Dr. Slaa: Kikwete mmiliki wa DOWANS...

Dr. Slaa: Kikwete mmiliki wa DOWANS...

Kinachonishangaza, kunisikitisha na kunifadhaisha ni kuwa bado kuna watu miongoni mwetu Watanzania wenye ujasiri wa kumtetea Jakaya Mrisho Kikwete ! Duh !
Wengi wa type ya DSM hawaoni madudu ya mtu yeyote, ilimradi tu ni wa deen yao! Majuha hawa na si wazalendo
 
Mwisho wao umekaribia. Tena ni baada ya kuanza bunge vinginevyo mshauri wake asome majira ya nyakati.
 
- Ligi ya mchangani ni pale one anaposhindwa kuelewa kwamba CCM ina wabunge wengi waliochaguliwa na wananchi wengi, maana yake ni kwamba wao ndio wenye upperhand ya nini kibadilishwe na nini kisibadilishwe, unless hiyo katiba mpya ikatengenezewe nje ya bunge, against katiba ya Jamhuri.

- Haya wala sihitaji kufikiria sana kabla ya kuandika na wala hakuna haja ya ligi, maana ni kukimbiza upepo!


William.
Soma vizuri anachoongea Slaa, usitake ligi hujaelewa bado. Tatizo ukishakuwa shabiki wa CCM, akili ya kufikiri kidogo tu inakosekana.
 
Unategemea nini wakati rais Mwizi anapokuwa na shauku ya kuwaibia walipa kodi hata kile kidogo walichonacho. JK anafahamu wazi kwamba hakushinda urais hivyo alitumia mbinu zile zile za Wizi wa kura na kufikiri atakaa raha mustarehe, safari hii Wadanganyika wanasema No hatoki mtu hapo hadi kieleweke. Ukiiba unadanganya na njia ya mwongo ni fupi.

Msione makuwadi wengi wanaingia hapa na ngozi za kondoo na kusema ati Chama Cha Majambazi kilichaguliwa na wananchi au wabunge wengi wanakubalika na wananchi huu ni ulaghai kwa sababu wengi wao wametumwa/wanalipwa kuja kufunika kombe hapa ili mwanaharamu apite wanakumbana na visiki kwa sababu Tanzania ya leo sio ile ya jana iliyolala. Muulizeni JK alikwenda USA kufanya nini kama sio kuhamisha fweza za walipa kodi? Maajar baada ya kumtajirisha sana JK pale London alipelekwa USA strategically kwa kazi hiyo.


Kama kweli JK sio mmiliki wa Dowans aseme hadharani na mwenye Dowans Wadanganyika wanasema hawatamlipa hata akienda Jehanam.

- Wananchi wamewaongeza wabunge wengi Upinzani, lakini bado wakachagua majority wabunge wa CCM, ni FACT it has nothing to do na anything na ni wabunge wa CCM ambao ni majority bungeni, ndio wenye kauli ya mwisho kuhusu ishu zote muhimu za taifa na ndio Demokrasia yenyewe.

William.
 
Gazeti la Tanzania Daima la leo linatuhabarisha ya kuwa Dr. Slaa anamtuhumu JK ndiye mmilki halali wa DOWANS......................hili likiashiria ya kuwa kumbe kashfa nzima ya ufisadi dhidi ya watanzania ilisukwa na kuiva hapo Ikulu chini ya uangalizi mahiri, madhuuti na makini wa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania...............................je kweli tutafikika kwa hali hii?.................

Vile vile Dr Slaa anamtuhumu JK kuwa ni muasisi wa kasfa za IPTL................na ya kuwa hana nia ya dhati ya kuandika katiba mpya ila anatutupia changa la moto..........................................



