Mwanajamii
JF-Expert Member
- Mar 5, 2008
- 7,063
- 70
Hakimu aagiza Slaa, mchumba wake wafike mahakamani
Imeandikwa na Veronica Mheta, Arusha; Tarehe: 21st February 2012
[TABLE="align: right"]
[TR]
[TD]
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD][TABLE="align: right"]
[TR]
[TD="class: kaziBody"]Habari Zaidi:[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: Marquee"][/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]
[TABLE="align: right"]
[TR]
[TD="class: kaziBody"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: Marquee"][/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
HAKIMU wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, Charles Magesa ameagiza Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa na mchumba wake Josephine, kufika mahakamani hapo leo asubuhi kabla ya kuanza kwa kesi dhidi yao na kinyume na hapo atatoa hati ya kuwakamata.
Magesa alitoa amri hiyo jana baada ya washitakiwa hao na mwenzao, Aquiline Chuwa kutofika mahakamani hapo na wakili wao, Albert Msando alipoulizwa akawatetea kuwa wamechanganya siku ya usikilizwaji wa kesi ya kufanya maandamano yasiyo halali na kesi ya kutoa matamshi ya uchochezi.
Jana katika kesi hiyo, usikilizwaji wa awali ulikuwa uanze kwa washitakiwa 19 akiwemo Dk. Slaa kusomewa mashitaka mapya 13 yanayowakabili.
Awali wakili wa Serikali, Edwin Kakolaki aliiomba Mahakama kutoa hati ya kuwakamata washitakiwa hao na kuwaleta mahakamani kwa nguvu kutokana na kudharau Mahakama.
Si kweli kuwa wamechanganya tarehe ya kesi kutokana na wingi wa kesi walizonazo kwa kuwa wanaowadhamini wangepaswa kufanya nao mawasiliano pamoja na wakili wao.
Naomba mahakama itoe hati ya kuwakamata na kuwaleta hapa kwa nguvu ili wasipate mkanganyiko wa kuchanganya tarehe, aliomba Wakili Kakolaki.
Kakolaki pia aliiambia Mahakama kuwa washitakiwa hao wanadharau mahakama hiyo kwa sababu Januari 17 mwaka huu waliambiwa wakumbushane ili wasikose mahakamani siku hiyo kwa sababu ndiyo usikilizwaji wa awali wa kesi hiyo utafanyika, lakini hawakufanya hivyo.
Mimi nasema hawajasahau wamefanya makusudi, kwa sababu wangeweza kutumia njia ya kuandika katika kumbukumbu zao ili wasisahau tarehe za kesi zao, pamoja na kudai wana kesi nyingi zinazowachanganya lakini hiyo siyo sababu ya msingi, alisema Kakolaki.
Baada ya wakili Kakolaki kutoa ombi hilo, aliomba Mahakama iendelee na usikilizwaji wa kesi hiyo kama walivyokubaliana na washitakiwa ambao hawakuwepo, wasomewe mashitaka yao siku watakapofika leo.
Kakolaki baada ya kutoa ombi hilo, Hakimu Magesa alimwamuru aendelee na usomaji wa mashitaka ya awali.
Wakili Kakolaki alidai washitakiwa wote 19 wanashtakiwa katika kosa la kwanza, kula njama Januari 3 na 5 mwaka jana katika Manispaa ya Arusha ya kutenda kosa la kufanya fujo.
Katika kosa la pili linalowahusu washitakiwa 18, wameshitakiwa kula njama kufanya mkusanyiko usio halali na kufanya vurugu baada ya katazo halali.
Katika shitaka linawahusu Dk. Slaa na Mbunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo, wanashitakiwa kwa kutoa matamshi yenye lengo la kuleta uchochezi.
Pamoja na mashitaka mengine, pia walishitakiwa kwa kufanya mkusanyiko usio halali kwa ajili ya lengo moja la kukataa kutii amri ya OCD iliyowataka watawanyike.