Wakuu samahani sana maana ilibidi niende kutafuta juice kidogo maana tangu asubuhi nilikuwa kwenye pilika pilika za kampeni maana ilikuwa pata shika hapa Bukoba.
Baada ya mikutano yake katika maeneo ya Kibengwe Bukoba vijijini na Rubale Dr Slaa alielekea Kaisho karagwe kwa mikutano zaidi maana jana hakupata nafasi ya kufika eneo hilo. Huko ni mbali kidogo.
Amefika Katika eneo la Ijuganyundo, kata ambayo iko pembeni kama kilometa 10 hivi kutoka kati kati ya mji wa Bukoba mnamo kama saa 9.30 mchana.
Hakuhutubia mambo mengi sana mbali na kuinadi kidogo Chadema na kumuombea kura mgombea udiwani wa kata hiyo ndugu Gerasius Muhimba ambaye anachuana vikali na mgombea wa sisi m ajulikanaye kama Kalumuna ambaye kwa kipindi kilichopita amekuwa ni naibu meya.
Ukweli ni kwamba Kalumuna anapumulia katika mashini ICU kwa jinsi alivyoshikwa pabaya na mgombea huyu wa Chadema. Dr alichofanya ni kuwabembeleza wana Ijuganyundo kutompa kura Kalumuna kwa kuwa hakuwatimizia kiu yao na badala yake waichague Chadema kwa kumpa kura yeye kwa urais, Lwakatare kwa ubunge na Gerasius kwa udiwani.
Kisha alimpa nafasi diwani mtarajiwa kusema neno kwa wananchi kisha aliahirisha mkutano na safari ya kwenda mjini Bukoba ilianza kwa magari kama 50 na pikipki na baiskeli. Msafara ulikuwa mrefu sana huku Dr Slaa akiwa katika gari la wazi kwa safari iliyopitia maeneo ya Ibura, magoti, kibeta, Rwamishenye, hamugembe hatimaye uhuru platform ambako kulikuwa na umati mkubwa wa watu uliokuwa ukisubiri.
Tukio la kipekee ni pale helicopter ilipokuwa ikisindikiza msafara angani hadi kwenye uwanja wa mkutano. Pia watu walishangaa kuona Dr wa ukweli akifika kwa gari maana walidhani angefika pale kwa helicopter.
Ukweli umati uliofika pale uwanjani umevunja rekodi kwa wingi kiasi kwamba kuna watu waliokuwa wakisikia sauti tu bila kumuona Dr Slaa aliposimama kuhutubia.