Slaa: JK anamiliki Dowans


 Asema hana nia ya kuunda Katiba mpya

na Mwandishi wetu


amka2.gif
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dk. Willbrod Slaa amesema kuwa Rais Jakaya Kikwete ni dikteta.
Akizungumza na Tanzania Daima Jumapili, Dk. Slaa, alisema kitendo cha Rais Kikwete, kutangaza kuwa ameunda tume ya kuanzisha mchakato wa uundwaji wa Katiba mpya na atateua kiongozi na wajumbe kinaashiria kuendeleza udikteta wa uongozi.
Alibainisha kinachotakiwa kuanzishwa hivi sasa ni Constitutional Assembly au Baraza la Katiba (Bunge la Katiba) ambalo ndilo litakalokuwa na wajibu wa kuratibu kura za maoni ya wananchi juu ya uundwaji wa Katiba mpya.
Alisema kitendo cha Rais Kikwete, kutangaza kuunda tume ni kiini macho na kinadhihirisha hana nia ya kutaka kuundwa kwa Katiba mpya.
"Huyu Rais wetu haonyeshi kama yuko 'serious' katika uundaji wa Katiba mpya, anataka kuweka viraka ili aendelee kututawala kidikteta!" alisema.
Aliongeza kuwa kwa kawaida Baraza la Katiba ambalo hapa nchini halipo ndilo lenye jukumu hilo na linatakiwa lifanye mchakato huo kwa kuishirikisha serikali, Bunge, wadau na wananchi.
Alisema hakubaliani na tume ya kuratibu mchakato huo, kwani inaweza kufanya kazi kwa utashi wa aliyewateua na hata Bunge pia linaweza likatumbukia kwenye mtego wa kupitisha kitu kisichokuwa matakwa ya wananchi kwa sababu ya wingi wa wabunge wa chama kimoja.
Alisema katika nchi zote zilizoandika upya Katiba au kutengeneza zilipitia njia ya 'National Constitutional Congress au Convention' (Constitutional Assembly) ambapo ilikubaliwa kati ya serikali, Bunge, wadau mbalimbali na wananchi katika majukwaa yao.
"Constitutional Congress ni chombo kitakachoratibu maoni ya wananchi na wadau mbalimbali na siyo mtu aliyeteuliwa na Rais ambaye anafanya kazi kwa ajili ya kumfurahisha jambo ambalo ni kuendelea kuweka viraka" alisema.
Alisema baada ya chombo hicho kuundwa, maoni ya wadau, wananchi mbalimbali hukusanywa kwa njia itakayokubalika.
Dk. Slaa alisema kuwa 'Constitutional Congress hukaa tena kupitia maoni yote kipengele kwa kipengele na kukubaliana na siyo Rais Kikwete na tume atakayounda jambo ambalo liliwahi kutokea huko nyuma.
Alisema inawezekana Rais Kikwete, hafahamu au kwa makusudi amepuuza kilio cha wananchi ndiyo maana ameunda tume inayowajibika kwa maslahi yake.
Alisema kuwa Katiba siyo mali ya Rais wala ya serikali iliyoko madarakani, bali ni mali ya wananchi.
Dk. Slaa alisema wananchi wanatakiwa kufahamu kuwa wanahitaji chombo chao ambacho kinaweza kuwekewa utaratibu na Bunge, baada ya kupitishwa na Azimio la Bunge, lakini siyo mtu au watu wa tume wanaochaguliwa na Rais.
"Tume hiyo haikubaliki kabisa tunachotaka tunajua hakitakubalika kwa maana hakuna serikali duniani itakayounda tume ya kujinyonga yenyewe, mabadiliko makubwa kwa vyovyote, hayakupendwa na serikali iliyoko madarakani" alisema.
Alisema ana imani kuwa tume hiyo haiwezi kuleta Katiba mpya hivyo kutoa nafasi kwa Rais Kikwete kuendelea kuongoza katika sura ya kidikteta kwa kupitia Katiba ya sasa iliyopitwa na wakati.
Dk. Slaa alisema kuwa inashangaza katika hili ambapo hata Zanzibar wamepiga hatua kwani waliweza kuruhusu kukusanya maoni ya uundaji wa serikali ya kitaifa na si kuundwa kwa tume.
Alisema Katiba mpya haiwezi kamwe kupatikana kwa njia ya tume hiyo (Constitutional Review Commission) kwani zilishawahi kutokea tume za aina hiyo na hakuna kilichofanyika.
Alibainisha kuwa jambo hilo halina tofauti na tume zilizowahi kuundwa na Rais Mstaafu Ally Hassan Mwinyi pamoja na ile ya Benjamin Mkapa ambapo matokeo yalikuwa ni kuweka viraka kwenye Katiba tuliyonayo hivi sasa.
