Dr. Zakir Naik awasili Zanzibar, afafanua kuhusu mhadhara atakaofanya, asema hakuna utata kwa wale wanayoyajua maandiko

Dr. Zakir Naik awasili Zanzibar, afafanua kuhusu mhadhara atakaofanya, asema hakuna utata kwa wale wanayoyajua maandiko

TANGAZO

AZAM MEDIA LTD PAMOJA NA THE ISLAMIC FOUNDATION …

UJIO WA DR ZAKIR NAIK TANZANIA - RATIBA YAKE YOTE

View: https://m.youtube.com/watch?v=PLO0zcQm7ok

KWA MARA YA KWANZA TANZANIA WANAKULETEA MHADHIRI MASHUHURI WA KIMATAIFA , DKT ZAKIR NAIK AKIAMBATANA NA MWANAE SHEIKH FARIQ NAIK KATIKA MDAHALO WA MASWALI NA MAJIBU :

TAREHE 31/12/2024 MSIKITI ZINJIBAR, UNGUJA ZANZIBAR KUANZIA SAA 2 ASUBUHI HADI SAA 7 MCHANA

TAREHE 2/01/2025 DIAMOND JUBILEE DAM KUANZIA SAA 1 USIKU HADI SAA 6 USIKU

TAREHE 5/01/2025 BENJAMIN MKAPA STADIUM UWANJA WA TAIFA KUANZIA SAA 2 ASUBUHI HADI SAA 7 MCHANA

MATANGAZO HAYA YATAKUJIA LIVE - MUBASHARA KUPITIA CHANEL YA ZBC2 WEMA UNAOENDELEA

SOURCE : DUA TV

Anaoenda kuongea nao wanajua kiinglish Sasa!??
 
Amekosea kutua zanzibar kwenye waislam wengi, atajua ndio Tanzania yote iko hivyo, kwamba ni waislam watupu. Angetua bara tena kilimanjaro, au mbeya
 
Mjadala na Atheists huwa inamtoa kamasi muache akomae na waumini wenzake huko kidogo kuna nafuu.
Mimi mtu akija na mistari ya Bible au Quran, lazima asalimu amri..
Ila huwa namaliza kwa kumumbia faida za kuamini kwenye dini na kumsisitiza abaki na imani yake na siingilie imani za watu wengine.
 
Biblia gani imuongelee tapeli na nabii wa uongo Muhammad?

Biblia imewaongelea wayahudi maana wokovu umetoka huko,

Biblia labda imezungumzia Muhammad kama nabii wa uongo na tapeli katika siku za mwisho
 
Anaoenda kuongea nao wanajua kiinglish Sasa!??

Kweli itakuwa mtihani mkubwa kwa Taifa, hotuba zake katika lugha ya kigeni.

Kuanzia December 2024 nchini Kenya, Uganda kulikuwa hakuna changamoto ya lugha na pia miaka iliyopita kule Gambia, Ghana, Nigeria midahalo na mihadhara ilifanyika kwa mhubiri kuwasiliana moja kwa moja na hadhira (audience).

Mambo ya tafsiri au kupitia mkalimani wa lugha imefanya mwanzo wa ziara yake Tanzania kupooza kutokana na mhadhiri kupoteza kufahamu hadhira kama imemuelewa au la hapa Zanzibar.
 
Hapa Tanzania hamna Mklokole wakiujitokeza kabisa wengi wana fuata hiyo dini bila ushahidi wama andishi ni mbumbumbu.
Mzee, huwa unakaa chini kutafakari matendo yako au ndio wewe na dini, dini na wewe?
 
Karibu sana mtaalam. Naimani wakristo wengi watabadili dini na kufata dini ya haki baada ya mhadhara huu.
 
31 December 2024
Zanzibar, Tanzania

MUBASHARA kutoka Masjid Zinjibar

Muhibiri wa kimataifa akitoa muhadhara muda huu, ikiwa ni hatua yake ya kwanza tangu akanyage ardhi ya Tanzania

LIVE🔴 KONGAMANO LA AMANI MASJID ZINJIBAR- DR ZAKIR NAIK 31 December 2024

View: https://m.youtube.com/watch?v=ipig0nJIhIc
Source : Dua TV Tanzania (TZ)

Thatmini hatua ya mwanzo ya Ziara imekosa mguso uliotarajiwa Zanzibar na Tanganyika. Waliofaidi ni watu nje ya Tanzania wanaoongea lugha za kigeni Kiarabu na Kiingereza

