Nimewahi kuhudhuria mkutano mmoja wa kampeni wa Dr. Slaa na nikalinganisha na mikutano ya kampeni ya JK. kupitia Tv nikagundua tofauti kubwa sana.
1. Dr. Slaa anazungumzia masuala yake kwa kutaja vitu vya msingi na vichache sana bila kusoma mahali popote. JK. ninaona anazungumza vitu vitu ambavyo huwezi kujua kipi ni cha msingi. Mf. Dr. Slaa anaweza kuzungumzia juu ya uboreshaji wa huduma ya afya na Elimu na akaeleza kwa kifupi sababu ya serikali kufanya hivyo, namna ya kutekeleza hilo na muda wa kutekeleza. lakini ndugu Jk. akifika mahali akikuta Hospitali ambayo ina hadhi ya Hospitali Wilaya anaahidi kuwa hiyo itakuwa Hospitali ya Mkoa au ya rufaa.
Ukweli ulio wazi ni kuwa ama Jk anawaona Watanzania ni mbumbumbu au yeye ni mbumbumbu. Haiingii akilini kwa mfano kutuambia Hospitali fulani itakuwa Hospitali teule, wakati Dispensari imeshindwa kutoa huduma kama dispensari. Jk kama kiongozi wa serikali iliyopo madarakani anajua wazi kuwa haina maana kuipa Hospitali hadhi ya kuwa Hospitali kama hujaandaa madaktari wa kutoa huduma hiyo.
2. Uwezo wa Dr. Slaa ni mkubwa sana kuelewa kwamba wananchi wanahitaji nini na yeye kama mgombea anawaambia hilo tena kwa ufasaha na kwa hoja inayokubalika. Jk. haelewi kabisa watu wanatarajia nini kutoka kwake. Mfano: watu hawahitaji mgombea kuzungumzia ujenzi wa barabara inayojengwa wakati watu wanaiona kwa macho. Vile vile watu hawataki mgombea kuzungumzia vitu vinavyofanyika ambavyo vimetengewa bajeti ya serikali. Bajeti ya serikali inapitishwa mwaka hadi mwaka na wabunge wanahusika navo hvyo haina maana ya mgomea kuweka kwenye ahadi yake.
3. Dr. Slaa huwa anaweza kusema vitu anavyotaka kuwaambia wapiga kura bila kuhangaika kurejea kumbukumbu (data) zilizoandikwa. Jk. wakati mwingine husoma hutuba zake utafikiri anawasilisha hoja bungeni. Mgombea urais tena anayemalizia kipindi anashindwa hata kutambua kuwa wananchi hawahitaji uwingi wa ahadi na tarakimu nyingi bila sababu za msingi.
Natoa pole kwa Jk kwa kushindwa kujibu maswali ya msingi yaliyo katika vichwa vya wapiga kura na badla yake kuhangaika kuahidi vitu vingi kama ununuzi wa meli, viwanja vya ndege nk. vitu hivyo si hoja za kutosha kwamba wanachi wakuchague. Kitu cha ajabu ni kuwa itakuwaje endapo wagombea wengine nao wataahidi vitu kama hivyo? je, tumchague yule atakaye ahidi vitu vingi? JK akumbuke hata kama anaahidi mf. kujenga uwanja wa ndege ni wananchi ndiyo wanaojenga kwa kodi zao siyo yeye. Kutoka kwake watu wanataka dira na upeo alionao katika kuwaongoza wananchi.