"Uzoefu wa Tume za Mwinyi na Mkapa ni kuwa maoni yalikusanywa kwa upendeleo, hojaji zilipelekwa kwenye matawi ya CCM, halmashauri za wilaya vyombo ambavyo vyote ni vya CCM, hatimaye serikali ikatoa mapendekezo ya vifungu vya kurekebishwa na vingine kuachwa, alisema na kuongeza: "hatua hii inawezekana kwa kuwa tume ni ya Rais, na Rais kama alivyosema mwenyewe ndiye atakayepeleka marebisho kwa vyombo husika (Bunge) ambalo karibu lote ni la CCM bado wana wabunge wengi pamoja na kuwa wapinzani wameongezeka sana" alifafanua.
Katika hatua nyingine, Dk. Slaa alisema ameshangazwa na kitendo cha Rais Kikwete kushindwa kufafanua kuhusu suala la kulipwa kwa Kampuni ya Dowans sh bilioni 185 na Shirika la UmemeTanzania (TANESCO).
Alisema fidia hiyo iliyoamriwa na mahakama ya kimataifa ya usuluhishi wa migogoro ya biashara (ICC) hivi karibuni kuwa TANESCO inapaswa iwalipe Dowans fedha hizo baada ya kuvunja mkataba wa kununua umeme.
Alisema kimsingi uvunjwaji wa mkataba huo na sakata zima ni uzembe ambao unapaswa uwekwe wazi na watu wachukuliwe hatua lakini Rais Kikwete haonyeshi kushtushwa na jambo hilo.
Alisema kutokana na majibu ya kiongozi huyo inaonyesha kuwa naye ni sehemu ya kampuni ya Dowans.
Alisema Rais anaonyesha udikteta kwa kuamua kulibeba shirika la umeme nchini (TANESCO) huku wananchi ambao ni walalahoi wakiendelea kunyongwa na upandaji wa gharama hizo.
"Hasemi kuwa kitendo cha kulipa kampuni hiyo kimesababishwa na uzembe wao wenyewe kwa kuleta mitambo ya Richmond iliyozaa Dowans huku yeye akiwa sehemu ya kampuni hizo ameamua kuficha uovu wao" alieleza.
Alisema wataendelea kuhamasisha maandamano pamoja na kupinga gharama kwa kuwa vyama vya upinzani havikusajiliwa kwa Rais bali vimekuwepo kwa mujibu wa sheria ili kuhakikisha vinakataa uozo unaofanywa na serikali.
Dk. Slaa alisema Rais Kikwete amesahau hali ngumu inayowakumba wananchi imetokana na maamuzi mabovu yaliyoanzishwa na wanasiasa wenzake kwa kukubali kufanya mchakato wa IPTL.
"Eti Rais Kikwete anasema upandaji wa umeme ni suala la kibiashara na wanasiasa wasilizungumzie kisiasa inawezekana hana uchungu na Watanzania wanaoshindwa kununua umeme kwa ajili ya kuendeleza biashara zao" alisema.
Alisema vyama vya upinzani vina haki ya kujadili masuala mbalimbali na siyo kama anavyodai kufanya hivyo ni kuendeleza malumbano na ikiwa hataki vyama vifanye hivyo basi hana budi kuvifuta.
Wakati huo huo Chama cha Wananchi (CUF), kimemtaka Rais Jakaya Kikwete, kutekeleza kwa vitendo ahadi yake aliyoitoa juu ya kupata Katiba mpya itakayokuwa na maslahi ya Watanzania wote.
Naibu Katibu Mkuu wa CUF, bara, Julius Mtatiro, alisema kuwa kitendo cha Rais Kikwete, kukubali kuundwa kwa Katiba mpya kuendane na vitendo hasa kuiunda upya na sio kuifanyia marekebisho kama ilivyokuwa awali.
Alisema Tanzania imefanya marekebisho mara 14 lakini bado kumekuwa na malalamiko hali inayoweza kuleta machafuko nchini na kuipa nchi doa.
Alisema ni kipindi kizuri kwa Rais Kikwete kuiga mfano wa Rais wa Zanzibar wa awamu ya sita Amani Karume kwa kuridhia maridhiano yaliyoleta sura mpya ya Zanzibar.
Alisema suala la Katiba mpya limekuja wakati muafaka, kabla ya kutokea kwa misukosuko inayoweza kuchafua hali ya utulivu na amani ya nchi hatua itakayofanya kupoteza sifa hasa pindi amalizapo muda wake mwaka 2015.
Hata hivyo chama hicho kilimtahadharisha Rais Kikwete kuhakikisha anatembea katika kauli zake hasa kwa kuunda tume makini itakayokuwa huru na isiyokuwa na upendeleo au agenda ya kuibeba CCM, hasa kwa kufanya maamuzi ya upande mmoja.
Aidha katika hotuba yake Rais Kikwete aliahidi kuunda Tume Maalum ya Katiba (Constitutional Review Commission), itakayoratibu mchakato kwa kushirikisha wananchi wote ili waweze kutoa maoni yao juu ya yale wanayotaka yaingizwe katika Katiba mpya.

