa chako ni sawa sana, nielmishe katiba mpya yenye mawazo ya Dr. Slaa na Chadema tu itaipitishia bunge lipi hilo? Maana la sasa kwa mujibu wa katiba yetu, CCM ndio majority! ha! ha! ha! lol!


William
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…