Dream League Soccer Special Thread

Dream League Soccer Special Thread

Hebu tucheze real games.

Kati yenu kama kuna yeyote anaweza kucheza PS 4 FIFA na yupo Dar tukutane tupige mechi
Kwani nyie game lenu hamchezi online na mtu aliyembali? Basi hamia DLS kumenoga safari hii. Ukitamba sana unapewa code then unaburuzwa
 
Kwani nyie game lenu hamchezi online na mtu aliyembali? Basi hamia DLS kumenoga safari hii. Ukitamba sana unapewa code then unaburuzwa
Kwa bongo ngumu kidogo kucheza online PS 4.

Hili DLS nilicheza kwenye simu ya mshkaji sikupenda graphic yake ila ni zuri kwa kupotezea muda
 
Hapa ni mahala salama kwa mpenzi wa Dream League Soccer(DLS). Game hili limetengenezwa na Kampuni ya FIRST TOUCH SOCCER(FTS). Game la DLS ni game bora zaidi kwa sasa duniani kwa upande wa soccer.

SIFA PEKEE YA DLS.
1. Linachukua nafasi ndogo kwenye simu.
Pamoja na ubora wake wa graphics bado game hii ina 500MB na ni tofauti na magame mengine yanaanza na 2GB mfano PES.

2. Uhalisia wa wachezani wa timu wanazochezea
Kitu pekee kinachotofautisha game hii na magame mengine ni uwezo wa ku update wachezaji kadri timu mpya zilivyo. Mfano Mess kwenye game hii anachezea PSG na magame mengine bado Mess anachezea Barcelona. Mfano FIFA hadi leo Xavi,Iniesta bado wanakipiga soka. Huko kwingine hata ukimtaka Gaucho au Drogba au Maradona au Arteta au Guardiola utawapata na bado wanacheza mpira. Ili kujua sajiri za ulaya na kwingineko karibu DLS utawajua wachezaji wote current.

3. Wepesi wa kucheza .
Game hii haihitaji rocket science ili uweze kucheza kwani vya kuchezea viko 3 tu 1. B kwa ajili ya pass fupi 2. C kwa ajiri ya kuchop,kubadili wa kumchezesha na pass ya juu. 3. A kwa ajili ya shuti na pass ndefu. Vitufe vyote hivi unakadilia kwa kubovya tu ni simple sana kama kuvaa nguo tu.

4. Wachezaji hawatabiriki uwanjani
DLS huwezi kucheza kwa namna moja mfano, uje angle au sehemu fulani ukishuti ni goli au chenga fulani tu. Hili game sio la kukariri kama Real football lenyewe mchezaji akivuka tu mstari wa kati, apige hatua tatu alafu jaza shuti basi ni goli. Hili game ni real kweli yaani kunakipindi hadi unaacha kula.

5. Uwezo wa kucheza kwa kupanda daraja kwa kikosi chako
Huko kwingine unaambiwa chagua timu, na kisha uichezeshe. Huku mambo ni tofauti Kwanza utapewa squad yako na itabidi uipandishe daraja toka Academy, daraja la 4,3,2,1,dalaja la Junior kisha ligi kuu(Legendary). Kuna kupanda na kushuka katika ligi hili kwa hiyo sio ni burudani bulibuli. Pia kuna ligi zingine hapo kati yaani mfano tu wa shirikisho na uefa.

NB: kikosi bora ndicho kinachoshinda. Game ni ya online(kwa ligi zote) na offline kwa friendly match.

View attachment 2099718View attachment 2099719View attachment 2099720View attachment 2099721View attachment 2099722
KARIBU KWA KUPEANA MAUJANJA NA STORI ZA GAME HILI.
Best player kwa game hili ni Ngoro Kante na Mousa Sisoko. Hawa ni wachezaji wenye uwezo mkubwa sana katikati kwa maana wanakaba na kushambulia vizuri.

