Elections 2010 Dr. Slaa mgombea urais 2010 kupitia CHADEMA

Status
Not open for further replies.
Wajipanga kwa urais

Mwandishi Wetu
Mei 21, 2008

Masha, Membe watajwa CCM
Slaa, Hamad kusimama upinzani

MIAKA miwili tu kabla ya Rais Jakaya Kikwete kumaliza kipindi chake cha kwanza mwaka 2010 na huku serikali yake ikiandamwa na kashfa za ufisadi, wanasiasa ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na wale wa upinzani wanajipanga kwa nia ya kujiandaa kushika nafasi hiyo, Raia Mwema imefahamishwa.

Habari zinaeleza kwamba kwa sasa baadhi ya wana CCM wanajenga msingi wa kuwawezesha kumrithi Rais Kikwete katika uchaguzi mkuu ujao lakini wakishindwa, angalau basi kwa uchaguzi mwingine wa 2015; huku wapinzani wao wakipania kuchukua madaraka mwaka 2010, wakitumia kuyumba kwa nchi katika sehemu kubwa ya awamu ya kwanza ya uongozi wa Serikali ya Awamu ya Nne.

Kwa mujibu wa habari hizo, tayari mazungumzo na mikakati imekuwa ikifanyika katika maeneo mbalimbali nchini kwa nia ya kuangalia wanasiasa wanaoweza kushika nafasi ya urais, lakini pia kuwazuia wale ambao wanahofiwa kuweza kuharibu mikakati hiyo.

Wanasiasa kadhaa wakubwa nchini wa sasa, wastaafu na hata wale walioguswa na kashfa, wamekuwa wakitajwa moja kwa moja kujihusisha katika mikakati hiyo ama kwa kupima upepo kama wanaweza kujitokeza wao au kwa kuandaa watu wanaowaunga mkono.

Kwa upande wa upinzani, wanasiasa wapya kabisa wanatajwa kuweza kuibuka na kwa kupishwa na wanasiasa waliogombea katika Uchaguzi Mkuu uliopita, ikiwa ni mkakati unaoelezwa kujaribu kuwavuta wapiga kura wengi.

Imeelezwa kwamba waliogombea katika chaguzi za nyuma ikiwa ni pamoja na ule wa mwaka 2005, kupitia vyama vya upinzani, wanaweza kuwaunga mkono wagombea watakaouzika katika uchaguzi wa mwaka 2010.

Wanaopewa nafasi kubwa zaidi ya kuweza kusimamishwa kwa nafasi ya urais kwa upande wa upinzani ni pamoja na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbroad Slaa na Kiongozi wa Upinzani ndani ya Bunge, Hamad Rashid Mohamed, ambao wanaelezwa kuweza kukubaliana mmoja akawa Mgombea Mwenza.

Wanasiasa hao wa upinzani wanaelezwa kusukumwa zaidi na wabunge wenzao pamoja na watu wa kawaida wanaofuatilia mwenendo wa kisiasa nchini hasa kutokana na mchango wao ndani ya Bunge ambalo limebadili hali ya kisiasa nchini kwa kurudisha mwamko wa wabunge na wananchi.

Hamad Rashid amelithibitishia Raia Mwema jana kwamba ameshauriwa kujiandaa kuwania urais mwaka 2015 lakini baadhi wametaka aanze mwaka 2010, akiwataja baadhi ya wabunge waliomshauri, wakiwamo hata wa Chama cha Mapinduzi (CCM).

"Ni kweli nina nia ya kuwania urais lakini si wa Zanzibar na kwamba nilijiandaa kwa mwaka 2015, lakini wabunge wenzangu baadhi kutoka CCM wamenishauri nianze kujitokeza mwaka 2010," alisema Hamad, ambaye amewahi kuwa ndani ya Serikali ya Muungano katika wizara za Fedha na baadaye Mambo ya Ndani.

Akizungumzia suala hilo, Dk. Slaa alisema sasa ni mapema mno kuzungumzia mambo ya urais kutokana na nchi kuwa katika harakati za kupambana na ufisadi unaoihusisha hata Ikulu yenyewe.

Alisema Dk. Slaa: "Bado tuko mbali tukipambana na ufisadi. Nchi haitaki wanaokimbilia Ikulu. Inataka wenye ujasiri wa kusafisha Ikulu. Ukisema nawe unakimbilia Ikulu, unakuwa unataka ukafanye biashara au ukachote Ikulu. Wakati ukifika, hayo tutayajadili."

