Dunia inabadilika sana ila kuna watu hawabadiliki, nimesoma maswali ya wadau hapa yanatia huruma.
1. Dragon Fruit ni biashara kubwa sana na matunda yake yanauzwa aghali sana hapa Mwanza Sh 15,000/ moja na yanatoka Kenya.
2. Almond anayesema naona hazijui hebu aende Supermarket akaulizie bei yake hata Korosho haifikii na bado watu hawajashtulia kuzilima.
3. Kwale Bora umewawekea picha, nilikwenda Dodoma jamaa yangu akinitaka twende mnadani tulale Kuku, tulipofika akamuita muuzaji atuletee kuku wachanga, sikuelewa nikahoji kuku wakubwa wapo iwekee tule wachanga, akacheka akanieleza ni wazuri Sana walupofikika akanieleza hawa mie huwaita Kuku wachanga sababu ni watodo lakini waita ni Kwale. Ni biashara kubwa sana watu wanatajirika nayo.
3. Mafuta ya ubuyu, mafuta ya mlonge, mafuta ya Vitunguu swaumu, mafuta ya karanga watu wanazalisha na bei ni mbaya.
Kwa kifupi Jambo usilolijua ninusiku wa Giza unachokiona hakifai kwako ni fursa kwa wengine na wanasomesha watoto na maisha yanasonga mbele.