Elections 2010 Dr. Slaa kumuwekea pingamizi Kikwete!

Ngoja niandae 'bisi' za kutosha!
 
Huyu ni kibaraka. Kapewa kula na kikwete, unadhani ana ubavu? washikaji msitegemee miujiza. wote hao wasanii tu.
Mi nashauri vya vijipange kulinda kura baada 31/10/2010 make ccm watakuwa na kura kiduchu
 

Nina kerwa sana na UDINI WENU matawafukuza watu wengi sielewi kwanini mnaweka dini mbele kuliko maslahi ya nchi....

If you can't fight them join them
 
Ee Mungu,
Weka mkono wako hapa ili haki itendeke!!!!:confused2:
 
KWeli baadhi ya waTZ wana roho mbaya kushinda simba ambaye akimkamata mnyama anamla,lakini baadhi ya watz wapo sawa na kobla(nyoka) ambaye yeye anajisikia raha kutema mimate na kudonoa watu bila kula!
Yaani mijitu inakasirika wafanyakazi kuongezewa mishahara wakati wenyewe mlishasema wafanyakazi kura zao kwa padri sasa yamegeuka nini?Yaani mnakuwa vigeugeu kama kinyonga!Acheni roho mbaya kwasababu wafanyakazi wameongezewa mishahara,nanyi mkitaka kafanyeni kazi serikalini ili muongezewe hivyo vijimishahara.Wafanyakazi wanajua wa kumpa kura kama Padri,Jk,Lipumba n.k
 
kwa hili nadhani kinachoonekana ni kwamba hii issue ni very serious kwani kuna mgongano wa tafsiri ya mswaada wenyewe.Kikubwa pengine na sisi wananchi tujilizishe kwa kuusoma.Jamani kama kuna mtu anao naomba aupost tujaribu kuamua pengine sheia ikikwepeshwa tuweze kupaza sauti.
 
Hivi ile mishahara Kikwete aliyoahidi Mwanza imeshatoka, kama haijatoka basi rais ni mwongo na kama imetoka basi Kinana mwongo. Either of the two answers CCM watakuwa wamebanwa tu, kwa sababu kama mishahara imetoka mwezi huu basi Kikwete kakiuka sheria ya uchaguzi na kama haijatoka vile vile wanalo kwa kuwadanganya wafanyakazi. Kwahiyo iliyobaki kwao ni kuchagua bega ila safari iko pale pale.
 
Nina kerwa sana na UDINI WENU matawafukuza watu wengi sielewi kwanini mnaweka dini mbele kuliko maslahi ya nchi....

If you can't fight them join them
Hebu rejea ktk post yangu unioneshe hicho kitu kinachoitwa UDINI
Naona wehu umekukamata sawia mzee.
 
kidini!? Nasikia JK ni mmoja wa watu walio lelewa kwa maadiri ya kikristo na hata hiyo elimu aliyo nayo ni kanisa ndiyo lilimsaidia kufika hapo alipo ni kweli
 
Haaa haaa

Unajiweka Pembeni Mkuu?
Unaogopa Msongamano?

Bora utulie utafute Po-Corn ule . . . .

Najaribu 'kuota' jinsi itakavyokuwa kama Tendwa atam-disqualify Kikwete kwenye kinyang'anyiro cha urais! Hapo ndio mtakapomjua kwamba aliwahi kuwa Luteni Kanali (Lieutenant-Colonel)!
 

think before you reap,have you you gone through mswaada?
 
Soini uhusiano wowote wa post yako na topic hii hapa tunaongelea sheria zimekiukwa wewe unaongelea roho mbaya, hata kama JK amefanya vizuri kuongeza mishahara lakini kakiuka sheria. Ni sawa na kuiba chakula cha mtoto wa jirani kumpa mtoto wako ni sawa lakini umefanya kosa simple.
 
