love life live life
JF-Expert Member
- Sep 12, 2021
- 2,584
- 3,051
Hayo umesema wewe.Sisi Ni nyani
Wao Ni Binadamu.
Nimekuelewa.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hayo umesema wewe.Sisi Ni nyani
Wao Ni Binadamu.
Nimekuelewa.
Sasa Kuna Umuhimu gani wa kuwa na Jumuia ambayo wanachama wana Malengo tofauti? Ni sawa na Kuleta Mafundi Wawili(Mmoja Mjenzi na Mwingine Fundi Cherehani) harafu eti wakutengenezee Gari iliyoharibika. Ni Kichekesho kitupu,Nyani tu ndio anaweza kufanya hayo maamuzi.Hayo umesema wewe.
Jumuiya zetu ni kuviziana tu, kenya na Rwanda wana vizia ardhi,Sasa Kuna Umuhimu gani wa kuwa na Jumuia ambayo wanachama wana Malengo tofauti? Ni sawa na Kuleta Mafundi Wawili(Mmoja Mjenzi na Mwingine Fundi Cherehani) harafu eti wakutengenezee Gari iliyoharibika. Ni Kichekesho kitupu,Nyani tu ndio anaweza kufanya hayo maamuzi.
Ndio maana nikwambia kwamba Hata hizo Mbwembwe za DRC kupata amani ya Kudumu Kisa kujiunga EAC Ni Ndoto za Mchana. EAC haiingilii Mambo ya ndani ya nchi Mwanachama. Na hii IPO Kimakusudi ili Kulingana kutokukosoana.Jumuiya zetu ni kuviziana tu, kenya na Rwanda wana vizia ardhi,
Kesho mnakubaliana hakuna kuimport bidhaa flani kutoka nje kesho Kenya ana import.
Tanzania sijui anavizia nini burundi ni mtoto wetu anamfuata baba same to Congo.
Hilo halina ubishi ila uswahiba unaweza fanikisha.Ndio maana nikwambia kwamba Hata hizo Mbwembwe za DRC kupata amani ya Kudumu Kisa kujiunga EAC Ni Ndoto za Mchana. EAC haiingilii Mambo ya ndani ya nchi Mwanachama. Na hii IPO Kimakusudi ili Kulingana kutokukosoana.
Hopefully it sunk into your skull which is full of shonde.Porojo miiingiii...
Hakuna Uswahiba uliowahi kufanikisha Amani Barani Afrika. Uswahiba wa Marais Ni Kunyemelea Utajiri wa DRC. Tumeona Kenya,Rwanda na Uganda wakianza kujisogeza karibu na DRC. Kenya imeshanunua Ekari za Kutosha huko DRC kwa ajili ya kulima NGANO. Rwanda inataka vitalu vya Madini huko KIVU KUSINI. Kidogo Uganda ndio inaweza kuwa bega kwa bega na DRC kupambana na Waasi baada ya Waasi kuanza kuvuka mipaka na kuvamia Uganda.Hilo halina ubishi ila uswahiba unaweza fanikisha.
Tanzania imeingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine kwa mualiko wa maswahiba sio ajabu.
Rafiki mwaminifu ni Tanzania tu kwa Congo.Hakuna Uswahiba uliowahi kufanikisha Amani Barani Afrika. Uswahiba wa Marais Ni Kunyemelea Utajiri wa DRC. Tumeona Kenya,Rwanda na Uganda wakianza kujisogeza karibu na DRC. Kenya imeshanunua Ekari za Kutosha huko DRC kwa ajili ya kulima NGANO. Rwanda inataka vitalu vya Madini huko KIVU KUSINI. Kidogo Uganda ndio inaweza kuwa bega kwa bega na DRC kupambana na Waasi baada ya Waasi kuanza kuvuka mipaka na kuvamia Uganda.