Dr Slaa anajua 'kuua nyani hakuna kuangalia usoni'
'Nyani wote' wanaolifilisi taifa kama shamba la bibi, lazima Dr Slaa kuwawahi kabla ya shamba la wananchi kuachwa tuvune mabua badala ya mavuno ambayo 'nyani' wamekuwa wakijigawia kwa uozo wa mikataba feki ya kifisadi na hila.

Tunaomba kama JK mwanaume wa kweli, ajitokeze akanushe kuwa sio kinara wa DOWANS na 'mzazi' wake yaani Richmond-uli.

Tukumbuke kuwa kukubalika wa Richmond - kulingana na Tume ya Mwakyembe na kuthibitishwa na Lowassa mwenyewe pamoja na Mkuu wa TIC -Ole Naiko wa kituo cha uwekezaji, ni kuwa ilikuwa 'order toka juu' kwa Lowassa kwa 'kimemo' alichomwamuru Ole Naiko -kwa ajili ya 'dharura iliyokuwepo' aruhusu Richmond 'ikabidhiwe kazi' kuondoa tatizo la umeme.

ANGALIZO: Tukumbuke yafuatayo:
* Lowassa alipotoa order alikuwa ikulu - kwa Waziri Mkuu, na Rais ni uzio mmoja wa ikulu na hivyo maamuzi hayo yalikuwa ni ya JK mwenyewe kupitia Lowassa. Jibu liko wazi hapa.

* JK alishasema EL ni mtendaji wake makini na hadi leo anasikitika kumkos alipojiuzulu. Jibu tunalipata tena hapa.

* Tuliambiwa ktk Tume, wahusika ktk kuileta Richmond ni RA na Jamaa anaitwa N. Gire. Na kiukweli JK, EL na RA ni partners na marafiki wa kufa mtu. Jibu hapa tunalo.

* Tukumbuke mbali na shida zote ambazo Richmond na Dowans yameleta kwa Watanzania, wakati wa kampeni JK alipoenda kumnadi ELalisema tena kuwa EL ni mtendaji mahiri ambaye amekumbwa tu na bahati mbaya na JK anamjutia kumkosa ktk utawala wake. Jibu lipo wazi hapa.

Hivyo kwa kujumuisha hayo yote na msururu wa mengine ambayo hatuwezi ku-list hapa, tunapata jibu moja la hakika (formula) kuwa EL + RA + JK = Richmond & Dowans.

....for Gods sake, iokoe nchi yetu na 'ukungu' huu ee Mwenyezi.
 
Haha now you are talking. Bonge umesema sawia kabisa. Usalama wa Taifa si usalama wa taifa, ni usalama wa CCM, and to be more specific na wa baadhi ya watu ndani ya CCM. Ukiangalia issue nzima ya umeme kwa Tanzania, inaweza kuwa ni moja ya top prioroties za usalama wa Taifa, lakini angalia jinsi Usalama wa taifa wenyewe wanavyoiangalia na kuishughulikia, si prioroties kabisa. I can not believe tunarudia tena ujinga uleule tuliou-face wakati wa Richmond, kama kweli uslama wa taifa wangefanya kazi yao tusingekuwa na tatizo hili.

Unauhakika gani kuwa riport zao zinafanyiwa kazi? inawezekana kabisa wanayempelekia taarifa na ushauri wao ni MR know it all. Hapo utawalaumu wao vipi?
 
