kibaravumba
JF-Expert Member
- Dec 21, 2012
- 6,634
- 7,015
Hawa watu wana mbinu nyingi sana za ku-survive katika mazingira yoyote kwenye nafasi zao.
Sakata la wazee wa Yanga unaeweza kufikiri viongozi hawajui. La hasha! Wanafahamu sana na ukweli inaonesha anayelengwa hapo ni GSM. Viongozi hawamtaki na kwa vile wameshamwona Manji, wanatengeneza fitna ili Manji akabidhiwe timu. Walijua nini wale wazee wataongea.
Ni hawa hawa viongozi, wamefanikiwa kuwaaminisha wanachama wao kuwa Sarpong hafungi kwa sababu ya TFF. Kila mwanachama wa Yanga anajua kuwa timu inaonewa na TFF ndio maana haijapata ubingwa. Hii mbinu ya kuhamishia malalamiko kwa watu wengine ni mbinu iliyowasaidia sana kwa vile hata wanachama wao huwa hawafikiri vizuri na wanawaunga mkono.
Hofu ya kufungwa na Simba imewafanya watafute sababu na kwa kupitia kiongozi mmoja, mwana Yanga, mwenye wadhifa mkubwa serikalini, walimtumia kuhakikisha mechi inasogezwa mbele masaa kadhaa ili wapate sababu ya kuikwepa Simba. Waliganikiwa kwa hilo kwani hadi sasa TFF ndio wameangushiwa jumba bovu.
Katika timu iliyonufaika sana na udhaifu wa waamuzi kuliko timu yoyote nchi hii ni yanga. Walifanikiwa baada ya kuwatisha waamuzi na waamuzi wamekuwa wakiwabeba sana ili wasilaumiwe. Bahati mbaya tu nao hawabebeki. Akiba Kalinho wameondoka clubuni kisa TFF inaonea yanga. Mchezaji aliyesifiwa sana na kanjanja moja wa uchambuzi wa michezo, Ntibanzokiza, hatujui nini kimemkuta ila kwa mujibu wa viongozi wa yanga ni TFF inawaonea.
Wamefukuza walimu kadhaa, lakini sababu kubwa kwao na wanachama wao ni TFF inawaonea sana yanga. Wao hawajawahi kukosea. Timu ya wananchi inaezaje kukosea?