Tanzania Ni Kubwa Jinga kwa Mda MREFU. Manfesto ya Tanzania imeshabadilika,Tanzania inafocus Mambo yake ya ndani hasa uchumi kuliko kupambana Kijeshi nje ya nchi Kama ilivyokuwa miaka ya 60's.Rafiki mwaminifu ni Tanzania tu kwa Congo.
Ngoja tuone.
Jumuiya zetu ni kuviziana tu, kenya na Rwanda wana vizia ardhi,
Kesho mnakubaliana hakuna kuimport bidhaa flani kutoka nje kesho Kenya ana import.
Tanzania sijui anavizia nini burundi ni mtoto wetu anamfuata baba same to Congo.
Kama huwezi kupambana nao ungana nao!!DRC ndani ya EAC: Nini maana yake?
Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) leo wanatarajia kukubali Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kuwa mwanachama wake wa saba katika mojawapo ya matukio yenye maana kubwa kiuchumi, kisiasa na kijamii katika eneo la Maziwa Makuu.
DRC - ikiwa na watu takribani milioni 92, litakuwa ndiyo taifa lenye watu wengi zaidi miongoni mwa nchi wanachama na kutaifanya EAC sasa kuwa jumuiya yenye soko la takribani watu milioni 260. DRC ni kubwa kieneo na inapakana na takribani nchi tano wanachama wa jumuiya hiyo - kwa maana ya nchi zote kuondoa Kenya. Nchi wanachama wa EAC ni Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na Sudan ya Kusini.
Hatua hiyo ya wakuu wa EAC kupitia mkutano wao utakaofanyika kwa njia ya mtandao leo, ni hitimisho la safari ya takribani miaka 10 - iliyoanza wakati wa utawala wa Rais Joseph Kabila na kuhitimishwa kwa zoezi la uhakiki lililoongozwa na Katibu Mkuu wa EAC, Dk. Peter Mathuki, kati ya Juni na Julai mwaka huu.
Mwisho wa Twitter ujumbe, 1
Rais Felix Tshisekedi wa DRC ameonyesha hamu kubwa ya taifa lake kujiunga na jumuiya hiyo na alitumia sehemu kubwa ya maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa taifa lake mwaka huu kueleza namna taifa lake lilivyokuwa tayari kuwa mwanachama mpya wa EAC.
Kwanini Tshisekedi na Wakongomani wana hamu ya kujiunga muungano huu?
Jiografia
Kijiografia, hakuna nchi nyingine yenye sifa ya kuwa mwanachama wa EAC kuizidi DRC. Mojawapo ya masharti ya mwanzo ya kuwa mwanachama wa jumuiya hiyo yalikuwa kwamba nchi ni lazima iwe inapakana na mojawapo ya nchi wanachama lakini taifa hili mashuhuri duniani linapakana na nchi zote wanachama.
Kuondoa ujirani mwema huo, Wakongomani ni kama vile walikuwa wanachama wa EAC hata kabla ya nchi yao kuwa mwanachama rasmi wa jumuiya. Kwa mfano, kwa muda mrefu, DRC ilikuwa inaongoza kwa kutumia bandari ya Dar es Salaam kupitishia mizigo yake kuliko nchi wanachama, muziki wenye asili ya taifa hilo ukiwa mashuhuri katika nchi zote za Afrika Mashariki na watu wake mbalimbali wakiweka makazi yao ya kudumu katika nchi tofauti inazopakana nazo.
Je, DRC inaweza kuwa sehemu ya Jumuiya ya Afrika MMashariki
Miongoni mwa nchi wanachama wa EAC, pengine hakuna taifa ambalo watu wake wametapakaa katika nchi zote za jumuiya hiyo - Wakongomani wakijulikana kwa tabia yao ya kutoogopa kutafuta riziki popote nje ya taifa lao - tofauti na wananchi wa baadhi ya nchi wanachama wengine ambao si watu wa kuhangaika duniani kutafuta maisha.
Kwa sababu hiyo, kijiografia na kiutamaduni, DRC ilikuwa mwanachama wa EAC miaka mingi kabla hata haijapata fursa hii ya kukaribishwa rasmi kuwa mwanachama wa sita.
