Mkuu Ndege ya Uchumi,
Naona Mungu kasikia kilio changu. Ni zaidi ya miaka miwili sasa nilikuwa nikimpigia KAMPENI ya waziwazi humu ndani ya JF huyu Dr. Slaa.
Siku wakimtangaza mshindi, bila ya kujali ataniandikia au lahh, ntakuwa mwenye FURAHA zaidi yake. Kuna sababu fulani fulani zinanifanya niwe hivyo. Wakati wa Mwinyi, kutokana na siasa yake ya RUKSA, nilipoteza ndugu wawili muhimu sana kwenye familia na kisa ni Muhimbili kutokuwa na mashine fulani ambayo sidhani hata ina bei kubwa.
Dr. Slaa, nitahakikisha NAKUSANYA NDUGU na JAMAA zangu zaidi ya 100 ili wakupigie kura. Nitawapa somo hadi kieleweke na nina imani hawatavunja ahadi tutakayowekeana kuwa WAKUPE WEWE KURA. Leo peke yake nimeshapata watano.
MODS: Tafadhali ifungulieni ile PETITION ya Dr. Slaa kugombea URAIS na mbadilishe tu kichwa cha habari kuwa WANAOMUUNGA MKONO DR. SLAA wajiandikishe hapo. Ikibidi basi ifungeni hiyo Kura ya Maoni ya Kikwete na muweke ya DR. SLAA.
Nilipoanzisha hii petition, kuna wengi waliona kama upuuzi. Ila ukweli ni kuwa Wasomi wa UDSM wamefanya kitu kama hichohicho na kwenda kumsinikiza Dr. Slaa agombee Urais. Nina uhakika kama tungelifika walau watu 500 humu ndani na kumuandikia barua, basi tungelizidi kuipandisha hadhi JF. Lakini bila ya kujali nini kimetokea, nina imani bado JF tuna kazi kubwa ya kufanya ili tubaki kwenye ramani ya Tanzania kuwa TULIHUSIKA NA MABADILIKO.
_____________________________________________________________________________________________
Wanachama wasomi wajiorodhesha kumtaka Dk. Wilbroad Slaa
Wakati Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kikiumiza kichwa juu ya mgombea wake wa urais, wasomi wanachama wa chama hicho kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, wamejiorodhesha kuwasilisha hoja yao kwenye chama hicho kutaka Katibu Mkuu wao, Dk. Wilbroad Slaa, awanie nafasi hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa za ndani ambazo Nipashe imezipata wasomi hao kwa muda wa wiki kadhaa sasa wapo katika harakati za kukusanya majina ya wanachama wao ili kuwasilisha hoja yao kwenye chama.
Tayari orodha yenye majina 412 imewasilishwa kwenye chama ikitaka Dk. Slaa akubali kubeba jukumu hili zito ili kupeperusha bendera ya Chadema kwenye uchaguzi mkuu wa Oktoba 31, mwaka huu.
Nipashe jana iliwasiliana na Dk. Slaa kumuuliza kama ana habari za harakati hizo na alisema hajui lolote.
"Kama kuna lolote tafadhali wasiliana na Mwenyekiti. Hayo ni mambo ya ndani ya chama," alisema Dk. Slaa ambaye hakuwa na muda mrefu zaidi wa kuingia kwenye mahojiano ya simu kwa sababu alikuwa akihudhuria vikao vya chama.
Dk. Slaa amekuwa mbunge wa Karatu tangu mwaka 1995 akiwa ni moja ya mihimili imara ya Chadema ndani na nje ya Bunge, lakini akiwa miongoni mwa wanasiasa walijizoelea heshima kutokana na msimamo wake wa kupambana na ufisadi na kutetea maslahi ya umma.
Kama Dk. Slaa atakubaliana na shinikizo la wanachama hao itakuwa ni mara ya pili kwa Chadema kumsimamisha mgombea urais tangu kufanyika kwa uchaguzi wa vyama vingi mwaka 1995.
CHANZO: NIPASHE
Sikonge Roho Kwatu He he he heeeeeeeee