Halafu Lipumba wampe PM au waziri wa fedha, waangalie wenzao wa kenya wanavyo unga unga mpaka upinzani umefanikiwa.Hatujachelewa. Lipumba aende Sikonge au jimbo lolote analoona atashinda ili tuunganishe nguvu!
Hata Michuzi kimyaaaa!!Mkubwa
Sio wewe peke yako. Hata mimi nilikuwa nategemea waseme kitu fulani. Sio TBC tu, hata ITV kimya. Wanaogopa reaction ya boss wao?
Wananchi ndio wenye nchi; na watashinda tu. Zilikuwepo dola za kirumi na zikaanguka; sembuse hii CCM ya waswahili wa pwani, ya mipasho?
Hata Michuzi kimyaaaa!!
Utawatambua kwa matendo yao...
Bado wako thunderstruck = uko sahihi kwa 110%!!Mkuu M-babe si hao peke yao - wengi bado wako thunderstruck, Malaria Sugu na Tumain nao wamo.
Pia mnatakiwa mjue kuna ubunge wa kuteuliwa, hivyo akiukosa wa karatu, bado anaweza ingia mjengoni. na lazima kwenye Uraisi tutie timu huko.
Amechemka sana. Kuliko wakati wowote. Au wamemfanyia uhuni wenzake. Basi hata Bunge limeisha utamu wake. I will mis him.
Yaelekea habari hii imekuchoma kumtima. Pole we!
Pia mnatakiwa mjue kuna ubunge wa kuteuliwa, hivyo akiukosa wa karatu, bado anaweza ingia mjengoni. na lazima kwenye Uraisi tutie timu huko.
Wanaume wanaweza kupata Ubunge wa kuteuliwa na Rais tu. JK akishinda uchaguzi hawezi kumteua Dr. Slaa kuingia mjengoni maana atakuwa anajipalia makaa ya moto. Viti vya kuteuliwa kwa upande wa Upinzani ni vya Wanawake tu, labda kama ikitokea yale makubaliano ya CUF na CCM kama jinsi Juma Duni Haji alivyoukwaa.
Pamoja na hayo, CHADEMA wanapokuwa na mgombea strong kama Dr. Slaa inawapa pia opportunity ya kupata support kubwa kwenye ngazi za Ubunge.
CCM hawakutarajia kama Dr. Slaa angekubali kugombea maana siku zote amekuwa akikanusha kwamba hana nia ya kugombea. Lakini nadhani pressure ya watu kumuomba agombee imemzidi na hivyo kuona haja ya kutaka kuwatumikia wananchi. Let us wait CCM's next move maana najua kwa sasa matumbo yanawachemka.
Kabla hatujasema mengi humu, labda tungefanya tathmini kutoka vijijini namna gani watu wamepokea habari hii, maana huko ndiko mtaji wa CCM uliko, sina tatizo na mjini. baada ya hapo angalau tunaweza kupata picha ya nini kitatokea.
Baada ya hii habari nilimpigia mmoja wa wana CCM, yeye anasema Slaa sio tishio kwa sababu Chadema haina network vijijini, tujadili hili pia
Yaelekea habari hii imekuchoma kumtima. Pole we!