Wakati jumuiya ikionekana kuzidi kutanuka, ni vigumu kuona taifa lingine litakalokuwa na "wenyeji wengi walio wageni "kuzidi ujio huu wa taifa lililokuwa likijulikana kama Zaire wakati wa utawala wa Mobutu Sesesseko.
Uchumi
Kwa sasa, Pato la Nchi Wanachama wa EAC linafikia kiasi cha dola bilioni 193 na ujio wa DRC utaongeza pato hilo kwa dola bilioni 50 zaidi kufikia dola 240. Hiki ni kiwango kikubwa kuongezwa na nchi moja katika eneo la dunia linalofahamika kwa umasikini mkubwa.
Lakini siri kubwa iko katika soko. Kwa sababu ya matatizo mbalimbali ya kijamii, kisiasa na kiuchumi, DRC inaonekana kama nchi ambayo bado fursa zake hazijatumiwa ipasavyo na wananchi wake lakini pia na nchi Jirani.
Hata kabla ya kuiruhusu DRC kuingia EAC, viongozi wa juu wa nchi wanachama kama vile Uhuru Kenyatta, Paul Kagame na Yoweri Museveni wameonekana kujisogeza karibu na Tshisekedi.
Kuna mpango wa Afrika wa kuunganisha upande wa Mashariki na Magharibi - kutoka Bahari ya Hindi hadi Atlantic na DRC ni mojawapo ya nguzo muhimu kwenye jambo hilo kubwa.
Kuna mpango wa kujenga barabara kupitia mradi wa TAH8 unaounganisha bandari ya Mombasa, Kenya kwenda katika jiji la Younde, Cameroon na kisha Atlantic. Hizi ni mojawapo ya miradi mikubwa ya miundombinu barani Afrika inayotazamwa kwa jicho la kipekee na Umoja wa Afrika.
Rais Museveni amewahi kuzungumza huko nyuma kwamba tatizo kubwa la Afrika ni ukosefu wa masoko kwa ajili ya bidhaa zinazozalishwa ndani ya nchi na ujio wa taifa lenye watu milioni 92 unamaanisha soko kubwa kwa bidhaa za nchi wanachama wa EAC.
Usalama
Mara zote ukubwa wa DRC umekuwa na changamoto za kiusalama kwa nchi wanachama. Rwanda na Uganda zimekuwa zikisumbuliwa na makundi ya waasi yanayojificha katika misitu minene ya DRC. Lakini pia nchi hizo mbili zimewahi kupigana zenyewe ndani ya taifa hilo kwa sababu ya kuwania kuwa na ushawishi kwa viongozi wa DRC.
Ni matarajio ya viongozi wa EAC kwamba kuwa na DRC ndani yao kutasaidia kujenga mipango itakayowezesha urahisi wa kudhibiti vikundi vya waasi na ugaidi lakini pia kufanya biashara kwa Pamoja badala ya kudhulumiana.
Kuna dhana kutoka katika baadhi ya jamii ya Wakongomani kwamba Rwanda na Uganda wamekuwa wakitumia utajiri wa taifa lao kwa faida yao kwa kutumia visingizio vya kiusalama.
Amani ya kudumu katika eneo la maziwa makuu itasababisha viongozi wa nchi husika sasa kutumia nguvu zaidi katika kujenga uchumi na ushirikiano badala ya kupanga namna ya kufanya uvamizi au kutumia kisingizio cha kupambana na ugaidi au uasi kupora mali za DRC.
Ndoto ya Waasisi
Hatua ya DRC kuingia EAC inachukuliwa pia kama kutimia kwa ndoto za waasisi wa siasa za Umajumui wa Afrika walioamini kwamba namna pekee kwa Afrika kusonga mbele ni kwa kuwa na umoja wa kisiasa na kiuchumi miongoni mwao.