Katiba si iko juu ya mihimili yote. Ukiamua kutumia tu bunge hutawakilisha mawazo ya Watanzania wote. Hata ukiangalia idadi ya waliopiga kura ni Watanzania wachache sana. Nadhani Dr Slaa yu sahihi kabisa.

- Katiba inasema waliopiga kura wanatosha kuwakilisha wananchi wote wa Tanzania, na kwenye uchaguzi ulioisha wapiga kura wameongeza wabunge wengi wa Upinzani bungeni, lakini wamechagua majority kuwa CCM, until katiba itakapobadilishwa kuhusu udadi ya wapiga kura uchaguzi ulioisha ni valid kwa mujibu wa katiba ya sasa.

William.
 
Kinachonishangaza, kunisikitisha na kunifadhaisha ni kuwa bado kuna watu miongoni mwetu Watanzania wenye ujasiri wa kumtetea Jakaya Mrisho Kikwete ! Duh !

- Tunatetea principle na haki ya wananchi wengi walioichagua CCM as majority bungeni, hatetewi Rais hapo.

William.
 
Mr. President, huyo William hajakuelea bado, let me assist you,.... shika chini
ww William, angalia mbele kuleeee, umezoea kufeli, shikaaaaView attachment 19536 siku nyingine use u r brain to control u r mouth & not mouth to control u r brain, mboko 30 hadi ukome

- Mkuu tujadili mada iliyoko mbele yetu ya kwetu binafsi hayana nafasi hapa, vipi huna hoja kuhusu mada?

William.
 
W. J Malecela, je, kila wanachopitisha Wabunge wa CCM Bungeni ndio matakwa/maoni/mapenzi ya wananchi kwa kuwa tu wamechaguliwa katika uchaguzi wa vyama vingi unaoendeshwa kwa Demokrasia ya Kiliberali? Kwa mfano, je, maamuzi yote kuhusu Richmond na Dowans yaliyofanywa na Bunge baada ya Dkt Mwakyembe kuwasilisha hotuba ya Kamati yake kwa mbwembwe nyingi zilizopelekea kujiuzulu kwa Lowassa ndio maamuzi ya Watanzania wanaotesekana na mgawo wa umeme? Na, je, una maoni gani kuhusu 'Tyranny of the Majority', yaani, 'Udikteta wa Walio Wengi'?
 
Huyu ndiye Msomi kuliko wote Tz, Dr..Dr...Dr....Dr..........JK. We don't wan't him anymore bcoz he thrusted us when we trusted him.

Bwana wee rahisisha tu kwa kusema mh Dr mara 5.........Halafu utakuwa unabadilisha namba kadiri atakavyokuwa anaomba kutunikiwa uDr.

 
W. J Malecela, je, kila wanachopitisha Wabunge wa CCM Bungeni ndio matakwa/maoni/mapenzi ya wananchi kwa kuwa tu wamechaguliwa katika uchaguzi wa vyama vingi unaoendeshwa kwa Demokrasia ya Kiliberali? Kwa mfano, je, maamuzi yote kuhusu Richmond na Dowans yaliyofanywa na Bunge baada ya Dkt Mwakyembe kuwasilisha hotuba ya Kamati yake kwa mbwembwe nyingi zilizopelekea kujiuzulu kwa Lowassa ndio maamuzi ya Watanzania wanaotesekana na mgawo wa umeme? Na, je, una maoni gani kuhusu 'Tyranny of the Majority', yaani, 'Udikteta wa Walio Wengi'?

- Mkuu rudi nyuma ukaone nilipoanzia, nimesema hivi wabunge wengi wa CCM wamechaguliwa na wananchi wengi kwa hiyo kama kuna ishus za katiba zitaenda kuwa approved bungeni, then CCM itakua na the upperhand ya kuamua kwa sababu ina wabunge wengi waliochaguliwa na wananchi wengi hivyo wanawakilisha mawazo ya wananchi wengi, I hope umenielewa hapo mkuu!

William.
 
- Wakati mwingine Dr. Slaa huwa ananiacha hoi sana, I mean wabunge wengi wa CCM wamechaguliwa na nani kama sio wananchi wengi?, sasa watapitishaje matakwa yasiyo ya wananchi wengi wakati sio siri kwamba wabunge wengi wa CCM wamechaguliwa na wananchi wengi!

