Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 6,236
- 10,774
Katika miji kama Dar es Salaam, Dodoma na Arusha, matangazo ya Blockchain Masterclass yamekuwa kama matangazo ya tamasha la muziki—kila wiki yapo, kila kona yanavutia sana. Ahadi ni ile ile: “Jifunze teknolojia ya baadaye, badilisha maisha yako.” Lakini tujiulize je, haya madarasa yanaendana na uhalisia wa kisheria nchini?
Angalizo:
Kwa namna yoyote ile sina nia mbaya kwa walimu na wakufunzi wa semina na madarasa ya Blockchain Masterclass! Andiko hili lipo kwa ajili ya kuelimisha na kuongeza nguvu pamoja na kutoa hoja pekee, na wala sitangazi biashara la huduma yoyote.
Kwanza, tukubali ukweli: Blockchain ni teknolojia nzuri, bora na halali ikiwa ni yenye matumizi mapana duniani—kuanzia fedha za kidijitali hadi mifumo ya mikataba (smart contracts). Lakini hapa Tanzania, mfumo wa sheria bado uko hatua za awali na nyuma katika kuikumbatia kikamilifu teknolojia ya namna hii.
Kwa mfano, Benki Kuu ya Tanzania imewahi kutoa tahadhari na taarifa kadhaa kuhusu matumizi ya sarafu za kidijitali (cryptocurrencies), ikisisitiza kuwa hazitambuliwi kama fedha halali nchini. Hii ina maana kuwa ingawa unaweza kujifunza Blockchain darasani, matumizi yake hasa kwenye fedha yana mipaka ya kisheria. Hapa ndipo tofauti kati ya “maarifa” na “matumizi halali” inapojitokeza.
Aidha, sheria za usimamizi wa miamala ya kielektroniki na ulinzi wa taarifa, kama Electronic Transactions Act na Personal Data Protection Act, zinaanza kugusa maeneo yanayoweza kuhusiana na Blockchain moja kwa moja, hasa kwenye usalama wa taarifa na miamala. Hata hivyo, hakuna sheria mahsusi inayosimamia moja kwa moja Blockchain au smart contracts kwa undani.
Ni jambo jema sana kuona baadhi ya madarasa haya yanafundisha teknolojia hii ila ni teknolojia ambayo bado haina mwongozo kamili wa kisheria nchini kwetu. Ni kama kufundishwa kuendesha gari la CyberTruck ukiwa Sengerema Vijijini.
Kwa upande wa uhalisia wa madarasa yenyewe, hali ni mchanganyiko na mkanganyiko mkubwa sana. Zipo zinazotoa elimu ya msingi yenye manufaa—hasa kwa vijana wanaotaka kuingia kwenye sekta ya TEHAMA. Lakini pia zipo zile semina zinazofanana na zile hadithi za zamani za QNET au AIM Global, ambapo msisitizo mkubwa uko kwenye “fursa” kuliko ujuzi.
Kitaalamu unaweza kuingia darasani ukitarajia kujifunza blockchain architecture, ukaishia kujifunza jinsi ya “kuamini ndoto zako kwa nguvu zote!” na kuuziwa kitabu cha motivational speaker kwa buku tano.
Blockchain Masterclass zinaweza kuwa na faida, lakini sio tiketi ya utajiri wa haraka ama ule wa pupa. Na muhimu zaidi, kabla ya kuwekeza muda au pesa, jiulize—je, kile ninachofundishwa kinaendana na mazingira ya kisheria ya Tanzania? Kwa sababu katika dunia ya teknolojia, si kila kinachowezekana, kinaruhusiwa.