Dragon fruits mdogomdogo inaanza ingia sokoni

Tunda lenye faida nyingi sana mwilini na Wazungu, Wachina, wahindi wanayapenda sana haya matunda, Wachina ndio usiseme.
 
Nilikuwa nishakupandisha kiwango kukuona bonge la smart man unafunga kware unakula mayai ya kware ..huo' mkono wa mwarabu cjui Mzungu ndio nikajua kumbe umetoa mtandaoni [emoji1]
Kwa hio wewe una tatizo na Mkono mweupe? vipi ungekuwa mkono mweusi na still nisiwe mimi? yaani shida kuu kwako ni mkono mweupe? Aisee, Unataka ya mkono mweusi? Ubonge wa smart unanisaidia chochote kile? Take time mkuu
 
Nilikuwa nishakupandisha kiwango kukuona bonge la smart man unafunga kware unakula mayai ya kware ..huo' mkono wa mwarabu cjui Mzungu ndio nikajua kumbe umetoa mtandaoni [emoji1]
Kware nafuga kitambo sana, nakula yes sana nyama yake, kwa wiki naka sio chini ya kware 35 hadi 40. Shida iko wapi?
 
Tulianza na aloe vera,mafuta ya ubuyu, mayai ya kwale, almond,mbegu za maboga,mkojo wa sungura,kilimo cha nyoka, Tikiti elfu 1 kwa eka, ufugaji wa mende na sasa tumefika kwenye Kilimo cha Dragon

Job kweli kweli.
Nchi imejaa watu ambao kiwango cha kuwaza kimekita kwenye tope, ni sawa na gari difu ikite chini sasa ndio watu kama hawa
 
Hilo tunda halina cha ajabu chochote. Ni tunda tu kama matunda mengine. Kwa sasa kuna wenye nazo watajisikia spesho sana kula hilo tunda (waache wapigwe), ila baadaye uzalishaji ukiwa mwingi, hata sisi wengine tutakula tu.
 
Ghari = Ghali
 
Mayai ya kware yanautofauti gani na mayai ya kuku. Nyama ya kwareninatifauti gani na nyama ya kuku?
Dunia inabadilika sana ila kuna watu hawabadiliki, nimesoma maswali ya wadau hapa yanatia huruma.
1. Dragon Fruit ni biashara kubwa sana na matunda yake yanauzwa aghali sana hapa Mwanza Sh 15,000/ moja na yanatoka Kenya.
2. Almond anayesema naona hazijui hebu aende Supermarket akaulizie bei yake hata Korosho haifikii na bado watu hawajashtulia kuzilima.
3. Kwale Bora umewawekea picha, nilikwenda Dodoma jamaa yangu akinitaka twende mnadani tulale Kuku, tulipofika akamuita muuzaji atuletee kuku wachanga, sikuelewa nikahoji kuku wakubwa wapo iwekee tule wachanga, akacheka akanieleza ni wazuri Sana walupofikika akanieleza hawa mie huwaita Kuku wachanga sababu ni watodo lakini waita ni Kwale. Ni biashara kubwa sana watu wanatajirika nayo.
3. Mafuta ya ubuyu, mafuta ya mlonge, mafuta ya Vitunguu swaumu, mafuta ya karanga watu wanazalisha na bei ni mbaya.
Kwa kifupi Jambo usilolijua ninusiku wa Giza unachokiona hakifai kwako ni fursa kwa wengine na wanasomesha watoto na maisha yanasonga mbele.
 
Mbona mnatumia nguvu sana kutushawishi
 
..labda dragon fruit itakuja kuwa kilimo kikubwa kama parachichi.

..watu wa mwanzo kulima parachichi kibiashara walionekana wendawazimu.
 
Wakuu, pale songea mjini nilipita Siku moja kuna matunda wanaita "matunda Mungu", niya msimu, Ni matamu sana, madogo Kama embe, Ila matamu kuliko papai, Yana rangi ya kijani, sijawahi kuyaona mkoa mwingine wowote

Yalikuwa yanauzwa sh 200 au Mia, miaka mtatu iliyopita, yanauzwa sokoni au na akina mama waotembeza kwenye dishi, kuna mtu amewahi kuona tunda hilo mkoa mwingine?, japo huenda jina likawa tofaiuti
 
βœ…πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ™
 
Hayo matunda yenyewe ya kichina,
Kuleni matakapela nyinyi na mapapai,nanasi,embe,machungwa,machenza yamejaa popote pale,we unaendaje kula tunda lina rangi ya Pink?
Mkuu, unafahamu asili ya hayo matunda uliyoyataja?
1. Mapapai yalitoka South America

2. Maparachichi (makatapela/makatapera) yalitoka South America

3. Maembe yalitoka Asia

4. Machungwa yalitoka pande za China

5. Hata nanasi inawezekana asili yake si bara la Afrika.

Kama haifai kula PITAYA (dragon fruits) kwa kuwa ni matunda ya kigeni, na hata hayo mengine nayo hayafai. Yote ni ya kigeni.

Lakini kama unazingatia afya, MSHOKISHOKI (dragon fruits) ni moja ya matunda yenye faida sana kiafya. Binafsi ninatamani niwe ninayala kila siku, ila upatikanaji wake huku niliko ni adimu. Hayapo kabisa, na wala hayajulikani.
 
Tulianza na aloe vera,mafuta ya ubuyu, mayai ya kwale, almond,mbegu za maboga,mkojo wa sungura,kilimo cha nyoka, Tikiti elfu 1 kwa eka, ufugaji wa mende na sasa tumefika kwenye Kilimo cha Dragon

Job kweli kweli.
Mkuu, unamaanisha fursa zimeendelea kuongezeka au kinyume chake?

Natamani sana Mataifa ya kware, naweza kupata wapi?

Ni wapi ninaweza kupata kware wa kuwafuga?
 
Hata panya kuna watu wanaofuga kibiashara.

Mbegu ya maboga nishawahi kununua mara kadhaa supermarket
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…