Mhhhhhhhhhhhhhhhhhh. Anahitaji siku tano za kupindisha sheria!! Chadema wajiandae na nyaraka za kuthibitisha madai yao, hasa zile nyaraka za kuzuia kutamka hadharani mishahara ya wafanyakazi wa serikali. Upo waraka wa siri unaozungumzia jambo hilo. Ila sijui kama umetamka nini kuhusu mamlaka ya Rais kama anaweza revoke hiyo siri ikawa public?
 
Utakerwa sana mwaka huu. Na kibaya zaidi ni kuwa John Tendwa ni MKRISTO, heheheeee. Na kwenye NEC kuna Jaji Lewis Makame.

Muislaam mwenzio atapata aisee nyingine, MDINI WEEE................
Nina kerwa sana na UDINI WENU matawafukuza watu wengi sielewi kwanini mnaweka dini mbele kuliko maslahi ya nchi....

If you can't fight them join them
 

chadema mtu akiwa unga juu ya lao huwa makini. lakini akiwaambia hili hapana na mnavyofikiria nyinyi basi hapo huwa hana akili
 
Kumbe hizi methali bado zinamaana NAONA JK ALISHINDWA KABISA KUFIKIRIA HUKU
1) Mchimba kisima kaingia mwenyewe-ALIJUA WAPINZANI NDIO WATAKAO KWAMBA
2) asimamaye angaalie asianguke=ALIJIONA YEYE NA CCM YAKE WAKO IMARA NA JUU YA SHERIA
3) muosha uoshwa=WAMEWAPIGA CHINI WAGOMBEA WENGI WA UPINZANI (CHADEMA) SASA CHADEMA WAMEAMUA KULA KUBWA LAO
4)Asiyesikia la mkuu uona makuu=WATU WALISHAMSHAURI HIYO SHERIA NA MATATIZO YAKE, LAKINI WAPI AKAISAINI KWA MBWEMBWE
5)Kikulacho ki nguoni mwako=mASKINI jK AKUJUA KUWA HIYO SHERIA NDIYO ITAKAYO MLA
6)Hakuna marefu yasiyo na ncha=NADHANI SASA NDIO TUMEFIKIA KILELENI NA HUU NDIO MWISHO WA CCM
7) Mwanamke mzuri akosi kasoro= CCM WALIJIONA WAKO PERFECT NA WAKO MAKINI NA CAMPEN ZAO KUMBE....
8) Barabara ndefu haikosi kona=YAAAAH KWA KWELI
9)
*
*
 

wewe na hao Chadema mnagombea Uhuru? hee uhuru gani huo tuliokuwa hatuna? hivi umesahau kuwa uhuru tumepewa toka 61 na zanzibar 63 na baadae nchi mbili huru zikaungana 64.

nyie oteni tu, semeni tunaganga njaa watu watakuweleweni
 
Pengo acha ushamba huo. kama umechoka au huna la kuchangia acha nenda kalale nyumbani kwako kuliko kutoa hoja chakavu na zisizo na mantiki, usilete ubaguzi wa kidini hapa, tunachoangalia sisi ni maslahi ya Taifa zima na si kuleta usingizi JF, wewe umeona huu ni wakati muafaka kwa mgombea kuongeza mishahara? Kikwete ni mgombea wa CCM na si Taifa, ni mgombea mwenye Chama chake kama walivyo wagombea wengine, ni lazima atofautishe nafasi yake anapokuwa ndani ya chama na nje ya chama, Huu ni wakati wa kampeni na Bunge ndo chombo chenye mamlaka ya kupitisha ongezeko la mishahara, atuambie hilo fungu analotaka kuongeza kalipata wapi? limepitishwa na kuidhinishwa na Bunge gani? Watanzania si watu wa kukaa na kuimbiwa nyimbo za akina Komba, Joti, na upuuzi mwingine ambao unaendelea ktk kampeni, Wanawachekesha watanzania badala ya kuwaeleza sera na mambo waliyoyafanya toka uhuru, acheni kutetea uozo, watu tumenuna tumechoshwa na ahadi za kuku juu ya vifaranga vyake ahadi za kunyonya kesho,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…