Zak Malang
JF-Expert Member
- Dec 30, 2008
- 5,404
- 239
Leo Dr Slaa ametinga ndani ya mji wa Ifakara na kufanya mkutano mkubwa ambao haujawahi kutokea hapo, kufuatana na habari nilizopata kutoka kwa swahiba wangu kule.
Anasema ingawa mkutano ulifanyika saa 5 mchana, lakini ulikusanya watu wengi mno ambao walifika bila kupatiwa usafiri wowote au bila ushawishi wowote.
Anasema kuanzia jana, viongozi wa CCM wa wilaya wamekuwa katika vikao visivyokwisha kujadili ujio wa Dr Slaa, mgombea ambaye amebadilisha sana upepo wa kisiasa sehemu hiyo.
Nimemwambia anitumie picha akiweza kuzipata.