Driving enthusiasts, Iyovi endesha ukiwa umetulia!

Driving enthusiasts, Iyovi endesha ukiwa umetulia!

Mkuu bado sehemu hizo ni hatari kwa spidi kali.
Nilimwazima shemeji yangu gari akielekea msiba wa baba yake huku Tukuyu.
Hakufika salama.
Gari aliipiga chini hapo Iyovi, aliingia gema- karibu na sehemu sasa inapanuliwa.
Nikapata kibarua cha kuifuata gari, maana yeye ilibidi apate usafiri mwingine kwenda msibani.
Hadi leo, napaheshimu.
Dah pole sana mkuu ilikuwa mbaya kweli yani. Gari haina ufundi kama una overspeed. Mie humo nakatizaga na 80-100 usiku ila gari ya chini.
 
Mkuu Iyovi at 150+ na kona kona zile?
Its almost impossible.
Ndio maana nikatoa tahadhari.
Stretch ya kukamua(hasa usiku), ni Moro- Doma, Ruaha-Comfort, Msitu wa Sao Hill, Makambako-Igawa.
Hapo hali ikiruhusu hata 200-220+ unakamua.
Inawezekana boss ni uwezo tu wa gari na umahiri wa dereva ,mkuu kuna watu hawawezi tembea chini ya 100 hata kwa dk 3.
 
Kipindi kile vi coaster vya hakuna kulala kulikuwa na vizuizi moro na Igumbiro ukichelewa unalala hadi alfajiri,sasa ukutane na dereva mwehu aliyechelewa na anataka kufidia muda,hapo iyovi abiria story zote huisha na wengi hujiapiza kutopanda tena.
 
Back
Top Bottom