Elections 2010 Dr Slaa ndani ya Ifakara leo

Zak Malang

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2008
Posts
5,404
Reaction score
239
Leo Dr Slaa ametinga ndani ya mji wa Ifakara na kufanya mkutano mkubwa ambao haujawahi kutokea hapo, kufuatana na habari nilizopata kutoka kwa swahiba wangu kule.

Anasema ingawa mkutano ulifanyika saa 5 mchana, lakini ulikusanya watu wengi mno ambao walifika bila kupatiwa usafiri wowote au bila ushawishi wowote.

Anasema kuanzia jana, viongozi wa CCM wa wilaya wamekuwa katika vikao visivyokwisha kujadili ujio wa Dr Slaa, mgombea ambaye amebadilisha sana upepo wa kisiasa sehemu hiyo.

Nimemwambia anitumie picha akiweza kuzipata.
 

Safari kuelekea Iringa imeiva. Wanyalu kaeni mkao wa kula.
 
Picha ziko hapa hapa jamvini tayari
 
iwe mwaka huu au 2115 au 2020 CCM ina mwisho.kama vile BABELI CCM ina mwisho ALELUYA:llama:
 
Kila dalili inaonyesha kuwa CCM itaanguka mwaka huu. Wengi wanasema kuwa Makamba ni Chaguo la Mungu kwa ajili ya kuingusha CCM.
Kikwete aombwe kukubhali matokeo isiwe kama ile ya Mrema iliyoibiwa. Alishinda kura zikaibiwa kulingana na taarifa zinazotolewa.
 
Kikwete anapita kila mahali kwa kuwaaga wananchi na sio kuomba kura. Kura alishakataaa.
 
Kuna habari ambazo zimeenea Kyela kuwa Dr Slaa anakuja tarehe 4-10-2010, na atahutubia mpaka vijijini. Japo baadhi ya viongozi wa chadema wanathibitisha hilo lakini ratiba yake haioneshi kitu kama hicho. Kama kutakuwa na habari zaidi tunaomba kujulishwa undani wa hili jambo ili tuweze kupangilia mambo yetu vizuri na kuhamasisha watu. Asantateni
 
Kwa nini Dr Slaa husahau mara nyingine kuambatana na Jose? Ni kivutio kikubwa!
 
naona watu wa viwanja 60,lipangalala,kibaoni,michenga watabadililka na kuiangusha ccm
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…