DRC: Kidiaba ateuliwa kuwa Waziri wa Michezo

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,621
Reaction score
8,411
Rais Felix Tshisekedi ame.teua Robert Kidiaba kuwa Waziri wa Michezo wa Taifa hilo

Robert Kidiaba aliwahi kuwa mlinda mlango wa Klabu ya Soka ya TP Mazembe na Timu ya Taifa ya DRC

Katika Uchagu Mkuu wa DRC uliofanyika mwezi Januari, 2019 alichaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Katanga

Wakati akicheza soka Kidiaba alijizolea umaarufu kwa aina yake ya kushangilia kwa kusota kwa kutumia makalio
 
Hongera kwake, naamini ataitendea haki hiyo nafasi kama alivyofanya akiwa goalkeeper wa TP mazembe.
 
Na sisi Samata akistaafu soka tunampa uwaziri wa michezo......!
 
mh!Tayari hapo kuja kuipita DRC kwenye michezo tusahau.Maana kidiaba ni mtu aliyekulia kwenye michezo.Sisi wa kwetu ni mwanasheria,hata sheria za mpira wa miguu hazijui
 
Bado tuna safari ndefu ya uandishi na waandishi ktk nchi yetu. Chombo cha habari kinatoa habari ambayo sio sahihi kwa umma. Robert Kidiaba ni waziri wa michezo ktk jimbo lake na sio taifa. Vyombo vya habari pateni muda kusoma na kujua mifumo ya kiutawala ya nchi kabla kukurupukia habari
 
mh!Tayari hapo kuja kuipita DRC kwenye michezo tusahau.Maana kidiaba ni mtu aliyekulia kwenye michezo.Sisi wa kwetu ni mwanasheria,hata sheria za mpira wa miguu hazijui
LA 343inches city
 
Mkuu kulikuwa na mpango wa kuipita Congo DRC katika michezo? mbona usianze kujikumbusha ya Simba, As Vita na Tp Mazembe!
mh!Tayari hapo kuja kuipita DRC kwenye michezo tusahau.Maana kidiaba ni mtu aliyekulia kwenye michezo.Sisi wa kwetu ni mwanasheria,hata sheria za mpira wa miguu hazijui
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…