Wakati Tshisekedi akitaka DRC iingie EAC, alikuwa anatimiza ndoto za Patrice Lumumba, Julius Nyerere, Milton Obote na Jomo Kenyatta. Ni matarajio ya wachambuzi wa masuala ya ushirikiano kwamba muda si mrefu nchi kama Somalia, Congo Brazaville na Ethiopia nazo zinaweza kutaka kujiunga na jumuiya hiyo.
Kwa kufanya hivyo, nchi wanachama wa EAC wanaweza kuwa na uwezekano wa kuwa na kura moja kwenye masuala muhimu yanayohusu mustakabali wa eneo la Maziwa Makuu na Afrika kwa ujumla - bila kuzingatia tofauti za lugha wanazozungumza.
Ni jambo zuri kwamba Museveni ambaye ndiye kiongozi mwenye ari zaidi ya mtangamano wa Afrika yuko madarakani bado na jambo hili linaendana na ndoto zake za muda mrefu za kuunganisha Afrika kwa mafungu.
Changamoto
Takribani miaka 10 iliyopita, Sudan Kusini iliingia EAC kwa mbwembwe na furaha kubwa. Wengi walitaraji makubwa kutoka katika taifa hilo. Hata hivyo, kuwepo kwake kwenye jumuiya hakuonekani kupunguza chochote kwenye migogoro na sintofahamu miongoni mwa vinara wakuu wa taifa hilo.
Kimsingi, hakuna mijadala inayofanyika au jitihada za makusudi zinazofanywa na EAC kuhakikisha nchi hiyo mwanachama inakuwa na amani ya kudumu.
Kwa maneno mengine, kuwa kwake mwanachama wa jumuiya hakujaondoa tofauti zake za ndani na hakujaongeza uwezekano wa nchi wanachama kusaidia kuondoa matatizo yake.
Hili ndilo swali ambalo wachambuzi wanajiuliza sasa kwamba kama DRC itakuwa tofauti na italeta kinachotarajiwa na wengi baada ya kujiunga kwake na EAC. Kama ilivyokuwa kwa akina Salva Kiir na Riek Machar huko nyuma, Tshisekedi anaonekana kuwa na nia na ari kubwa - tatizo ni kwamba haijulikana EAC iko tayari kiasi kuisaidia DRC kusimama vizuri.
Changamoto nyingine kubwa kuhusu DRC inahusu dhamiri za ndani za baadhi ya viongozi wa EAC kuhusu kuwa na taifa hilo jipya kama mwanachama. Kuna nchi zinaitazama Kongo kama taifa la kuibiwa - shamba la bibi, na haijulikani kama tabia hiyo itaondoka au itamea zaidi kupitia muungano huu.
Tayari baadhi ya viongozi wa nchi za EAC wamefanya ziara kwa Tshisekedi kufanya dili kwa ajili ya nchi zao hata kama ya tukio la leo. Ipo hatari ya uhakika kwamba huenda maslahi ya baadhi ya nchi yakagongana huko mbele ya safari na hatimaye nchi zikajikuta zinarudi palepale zilipokuwa awali.
Lakini, leo ni siku ya kusherehekea kuikaribisha DRC ndani ya EAC.
Rafiki mwaminifu ni Tanzania tu kwa Congo.
Ngoja tuone.
Nachomaanisha kama Tanzania itakuwa rafiki basi ndio rafiki wa kumuamin tofautiTanzania Ni Kubwa Jinga kwa Mda MREFU. Manfesto ya Tanzania imeshabadilika,Tanzania inafocus Mambo yake ya ndani hasa uchumi kuliko kupambana Kijeshi nje ya nchi Kama ilivyokuwa miaka ya 60's.
Kiufupi,Tanzania haina Mpango na Amani ya Congo Wala Kuiba Raslimali za Kongo.Tuko kivyetu vyetu tu. Sera yetu ya Mambo ya nje haijabadilika tangu Vita baridi (NON ALLIGNED MOVEMENT).