Sababu mojawapo mdau anaisema ni :

Walipaswa waweke mtu wa kutafsiri ni jambo la msingi waandalizi mmelipuuzia, lugha zilizo tumika na hao wahubiri wawilli wageni ni za Kiarabu na Kingereza ambazo zinawapiga chenga kubwa waliohudhuria hata kufuatilia katika majukwaa mbalimbali ya mawasiliano, ilipaswa akiongea kila baada ya nukta tafsiri inaletwa wangenufaika wengi zaidi na Kwa kiasi kile kile na Kwa hisia Ile Ile....lakini kutafsiri Kwa namna hii walio iweka Ile ladha inapungua na kutoweka kabisa
 
Waumini walalamika :

1 day ago

View: https://m.youtube.com/watch?v=ipig0nJIhIc
wamemfungia mhadhiri wa kimataifa Dr. Zakir Naik msikitini unamuulizaje, mtu anauliza swali yuko nje.

Mhadhara ukumbini ambapo kila mtu wa imani yoyote anaingia, na sio huo upuuzi wa kufungiana ndani waislam watupu. Eti wakristo wako nje.

Zanzibar mmetia aibu, na hata uyo mwenyewe Dr. Zakir Naik hajapenda ndo mana kawa mkali sana leo 31 December 2024 ndani ya Masjidi Zanjibar Zanzibar

Mdau mwingine :
Hakika lugha gongana imeleta changamoto :

Kujua lugha nyingi ni sunnah katika uislam ili uweze kulifikisha neno lake .napia mungu ndo kaumba hayo makabila na lugha. quran itasomwa kiarabu na tafseer inatumika lugha yoyote mpk kisukuma ukitaka unatfsiriwa tu .
 
Dr. Zakir Naik mhubiri wa kimataifa akutana na rais wa serikali ya mapinduzi Zanzibar aliye mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dr. Hussein Mwinyi

View: https://m.youtube.com/watch?v=UmzV1AExecw

Mheshimiwa rais wa SMZ Dr. Hussein Mwinyi asema ziara hiyo ni kwa ajili ya kueneza dini hiyo ya kiIslamu na pia ujio huo wa muhubiri huyo ataweza kusaidia utalii wa Halal na, rais anatumaini muhubiri huyo kupata wasaa wa kuzunguka maeneo kadhaa ya Zanzibar ili kuionesha dunia fursa ya utalii wa kifamilia wa Halal Tourism na inshallah kama itawezekana afike tena wakati wa mfumo wa Ramadhani aendelee kutoa daawa na darsa kwa waumini.
 
AZAM MEDIA LTD PAMOJA NA THE ISLAMIC FOUNDATION …

UJIO WA DR ZAKIR NAIK TANZANIA - RATIBA YAKE YOTE

TAREHE 2/01/2025 DIAMOND JUBILEE DAM KUANZIA SAA 1 USIKU HADI SAA 6 USIKU

Muhubiri wa kimataifa Dr. Zakir Naik atatoa muhadhara nyote mnakaribishwa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

Source : DAU TV Tanzania (TZ)
 
Dr. Zakir Naik mhubiri wa kimataifa akutana na rais wa serikali ya mapinduzi Zanzibar aliye mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dr. Hussein Mwinyi

View: https://m.youtube.com/watch?v=UmzV1AExecw

Mheshimiwa rais wa SMZ Dr. Hussein Mwinyi asema ziara hiyo ni kwa ajili ya kueneza dini hiyo ya kiIslamu na pia ujio huo wa muhubiri huyo ataweza kusaidia utalii wa Halal na, rais anatumaini muhubiri huyo kupata wasaa wa kuzunguka maeneo kadhaa ya Zanzibar ili kuionesha dunia fursa ya utalii wa kifamilia wa Halal Tourism na inshallah kama itawezekana afike tena wakati wa mfumo wa Ramadhani aendelee kutoa daawa na darsa kwa waumini.

Hàya mambo yalileta shida sana kipindi cha baba yake Hussein, mzee Alli hàssan Mwinyi.
Sàsa ànayaanzisha na bi ushungi. Sishabikii mihadhara ya kujadili dini usiyoiamini. Hii kitu mbaya sana maana kila muumini anaona Mungu wa mwenzake ni shetani tuu.
 
Back
Top Bottom