Draw ya CAF kwa timu za Africa

Draw ya CAF kwa timu za Africa

Underdog huwa anaanzia nyumbani ili ajenge confidence. Halafu mambo ya kulalamikia kupangiwa mwarabu si ya kimichezo. Kama timu imeingia kwenye mashindano, haina budi kuwa tayari kucheza na yeyote, sio kulalamika eti upangiwe na fulani. Mwaka 2003 Simba ilianza nyumbani kama underdog, lakini ikawang'oa mashindanoni mabingwa watetezi wa kombe la Klabu Bingwa Afrika, yaani Zamalek, tena kwa wakati ambao ndio walikuwa wametoka kutwaa tena kombe la ligi ya Misri. Jamaa walikuwa wamepanga kufanya sherehe ya ubingwa wa nchi yao baada ya mechi na Simba, lakini wakalazimika kuifuta sherehe kutokana na hali iliyotokea kiwanjani
 
Raha ya mashindano haya ni kuingia hatua ya makundi (robo fainali) kwani kuanzia hapo ndipo CAF huwa inatoa ruzuku kwa timu zinazoshiriki, na mamilioni hayo yanaongezeka kadiri unavyopiga hatua. Lakini kama kila mwaka unatolewa raundi ya pili, hiyo ni hasara kubwa na ni heri usishiriki, kwani hapo unakuwa ni mtu wa kuzitumia tu hela kuliko kuzipata
 
...shida hapa ni draw; huwa wanaifanyia wapi?,kwanini tuletewe jina la muarabu kila mwaka,hayo majina hupatikana wapi/vipi?
Draw hufanyika makao makuu ya CAF Misri kama UEFA wanavofanyia Uswisi .Ili kuepuka na waaojua sio waarabu tu (lazima tuboreshe viwango vya timu zetu na kuwafunga
 
Hapa misioni sababu ya kudai droo ya wazi.Kama timu nzuri hao waarabu lazima watoke tu!sisi wenyewe mpira tunachezea magazetini.
 
CAF hawafanyi draw live wahuni sana wanapendelea timu za North africa
 
Wanasema nch zile ambazo zipo kwenye kumi bora vilabu vyao hupewa upendeleo wa ratiba Pamoja na kupewa timu zinazoning'nia kwenye ubora
 
Leo CAF wanafanya draw Cairo Misri ya round ijayo kwa kombe la klabu bingwa na kombe la shirikisho la Afrika
 
Kwanza inatakiwa timu zicheze hatua ya makundi ndo zianze knockout stage
CAF wapumbafu tu
Ipo kienyejienyeji tu
 
Back
Top Bottom