Kwingineko kumekuwa na minong'ono kuwa Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Chacha Wangwe pia ana nia ya kugombea kwa tiketi ya chama. Nia ya kuwania urais ya viongozi hao wawili huenda ikawagombanisha na mwenyekiti wao, Freeman Mbowe, aliyesimama mwaka 2005 na ambaye inaaminika angependa asimame tena mwaka 2010.

Alipoulizwa kuhusu habari hizo za yeye kutajwa kuwania urais, Chache Wangwe alisema, "Ni kweli, ikiwa chama changu kitanipendekeza, nitakua tayari kugombea."

Mkanganyiko mwingine wa Chadema unaweza kutokana na habari kwamba Naibu Katibu Mkuu, Zitto Kabwe, akizungumza na Watanzania walioko Houston, Marekani alikokuwa kwa ziara hivi karibuni, alisema atawaunga mkono Dk. Slaa na Hamad kama mazingira ya kisiasa yatawafikisha watu hao wawili katika kugombea mwaka 2010.

Siku za karibuni zimeshuhudia kutoaminiana miongoni mwa viongozi wa Chadema na hata kumhusisha Zitto na madai ya kuwa na urafiki wa karibu na Rais Kikwete, kiasi cha Kikwete kutaka kumteua kuwa waziri katika Serikali kabla ya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri ya Februari mwaka huu.

Zitto ameiambia Raia Mwema wiki katika mahojiano kuwa wakati hapingi kuwa ana ukaribu wa kiasi fulani wa siku nyingi na Rais Kikwete, hakuna wakati alipotaka kuingia katika serikali yake.

"Sijawahi kuombwa na Rais Kikwete kuingia katika serikali. Msimamo wangu siku zote umekuwa ni kutumikia taifa bila kujali itikadi. Hata Rais anajua hili, kwamba siwezi kuhama chama au kwenda kinyume na maamuzi ya chama changu. Kwamba Rais Kikwete ni rafiki yangu, si kweli. Ninafahamiana naye kitambo. Ninajua ananiheshimu sana. Lakini hakuwa chaguo langu la urais wakati wa mchakato wa chama chao na hata katika uchaguzi mkuu," alisema Zitto.

Lakini wafuatiliaji wa masuala ya kisiasa wanasema Zitto hajawahi kusikika akimshambulia Rais Kikwete katika hotuba zake na mara kadhaa amekuwa akimsifia katika maamuzi yake mbalimbali ambayo yamepingwa na wenzake. Hata kuingizwa kwake katika Kamati ya Madini ya Jaji Mark Bomani kulizua maswali mengi kutoka kwa wanasiasa wa CCM iliyombana alipoibua hoja ya mgodi wa dhahabu wa Buzwagi, na wa Upinzani.

Wengi hawaamini maelezo ya Zitto kwani anaonekana ni mtu mwenye kujiandaa kutokana na kuwa kwake na mahusiano ya karibu sana na wastaafu kama Jaji Joseph Warioba na Dk. Salim Ahmed Salim, watu ambao wana ushawishi mkubwa katika jamii.

Alipoulizwa kuhusu hili Zitto alisema kuwa yeye anawaheshimu sana viongozi wastaafu na hupenda kujifunza kutoka kwao na mahusiano yake nao hayana maana ya kutafuta kuungwa mkono.

"Nimekuwa na mahusiano na wazee hawa kama viongozi. Sio hawa tu. Ninazungumza na mzee Kaduma (Ibrahim), mzee Butiku (Joseph), mzee Kimiti (Paul) na mzee Jackson Makweta. Pia ninazungumza sana na Spika Samuel Sitta. Huwezi kusema hawa wote wananiandaa mimi kuwa Rais. Huo ni woga tu wa watu. Ni hulka yangu kuheshimu wakubwa na kujifunza ndiyo maana ukinikuta na Hamad Rashid hutaona mahusiano ya kiubunge. Utaona mahusiano ya mwalimu na mwanafunzi," anasema Zitto ambaye mwaka jana gazeti moja la kila wiki lilimshutumu kwa kujipendekeza kwa viongozi wakubwa.

