Kwa habari hiyo hiyo Mlimani TV walionyesha umati mkubwa zaidi kuliko TBC, nadhani TBC walitafuta upande ulio wazi kidogo ndio wakauonyesha lakini bahati mbaya kote kulijaa hivyo wakawa hawana namna japo muda mwingi walimwonyesha Slaa na sio umati uliohudhuria, kinyume na mikutano ya CCM, muda wote camera kwa waliohudhuriaLakini kwa mkutano wa Slaa jana kule Biharamulo, TBC walionyesha ule umati uliohudhuria.
Rais wetu mtarajiwa Dr Wilbrod Peter Slaa yupo leo Bukoba. Amekuwa na mkutano maeneo ya Kibengwe Bukoba vijijini na anategemea kuwa Kanyigo baadaye.
Sasa hivi anategemewa muda mfupi ujao atakuwa katika kata ya Ijuganyundo katika Manispaa ya Bukoba. Kisha atahutubia katika viwanja maarufu hapa mjini kama Uhuru Platform. Watu ni wengi sana walio katika maandalizi ya kumpokea na kumsikiliza. Naona bendera kila mahali.
Nimepata habari kwamba kule Karagwe jana Dr alipokelewa na umati ambao haujapata kuonekana na kwa wale wakazi wa Karagwe inasemekana watu walijipanga njiani toka Kayanga hadi Nyaishozi ili kumlaki mwaka huu namshauri Kikwete aondoke kwa amani ikulu.
Habari zaidi na picha baadae wakuu wangu. Ngoja niwahi mkutano!
Pepleooooooooooooooos Poweeeeeeeeeeer!
[/QUOT
Excellent

we acha tu huyu bwana amemuweka kwenye ICU yule naibu waziri wa mambo ya ndani Hamis Kagasheki. Hana uhakika wa kurudi bungeni kama Jakaya asivyo na hakika ya kurudi Ikulu.Si hapo BK Mjini yupo Mbunge Lwakatare kwa tiketi ya Chadema bt nashangaa makeke yake hayasikiki kabisa
View attachment 15306
helicopter ilimbeba mheshimiwa dr ikiwa katika anga la ijuganyundo wakati ikitokea kaisho karagwe ikivinjali angani
View attachment 15307
usafiri uliombeba mh rais mteule ajaye ikijitayarisha kutua katika eneo la ijuganyundo manispaa ya bukoba
View attachment 15308
watu waliofika kumpokea dr slaa wakati aliposhuka kutoka katika helicopter yake eneo la ijuganyundo
View attachment 15309
dr slaa akimnadi mgombea udiwani wa chadema kata ya ijuganyundo bw.gerasius muhimba.
picha wap? mbona hizi zinazoonyeshwa hazina umati unaosema mkuu?Wakuu samahani sana maana ilibidi niende kutafuta juice kidogo maana tangu asubuhi nilikuwa kwenye pilika pilika za kampeni maana ilikuwa pata shika hapa Bukoba.
Baada ya mikutano yake katika maeneo ya Kibengwe Bukoba vijijini na Rubale Dr Slaa alielekea Kaisho karagwe kwa mikutano zaidi maana jana hakupata nafasi ya kufika eneo hilo. Huko ni mbali kidogo.
Amefika Katika eneo la Ijuganyundo, kata ambayo iko pembeni kama kilometa 10 hivi kutoka kati kati ya mji wa Bukoba mnamo kama saa 9.30 mchana.
Hakuhutubia mambo mengi sana mbali na kuinadi kidogo Chadema na kumuombea kura mgombea udiwani wa kata hiyo ndugu Gerasius Muhimba ambaye anachuana vikali na mgombea wa sisi m ajulikanaye kama Kalumuna ambaye kwa kipindi kilichopita amekuwa ni naibu meya.
Ukweli ni kwamba Kalumuna anapumulia katika mashini ICU kwa jinsi alivyoshikwa pabaya na mgombea huyu wa Chadema. Dr alichofanya ni kuwabembeleza wana Ijuganyundo kutompa kura Kalumuna kwa kuwa hakuwatimizia kiu yao na badala yake waichague Chadema kwa kumpa kura yeye kwa urais, Lwakatare kwa ubunge na Gerasius kwa udiwani.
Kisha alimpa nafasi diwani mtarajiwa kusema neno kwa wananchi kisha aliahirisha mkutano na safari ya kwenda mjini Bukoba ilianza kwa magari kama 50 na pikipki na baiskeli. Msafara ulikuwa mrefu sana huku Dr Slaa akiwa katika gari la wazi kwa safari iliyopitia maeneo ya Ibura, magoti, kibeta, Rwamishenye, hamugembe hatimaye uhuru platform ambako kulikuwa na umati mkubwa wa watu uliokuwa ukisubiri.
Tukio la kipekee ni pale helicopter ilipokuwa ikisindikiza msafara angani hadi kwenye uwanja wa mkutano. Pia watu walishangaa kuona Dr wa ukweli akifika kwa gari maana walidhani angefika pale kwa helicopter.
Ukweli umati uliofika pale uwanjani umevunja rekodi kwa wingi kiasi kwamba kuna watu waliokuwa wakisikia sauti tu bila kumuona Dr Slaa aliposimama kuhutubia.
picha wap? mbona hizi zinazoonyeshwa hazina umati unaosema mkuu?