VITU VYA KUZINGATIA WAKATI WA KUNUNUA MCHEZAJI.
1. Acceleration.
Kabla ya kumsajili mchezaji yeyote kwanza angalia acce yake ili awe na maamuzi ya haraka. Wengi sana wanaangalia speed tu ya mchezaji bila kuona acc yake. Hata ukimchukua mchezaji mwenye speed 100 ila kama acceleration yake ni 27 ni kazi bure kwani atachelewa kuanza kukimbia na ataporwa mpira mda wote.
2. Stamina. Baada ya kuona acceleration basi angalia stamina yake. Hapa panamwezesha mchezaji kukaba kwa nguvu lakini pia hanyang'anywi mpira kirahisi. Viungo na back wawe na stamina kubwa sana isiwe chini ya 75.
3. Speed. Kitu cha tatu ni pendwa kwa wachezaji wengi wa magame yani kukuimbia kwa kasi hasa kwa fowadi na back za pembeni. DLS wanashambulia sana winga hivyo hakikisha back zako namba 2 na 3 wanakuwa na speed kubwa na acceleration kubwa.
NB: usimruhusu adui apige kross ni hatari sana, kabla adui hajapiga kross press A ila uwe kwa pembeni yake na umsogee sana ili apige takoling. Takoling ya mbele ni kwa mbali kiasi ili mpira uwahi kuugusa ili kuepusha umeme.
4. Head.
Kwa beki za kati head nzuri sana kwani mipira ya kona na kross itasaidia sana kuokoa. Uwezo wa kupiga kichwa ni kwa beki na viungo.
5. Shoot na pass.
Kwa fowadi pia lazima uangalie uwezo wao wa kushuti ili hata nje ya 18 uwe unashuti na unafunga. Poor shoot inapelekea kupaisha au shuti kuwa chakula kwa golikipa.
NB. Formation au mfumo mzuri ni 4 4 2 na weka defensive kama unajifunza, moderate kama mchezaji wa kawaida na Attacking kama mzoefu kama mm.
Pia ukifungwa au kufunga unaweza kubadili ili kuendana na mchezo
Mim ninayo ya offline DLS
 
DLS 2020 OFFLINE KWA MECHI ZOTE
Screenshot_20220205-100957.jpg
 
Kwa bongo ngumu kidogo kucheza online PS 4.

Hili DLS nilicheza kwenye simu ya mshkaji sikupenda graohic yake ila ni zuri kwa kupotezea muda
jaribu sasa 2022 na kafanya setting ya graphics
 
DLS mpya huwezi sajili mwenyewe wachezaji mpk Agent uwape mpunga ?

Ipi tofauti ya kimajukumu Kati ya agent na Scout?

Nimetoa mpunga kwa scout coins 500 kaniletea wachezaji uto nikadiscard hapo nikirudi tena kutaka mchezaji inatakiwa nmpe tena au anabaki tu milele km agent wangu akiniletea wachezaji ?
 
DLS mpya huwezi sajili mwenyewe wachezaji mpk Agent uwape mpunga ?

Ipi tofauti ya kimajukumu Kati ya agent na Scout?

Nimetoa mpunga kwa scout coins 500 kaniletea wachezaji uto nikadiscard hapo nikirudi tena kutaka mchezaji inatakiwa nmpe tena au anabaki tu milele km agent wangu akiniletea wachezaji ?
Scout anakuletea wachezaji wazuri ili uwanunue na agent anakuletea mchezaji kulingana na thamani ya Gold ulizomlipia. Mfano 500 Gold anakuletea mchezaji kuanzia 81 hadi 95. Na ukimpa anakuletea yeyote iwe beki,kipa,kiungo au fowadi. Ukienda kule kuna thamani ya kianzia mchezaji. Ushauri ni jaribu kuwa mpole,ww hakikisha tu una coin za kutosha za kununulia mchezaji. Kila game ukicheza nenda sokoni kaangalie anayekufaa, kama hayupo achana nae cheza tena na uangaliie tena hadi utampata wa kuendana nae.
Nb; Boresha nyota(rate) ya timu yako ili uletewe wachezaji wakubwa.
 
HINTS ZA KUPIGA PENALT.
1. Upande atakaopigia awali mpinzani ndio upande wanaopigia 90% ya wachezaji wao wote.
2. Upande wa kwanza atakaorukia golikipa wao, ndio upande atakaokuwa anarukia zaidi.
3. Penalt ya 3 au 4 badilisha Maamuzi ya kupigia au kukamatia.
 
HINTS ZA KUPIGA PENALT.
1. Upande atakaopigia awali mpinzani ndio upande wanaopigia 90% ya wachezaji wao wote.
2. Upande wa kwanza atakaorukia golikipa wao, ndio upande atakaokuwa anarukia zaidi.
3. Penalt ya 3 au 4 badilisha Maamuzi ya kupigia au kukamatia.
Zinanisumbuaga sana penalt, wakati wa kupiga unaweza kuweka direction halafu ukiachia mchezaji anapiga kati
 
Nalijaje kana ni original naama fake ni mengi
Mara nyingi Og unakiwasha ya kwanza ,andika Dream Soccer League 2022 hlfu ikija angalia number of downloads na rate iwe km niliyo screenshot hapo chini
IMG_20220206_192104.jpg
 
Zinanisumbuaga sana penalt, wakati wa kupiga unaweza kuweka direction halafu ukiachia mchezaji anapiga kati
Golikipa usimchezeshe mapema ,ina bidi umhesabu mpigaji penalty yaani ile hatua ya kupiga kabla ya kushuti mchezeshe golikipa wako.
 
Mdau aliye online tukipige
nina mashaka na simu yangu, toka iende kwa fundi network iko down sana. Shida sio operator bali ni device yangu na ndio maana mda wote game online ina forfeit
 
Back
Top Bottom