Kwa upande wa CCM, habari zinaeleza kwamba tayari makundi yameanza kujipanga kwa uchaguzi mkuu wa Rais mwaka 2010 na wa 2015 kama Rais Jakaya Kikwete atafanikiwa kushinda patashika ya mwaka 2010 na kuendelea muhula wa pili ambao ni wa mwisho kwa mujibu wa katiba.

Makundi hayo yanajipanga mapema na kwa kuanzia imeelezwa kwamba wanasiasa na wafanyabiashara wanajiandaa kuweza kupata wajumbe wa kutosha katika Mkutano Mkuu wakati wa uchaguzi, wajumbe ambao ndio watakuwa waamuzi wakubwa wa mgombea kutoka chama hicho.

Licha ya kwamba kuna fununu za wagombea wengine kujitokeza kushindana na Rais Kikwete katika kinyanganyiro cha ndani ya CCM mwaka 2010, inaonekana uwezekano wa ushindi ni mdogo kutokana na utamaduni wa CCM kuendeleza muhula wa pili wa Rais aliyeko madarakani utaendelea. Hata hivyo, hali inaweza kubadilika kama Kikwete atakumbwa na dhoruba yoyote kubwa ya kisiasa kabla au kuelekea 2010.

Magazeti kadhaa, hivi karibuni, yalimtaja Profesa Mark Mwandosya kama mgombea anayetajwa kuweza kumkabili Rais Kikwete ikifika mwaka 2010. Mwandosya alikuwamo katika hatua za mwisho za mbio za urais mwaka 2005.

Wengine wanaotajwa kwa sasa kwa upande wa CCM kujiandaa ama kuandaliwa kumrithi Kikwete, iwe 2010 au 2015, ni pamoja na Waziri wa Mambo ya Ndani Lawrance Masha na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe.

Kumekuwapo pia na mijadala ya Watanzania, na hasa walioko nje, inayotaka Dk. Salim agombee ama kupitia CCM au kupitia muungano wa vyama vya upinzani. Yeye na Profesa Mwandosya walishindwa na Kikwete 2005, wote wakiwa wamefikia hatua ya mwisho kabisa.

Sources: Wajipanga kwa urais
 
Mbona naona ni kama outdated newz? tuwe makini na heading tunazotumia,"Breaking newz"
 
Mbona naona ni kama outdated newz? tuwe makini na heading tunazotumia,"Breaking newz"

Mkuu Jack, Breaking News ni Dk. Slaa kuwa mgombea urais si hiyo habari ya Raia Mwema ya Mei 21, 2008. Hiyo habari ni 'chombeza' ya hiyo Breaking News na zaidi eneo lililowekwa alama nyekundu. Ama kama hiyo ya Dk. SLaa kuwa mgombea Urais si Breaking News kwako, basi nadhani hiyo habari ya 2008 ndiyo ilikuwa habari kwako kwa hiyo si vibaya ukakumbushwa.
 
Kama ni kweli nimepata wa kumpa kura yangu ya Urais
 
CHADEMA hongera kwa hilo Dr. Slaa anachagulika na hata ukimwangalia mwenyewe ana uchungu sana na nchi hii.

ametushawishi kwenda kupiga kura. tunamtakia kila la kheri katika hilo
 
dah kwa mara ya kwanza hii habari imenifanya nionyeshe furaha yangu juu ya maaamuzi ya kishupavu na ya kutoangalia maslahi binafsi chadema hongera mmefanya maamuzi mazuri sana kumsimamisha dr Wilbroad Slaa.

Naamini JK sasa mAGOGONI HAPAKALIKI na tuina wasubilia wengi kuktoka ccm wakiisha angushwa huko kwenye kura za maoni hapo ndipo tutapo wagalagaza,kikubwa slaa ni mtu shupavu na mimi binafsi niko nyuma yako huu ni mwaka wa mapinduzi tumechoka na siasa za ki sultani, kuanzia Ridhwani Kikwete, January Makamba, na wengineo ambao nchi wameigeuza ni ya wazazi wao na kusahau hata ss mababu zetu pia wamejitolea maisha yao kwaajili ya tanganyika.

Kwaheri Kikwete ,slaa niko pamoja naww tunasubiri mgombea mwenza tupigilie msumari kabisa.
 
