Hilo wala si uongo.
Slaa alikuwa anatuaminisha kuwa Lowassa ni fisadi.
Lakini leo nnaona Slaa kazimwa na Mwenyekiti Mbowe, hasikiki wala haonekani.
Nnauhakika kazimwa kwa ajili ya ufisadi wake na alikuwa anadanganya kuwahadaa Watanzania kuwa Lowassa ni fisadi.
Mimi nnaamini Lowassa ni mtu safi kabisa, hana ufisadi hata chembe, kama anavyoamini Mbowe na wana UKAWA wote na ndiyo maana leo hii Mbowe alivyoingia tu chadema, siku hiyo hiyo kakaribishwa kwa kupewa kadi ya uanachama na siku hiyo hiyo kapewa nafasi ya kugombania Urais wa Tanzania.
Hakuna sababu nyingine yeyote zaidi ya kuwa Lowassa ni msafi, na ana uwezo kuliko mwana chadema yoyote katika uongozi ndiyo maana akapishwa haraka haraka kuchukuwa nafasi ya kugombea urais Tanzania.
Kwa upande mwingine, nnaamini kabisa kabisa kuwa Daktari wa Kanoni Slaa siyo mwadilifu na ni zaidi ya fisadi na ndiyo maana kapigwa chini na chadema na UKAWA kwa ufisdi wake hafai kugombea urais wala hafai kuwa Katibu Mkuu wa Chadema
Hali kadhalika kwa muasisi na aliyetowa wazo la UKAWA na aliyeongoza watu kutoka BMK, Professor Harun Lipumba. na yeye ni fisadi na kahongwa ndiyo maana kaachia Uenyekiti wa CUF.
Kumbe mafisadi tulikuwa nao tena mmoja ni Katibu Mkuu na mmoja ni Mwenyekiti wa vyama vyetu mahiri vya upinzani CUF na CHADEMA, hatukuwastukia mpaka hizi dakika za mwisho.
Ahsante Lowassa kwa kutujulisha kuwa hao ndiyo waliokuwa mafataani waliokuwa wanatukosesha ushindi miaka yote.
Tujadili.
Kuna wafia chama wengi wa CCM kama huyu mwanamke ambao wanaona impact ya alichokisema Dr slaa kwa wananchi haijawa kubwa,imekuwa kama pakiti moja ya chumvi kwenye bahari!Wamepagawa sasa they are trying every angle kuwachanganya wapenda mabadiliko!
Miaka yote huyu bibi amekuwa anamtukana Dr slaa kuwa ni Padre na Malaya,kuwa ameiba mwanamke wa watu!Yote hii ni kutokana na chuki za imani yake kwa Dr!Mara zote wanaCDM wamekuwa wakimtetea Dr kwa maamuzi yake ya maisha binafsi dhidi ya chuki za mleta mada!
Ili kufurahisha nafsi yake sasa anajifanya mwana CDM na ili kuwafanya wale waliomtetea slaa wamtukane ndio nafsi yake iridhike!Kinachomuuma zaidi ni slaa kumtaja JK(muislam) mwenzake kwenye list of shame,hilo linamuuma mpaka leo!
Dr Slaa ni kweli ametuvunja moyo wanaCDM hasa aliotukuta tukiwa wafuasi na tukampokea na akapata fursa ya kugombea ubunge na baadaye urais!Hatukumbagua kwakuwa alikatwa Ccm lakini tuliamini atasaidia kukijenga chama na kuleta ukombozi,kama ambavyo tunaamini lowassa anaweza leta ukombozi kwa kuliondoa kubwa la maadui,joka,shetani na kikwazo cha maendeleo "ccm"!Dr aliongea kwa namna ya kuwataka watz wasusie mabadikiko na wajitenge na ukawa!Suala moja ambalo mimi ni shahidi ni kuwa sikweli limenifanya nione dhamira yake si nzuri bali uchu wa madaraka!Ni pale aliposema cdm kimebeba watu na malori jangwani,hili limenifanya nione yote aliyosema ni uongo na ni kwa lengo alilokusudia!Kama alipewa chochote hilo sijui lakini siku ccm ikiondoshwa madarakani hatakumbukwa kama mtu aliyetoa mchango wa mabadiliko bali mtu aliyeasi mabadiliko ambayo tuliyapigania kwa kipindi kirefu bila mafanikio!
Siwezi kumtukana dr na kumuita hayo majina anayosema mleta mada kumfurahisha yeye,na wengi msiingie kwenye mtego huu!Huyu mwanamke ni mfia chama wa ccm na amekuwa akiendesha siasa humu jamvini za kibaguzi kidini,kikabila na kikanda!Watu kama hawa ni wajinga na wapumbav wasiojua thamani ya nchi yao na taifa linalwenda wapi,wanachojua wao ni kupika majungu,kunya na kulala!Wanajali maisha yao tu na si kizazi kijacho,kwa mwendo huu wajukuu na vitukuu miaka 50 ijayo watatuona malofa na wajinga!Nchi haina dira watu wamekalia ushabiki na maneno ya kanga!Watu wanaoliibia taifa ndio wanaolindwa na serikali!
Change will never come if we wait for someone or some other time,we are the ones we have been waiting for,we are the change we seek!
Tusikubali kuvurugwa katika kipindi hiki,ndivyo walivyozoea!Wameshindwa kumfanya mtanzania awapende kwa kumletea maendeleo sasa wanachofanya wanalazimisha kushika dola kwa kuzima harakati za upinzani kwa hila!Rejea vyama mbali mbali miaka ya nyuma vilivyowahi kushika kasi na kutishia uhai wa ccm!Vilihujumiwa na kuzushiwa mambo ambayo watanzania waliamini,this time tusikubali propaganda mfilisi za aina yoyote toka ccm!
The time is now,tukutane Oct 25!