- I m missing something hapa au what?


William.

Wewe ndiye unayetuaacha hoi yawezekana hujui nini matwakwa ya wananchi walio wengini wa tanzania na hasa walalahoi, acha mafisadi ambao pengine wewe ndio unawasemea kama si mmoja wao.
 
- Mkuu rudi nyuma ukaone nilipoanzia, nimesema hivi wabunge wengi wa CCM wamechaguliwa na wananchi wengi kwa hiyo kama kuna ishus za katiba zitaenda kuwa approved bungeni, then CCM itakua na the upperhand ya kuamua kwa sababu ina wabunge wengi waliochaguliwa na wananchi wengi hivyo wanawakilisha mawazo ya wananchi wengi, I hope umenielewa hapo mkuu!

William.

Lakini mabadiliko ya Kikatiba hufanywa na Bunge Maalumu (Constitutional Assembly) ama?
 
Wewe ndiye unayetuaacha hoi yawezekana hujui nini matwakwa ya wananchi walio wengini wa tanzania na hasa walalahoi, acha mafisadi ambao pengine wewe ndio unawasemea kama si mmoja wao.

- Nje ya mada mkuu, na sina muda wa kupoteza!, halafu ni heshima tu kwa Dr. Slaa ndio maana sikuichambua post nzima., otherwise rudi kwenye mada kama unaweza tuelimishane!

William.
 
- Mkuu rudi nyuma ukaone nilipoanzia, nimesema hivi wabunge wengi wa CCM wamechaguliwa na wananchi wengi kwa hiyo kama kuna ishus za katiba zitaenda kuwa approved bungeni, then CCM itakua na the upperhand ya kuamua kwa sababu ina wabunge wengi waliochaguliwa na wananchi wengi hivyo wanawakilisha mawazo ya wananchi wengi, I hope umenielewa hapo mkuu!

William.

Huwezi kujustify ushindi wowote walioupata wagombea wa CCM, kote ktk Urais, Ubunge na hadi Udiwani ni wizi mtupu. Hata Makongoro jana amewaambia vijana na ktk mkesha kuwa vijana wameiadhibu CCM, imekwama kila mahali na hata pale iliposhinda 'ilipita kwa mbinde'. Hili ni jibu kwako unafikiri kila wakati kuwa CCM ilishinda kihalali! La hasha. Ni wizi + NEC + UWT + Ufisadi, ndio unapata CCM na wewe unapoteza nguvu kutetea hili eti wabunge CCM ni 'majority'? You must have somethg wrong kichwani hapo!
Badilika, tetea wananchi na taifa ili likuenzi. Acha kutetea utupu na nonsense majority! Pole sana.
 
Huwezi kujustify ushindi wowote walioupata wagombea wa CCM, kote ktk Urais, Ubunge na hadi Udiwani ng wizi mtupu. Hata Makongoro jana amewaambia vijana na ktk mkesha kuwa vijana wameiadhibu CCM, imekwama kila mahali na hata pale iliposhinda 'ilipita kwa mbinde'. Hili ni jibu kwako unafikiri kila wakati kuwa CCM ilishinda kihalali! La hasha. Ni wizi + NEC + UWT + Ufisadi, ndio unapata CCM na wewe unapoteza nguvu kutetea hili eti wabunge CCM ni 'majority'? You must have somethg wrong kichani hapo!
Badilika, tetea taifa ili likuenzi. Acha kutetea utupu na nonsense majority! Pole sana.

- Unajua ni muda sasa unatumia sana matusi na lugha chafu kujaribu kuninyamazisha mtu ambaye unaamini kichwa changu hakiko sawa, sasa wenye vichwa sawa watapata taabu sana kuamini mwenye kichwa sawa kama wewe akipoteza muda mwingi kushindana na mwenye kichwa kisicho sawa kama changu, ha! ha! ha!

- Well, lets say kichwa chako ni sawa sana, nielmishe katiba mpya yenye mawazo ya Dr. Slaa na Chadema tu itaipitishia bunge lipi hilo? Maana la sasa kwa mujibu wa katiba yetu, CCM ndio majority! ha! ha! ha! lol!


William
 
Back
Top Bottom