Elections 2010 Dr. Slaa ndani ya Babati katika picha

n00b

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2008
Posts
1,015
Reaction score
2,680

Mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willbrod Slaa, akihutubia mkutano wa hadhara wa kampeni, kweny Uwanja wa Kwarah mjini Babati mkoani Manyara jana. (Picha na Joseph Senga)

Sehemu ya umati wa wakazi wa mji wa Babati na vitongoji vyake, wakiinua mikono juu kuashiria kukubaliana na hotuba ya mgombea wa urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa (hayupo pichani), wakati wa mkutano wake wa kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Kwarah mjini humo jana. (Picha na Joseph Senga)

Leo atakuwa Hanang na Mbulu, nikizipata picha nitaziambatanisha
 
Naomba Mungu na siku ya Uchaguzi watu wawe wengi hivi ili TUWAANGUSHE CCM KWA KISHINDO na kuwazui kuiba kura kama walivyo zoea
 
Mhhhh! Kuna mambo yanatisha.
Hebu angalia mgombea urais (rais mtarajiwa) anavyolindwa. Katika picha zote nne utaona kuna Polisi wa kawaida 1, Usalama barabarani 3 na wakampuni binafsi(kama si mgambo wa Halmashauri) 2.

Hivi kwa umati huu likitokea la kutokea watafanya nini hawa? hawafu hawajakaa kama walinzi bali kama wasikilizaji.

Kaaazi kweli kweli.
 
Kama nimeona vibaya, mbona wanaonekane wengi wana umri chini ya miaka 18 hasa safu ya mbele? Watasaidia ushindi kweli au watawashawishi wazazi wao?
 
Naona watoto wengi hpo mbele ambao kwa mtazamo wangu hawajitimiza hata umri wa kupiga kura!!
 
Mnadhani hao hawatafikisha miaka kumi na nane? Na hakuna kulala mpaka kieleweke nyinyi mnadhani ina maana gani?
 
Naona watoto wengi hpo mbele ambao kwa mtazamo wangu hawajitimiza hata umri wa kupiga kura!!
Watoto wapo safu ya mbele, wamekuja kusikiliza jinsi haki zao na nchi yao inavyoumizwa na mafisadi na hivyo watakua wakijua hilo na watakuwa wapiganaji tangu sasa hadi watakapoanza kupiga kura.

Mikutano yote including ya CCM watoto wanahudhuria kama kazi. Hata hivyo watoto waliopo kwenye mkutano wa Dr Slaa ni percentage ndogo sana ya umati wote uliohudhuria. Hivyo hapana shaka kuna wapiga kura wakutosha kumwangusha Goliath
 
Kama nimeona vibaya, mbona wanaonekane wengi wana umri chini ya miaka 18 hasa safu ya mbele? Watasaidia ushindi kweli au watawashawishi wazazi wao?

naogopa kusema unajipotosha. Umekataa kuiruhusu akili yako ikitafsiri vizuri kile unachoona. Watoto katika mikusanyiko kama hii lazima watakuwepo.
Kinachonekana kwenye picha ni kuwa watoto wako mbele mistari michache kwasababu wanataka waone (kwani wao ni wafupi). Hebu angalia mistari ya nyuma ambayo ni mingi zaidi unaona nini.

Kama huoni kitu nenda JF-Doctor kwa ushauri zaidi.
 
Watu bwana umeona watoto tuu,infact decision making nyingi katika familia they are based on the influence of watoto.
Imagine mtu anashindwa achana na mumewe kisa watoto nani atawalea.
So uwingi wao apo pia ni dalili tosha ya msukumo toka kwa wazazi wao na ata wakikuwa tayari watakuwa wanajua nini kinachijiri ktk siasa za Tz
 
Siko kinyume sana na walio wengi humu ndani, naandaa CV yangu mambo yakiwa mazuri mnipe hata ukurugenzi wa shirika moja la umma nami nionje angalau kwa miaka mitatu matunda ya uhuru
 
Naona watoto wengi hpo mbele ambao kwa mtazamo wangu hawajitimiza hata umri wa kupiga kura!!

du hao watoto hasa washule za msingi sijui kama wanaelewa chochote. maana akija mgombea mwingine wanajaa hivyo hivyo
 
du hao watoto hasa washule za msingi sijui kama wanaelewa chochote. maana akija mgombea mwingine wanajaa hivyo hivyo
Mara nyingi ni ngumu kwa wanadamu kuukubali ukweli ila uhalisia ndo huo..yaani pale watakuwa wamekuja kutokana na ile helikopta nadhani ilipiga misele kwenye viunga vya babati na watoto kwa kupenda ushabiki maandazi wakajazana kwenye tukio ..,pale walikuwa wapo wapo tu wanasubiria labda thoda au maji!!
Kampeni ngumu kweli jana niliona mgombea waCUF alifika eneo la tukio hakukuwa na mtu ikabidi zifanyike juhudi binafsi za kuokoteza watu waje kwa mkutano!
 
Naomba Mungu na siku ya Uchaguzi watu wawe wengi hivi ili TUWAANGUSHE CCM KWA KISHINDO na kuwazui kuiba kura kama walivyo zoea

Mkuu, ebu angalia hizo picha vizuri! wapiga kura hapo ni 20% tu, hao wengine hawana sifa za kupiga kura.
 
Mkuu, ebu angalia hizo picha vizuri! wapiga kura hapo ni 20% tu, hao wengine hawana sifa za kupiga kura.

20%?, you are joking, hawana sifa kwamba hawakujiandikisha, how do you know that?
 
kwa sababu hana kambi ya mafisadi
 
Naona watoto wengi hpo mbele ambao kwa mtazamo wangu hawajitimiza hata umri wa kupiga kura!!

Mkuu acha hizo, yaani umeshawasahau wale watoto waliokuwa wanapewa peremende na muungwana!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…