Sio mimi ni siasa za ujamaa za Mwalimu ambazo madhara yake ni makubwa hasa wakatiMaisha ya leo hamna cha urafiki ila maslahi, hizo pumba za mara urafiki mara undugu ndio zimeifanya Tanzania imekua shamba la bibi miaka yote kila mtu akija mnamkenulia meno na kumuita ndugu kisha anachuma na kujiondokea.
Mnapaswa kutanguliza maslahi yenu kwenye kila kitu, hata miungano ni maslahi, leo hii Zanzibar wamewashinda kete, wao wamekua makini sana kwenye maslahi yao na juzi rais wao kasema hamna cha Mtanganyika kumiliki ardhi kule, ukienda huko unaonwa kama mgeni yeyote yule uishi kwa kutulia, ukimaliza kilichokupeleka geuza rudi Bongo.
Lazima mjifunze kupiga mahesabu ya maslahi sio hizo pumba za ndugu, hata Mchina mnamuita ndugu kisha anachuma.
Tanzania lazma aviziwe kwa sababu ujamaa ulimlaza usingizi wa pono.Siku zote Tanzania ndiye huviziwa tu.....hehehe!!!
Mchawi wa Tanzania ni ujamaaSio mimi ni siasa za ujamaa za Mwalimu ambazo madhara yake ni makubwa hasa wakati
huu ambapo mbwa mkubwa anamla mdogo na kutokula chochote hakukufanyi uwe mwema.
Wanasiasa wetu waisome dunia ya leo wasafiri pamoja nayo vinginevyo tutakuwa wasindikkizaji.
#mchawi wa Tanzania ni ujamaa.
Umeandika maneno mengi mno ambayo hayalengi jambo 1, yametawanyika kwenye angles nyingi ambazo ni nyepesi kuhusishwa moja kwa moja na ujamaa sababu yapo karibu kwenye nchi zote za ulimwengu wa tatuAngalia tu namna raia mpaka viongozi , wanavyo behave ni pure ujamaa.
Na wanatumia ujamaa ku-compromise na ubepari lazima bepari ashinde.
Mjamaa anaenda kufanya mazungumzo na bepari kama ndugu yake bepari anaenda kufanya mazungumzo na mjamaa
kama trade competitor.
Sector zote ni mambo ya ujamaa tu yamejaa angalia elimu ilivyovurugwa na ujamaa...
Vingozi wetu wanatenda kama mabepari (blind capitalism) lakini wanauishi ujamaa wakienda kwenye meza ya mazungumzo
wanaamini bepari atawaonea huruma(hizi ni akili za kijamaa binadamu wote ni sawa/ni ndugu na life is fair).
Raia nao kwa blunder za viongozi wao wanaamini siku moja viongozi wao watatokewa na malaika na kuucha ufisadi akili
za kusema tutamlilia Mungu.
Viongozi wetu wamezaliwa katika ujamaa hawajui chochote kuhusu ubepari wanachojua ubeppari ni soko huria basi.
Nyerere naamini angeendelea kuwepo angeomba msamaha kuhusu ujamaa kama alivyoofanya kwa vijiji vya ujamaa.
Tanzania tunafuata sera ipi katika uchumi?Umeandika maneno mengi mno ambayo hayalengi jambo 1, yametawanyika kwenye angles nyingi ambazo ni nyepesi kuhusishwa moja kwa moja na ujamaa sababu yapo karibu kwenye nchi zote za ulimwengu wa tatu
Bado sijapata point yako kuhusu ujamaa kuwa mchawi wa Tanzania, Ningependa kujua kwa kifupi sababu kubwa kuhusu hiyo hoja.
Inapaswa kuwa tunafuata au tunatekeleza?Tanzania tunafuata sera ipi katika uchumi?
Uchumi huria kwenye raia na viongozi wenye mawazo na akili za kijamaa.Inapaswa kuwa tunafuata au tunatekeleza?
Anyway Tanzania tuna uchumi huria, uchumi wa Tanzania upo huria lakini wenye ushawishi wa ujamaa ndani yake.
Kwa lugha ya kiingereza Tanzania inajulikana kama moja ya Countries with constitutional references to socialism