Hapo ngoma inogile. JK atapata shida sana kwa Slaa. Jamaa ana uwezo mkubwa sana wa kuchambua mambo. Akikampeni vizuri nina uhakika watanzania wengi watamuunga mkono. Ingekuwa vema wapinzani wote wakamsimisha Slaa kwani ndiye pekee anaweza kukubalika na inshallah tukaondokana na chama kandamizi cha CCM. Nitashiriki kwenye kampeni kikamilifu na kuhamasisha wananchi wapige kura ya kuiondoa CCM madarakani. SAA YA UKOMBOZI INAKARIBIA.
 
Amejiandaaje kukaa miaka mitano kijiweni, simshauri kwa kuwa atapunguza msisimko bungeni
Tatizo wananchi hawana mwamko wa kutosha juu ya nani anafaa kuiongoza Tanzania.

Lakini kama mimi na wewe tutaamua sasa kwamba kura yetu tunampa Dr Slaa, na tukasaidiana kuwapa elimu ndugu zetu huko nyumbani, kaka zetu, dada zetu na wapendwa wetu, wakampa kura Slaa, uhakika wa kuongoza nchi utakuwa ni mkubwa sana. Sipendi kuamini kwamba atatakiwa kukaa kijiweni. Watu washaichoka CCM na Kikwete wake, wanaoendelea kuvaa mashati ya kijani na kuishangilia ni wale wenye njaa kali na wanatafuta huruma ya bwana mkubwa.

Kama kweli Slaa amepitishwa kugombea nafasi hiyo, kwangu ni faraja kubwa, na ni imani yangu kwamba huyu ndiye Rais ajaye.

Tanzania bila CCM inawezekana tumpe kura Dr Slaa.
 
Mungu akinijalia Nitapiga kura kwa mara ya kwanza
 
Right candidate at right time. May god listen to our prayer we need a president like him.
 
Bora aendelee na ubunge tu.
Urais naamini atakosa ni mapema mno haraka ya nn ajipange kwanza.
 
Hii ya Dr Slaa kuwa mgombea Uraisi 2010 Imekaa Vyema.

Ameishasema mchangiaji mmoja hapo Juu. Kikubwa ni kutoa elimu kwa wapendwa wetu hasa wale wanaoishi Vijijini mwetu ili tuweze kumtosa mzee wa Kijani na Njano!

Hata hivyo, nahisi kuna kakosa kadooogo kakiufundi kamefanyika ambako naona kanaweza kutupunguzia idadi ya kura zetu hata kabla sisi-emu hawajafanya vitu vyao.
Chadema walipaswa kuonyesha nia ya kumuweka Dr Slaa kuwa mgombea Uraisi, hasa wakati ulee wa uandikishaji wapiga kura.

Nina hakika kuwa kuna watu weengi tu ambao waliacha kujiandikisha lakini ambao wangejua mapema kuwa Dr Slaa ndiye mgombea Uraisi wangejiandikisha. Tuanze kulifanyia kazi hili...
 
Mungu amesikiliza kilio cha waja wake. Kama aliweza kutupatia nchi iliyojaa asali na maziwa kwa nini asitupe kiongozi shupavu in the name of SLAA na kuwatokomeza majambazi wa CCM?! Go Slaa, go...
 
Bora aendelee na ubunge tu.
Urais naamini atakosa ni mapema mno haraka ya nn ajipange kwanza.
======

Ndugu yangu Fidel, usikate tamaa mapema.
Obama alianza hivi kwenye senate wakasema hawezi, sasa yuko wapi?
Watu wamechoka na hali ilivyo kama Wamarekani walivyokuwa wamechoka na Bushenomics.

Slaa nampa zote kwa sababu tatu kuu:
-Hapendi kuwa Rais, ameshawishiwa sana na bado hatuna uhakika kama atakubali kabisa.
-Ana uzalendo wa kweli, integrity yake haina doa.
-Ana uwezo na ujasiri wa kiuongozi.

Nitakwenda kupiga kura siku hiyo.
 
Eeeh bwana, Dr Wilbroad Slaa (CHADEMA)akiwa mgombea uraisi na Hamad Rashid Mohamed (CUF) akakubali kuwa mgombea mwenza huo utakuwa mtihani mkubwa sana kwa CCM ...... like we have never seen before!
 
Yawezekana bila ya shaka huu ukawa ni mwanzo mzuri wa kuelekea mabadiliko. Mtu kapatikana sasa ni ujumbe!
 


Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania (2010 - 2015)

Dr Wibroad Sla
a
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…