Drogba

Mbu

JF-Expert Member
Joined
Jan 11, 2007
Posts
12,752
Reaction score
7,861
Reports: Chelsea Prepared To Sell Didier Drogba Following Barcelona Outburst
Blues owner Roman Abramovich was furious with the Ivory Coast striker's actions following the 1-1 draw with Barcelona at Stamford Bridge on Wednesday...

8 May 2009 07:38:11


...safi sana, kazidi!
 
Hiddink urges UEFA to go easy on Drogba - but striker could still leave Chelsea in the summer

...'kibarua' kimeota majani, sasa aende kwa yule 'Child-minder' wake pale Inter Milan, Jose Mourinho!
 

...Drogba, what goes around comes around! ...kama ulivyomfanyia Big Phil- Scolari nawe kwa wembe huo huo unanyolewa nao! I hate this guy, for real!
 

...duuuh, kumbe hata ROMAN ABRAMOVICH keshatosheka na 'madeko' ya huyu mtu!
 
Mbu uko biased kama magazeti ya UK. Nnachokiona hapa ni ubaguzi wa rangi, hamna cha ziada. Ni kweli Drogba kafanya makosa lakini sioni alichofanya kina tofauti gani na alichofanya kocha wake, Terry na zaidi Ballack,

Nakuhakikishia kama ataondoka Chelsea itawachukua muda sana kupata striker mwenye kufunga magoli muhimu ktk mechi muhimu kama Drogba.

Ukiangalia fomu aliyokuja nayo Hiddink Chelsea kwa kiasi kikubwa ili-rely on fitness ya Drogba, akiwa down utaona mambo yatakavyoenda mrama.

Yakumbuke maneno haya..
 
Ukiangalia fomu aliyokuja nayo Hiddink Chelsea kwa kiasi kikubwa ili-rely on fitness ya Drogba, akiwa down utaona mambo yatakavyoenda mrama.

Yakumbuke maneno haya..
__________________
YAAAAAAAAAAH ni kweli nduguu lakini kama hamna nidhamu ni bora mchukue miaka kumi kupata striker mwenye heshima na adabu amabe atajua umuhimu wa mchezo wa mpira wa miguu..napenda kukuhakishia ajioanavyo mtu ndivyo alivyo ...vile unavyomwona didie ndivyo anavyoishi hata maisha ya nyumbani kwake...nakuhakikishia hili na muda kama ana akili atajutia hili
 
Lakini Chelsea wameshawahi kumuonya?au ndio once and for all....??:hasira lazima wamsamehe maana adrenalin ilikuwa juu sana baada ya mchezo...labda kama alikuwa list ya kuuzwa hata kabla.ila si sababu ile tu....
 
Wengine si wapenzi/mashabiki wa mpira wa miguu.
Alichofanya kaka DROGBA wanafanya wengi ila kwakuwa ni black from AFRICA imekuwa taabu kwelikweli.
ABRAM anataka kumtoa ili aendeleze urafiki wake kwa BALLACK akiwa CHELSEA.
Chelsea watajuta kumkosa KAKA DROGBA
 

MIAFRIKA NDIVYO ILIVYO-NN, Kwa nini kila tunapokosea na kukosolewa tunaingiza racism??????Hata mtoto mdogo kwa kuangalia reaction ya Drogba angejua huyu mtu akili hana.Na siku hio alikuwa na guilty conscious baada ya kumiss two clear chances na two diving for penalties.Huyu amezidi lazima alipe alichopanda.Anataka kujifanya anaipenda Chelsea kuliko Abramovich,swine....
 


Ndugu yangu kwa Mchezaji mwenye kiwango cha kama Drogba awezi kufanya kama alivyofanya, tena mpira ukiwa umemalizika. Ballack alifanya vile ndani ya mchezo na alikuwa anamlalamikia akidhani wamenyimwa Penalt kitu ambacho si kweli kama mlivyoona. Lakini Drogba anamfata mwamuzi kama vile anataka kumpiga!!! Naona Drogba enzi zake zinakwisha kama mchezaji.
 
Lakini Chelsea wameshawahi kumuonya?au ndio once and for all....??:hasira lazima wamsamehe maana adrenalin ilikuwa juu sana baada ya mchezo...labda kama alikuwa list ya kuuzwa hata kabla.ila si sababu ile tu....


Kawaida ya wandimbwisa. Jamaa alishawahi kurusha Coin kwa mashabiki, Jamaa alishawahi kuact kama hivi kwa kumpiga kibao Vidic fainali zilizopita na mengine mengi nimekumbuka haya machache. Sasa hamuoni kwamba mshikaji haambiliki.

Maskini hajijui kama ni foreigner, ina maana ni peke yake alikuwa na hasira na refa? Angali watu smart kama Lampard, Terry na Ashley Cole. Jamaa ni mbwiga sana kazuiwa na Malouda, Guus Hiddink (Kocha wake) na wote kwa muda tofauti bado tuuu. This Guy Suck
 
Drogba ni binadamu kama binadamu wengine hasira alizokuwa nazo ni haki yake maana yule refer alibowa sana maana amewakosedha Chelsea penati napi tena za wazi kabisa, me nahisi alihongwa na barcelona si bure. Inekuwa mie ningemuweka na vibao kabisa kama noma naiwe noma kawanganya chelsea tonge mdomoni.
 
me nahisi alihongwa na barcelona si bure. Inekuwa mie ningemuweka na vibao kabisa kama noma naiwe noma kawanganya chelsea tonge mdomoni.

duh we unasema hivyo msanilo angefanyaje jamani...

yah kama ni kuhongwa waliongwa kuanzia dk 91 zilizowafanya chelsea waamaini mpira umekwisha wakati watu wako uwanjani.......

dk 90 USEMI WA MWISHO...
 
hehehehe anajifanya anamachungu sana kuliko mwenywe timu ataenda Portsmouth sasa
 

Wagjameni,
Kwakweli ndg yetu huyp Drogba amechemka sana last time wakiwa Russia he was key player na aka mess up wenzake wakatolewa this time nayo he was key player again na kwenye game kama hizi jamani tuelewe kuwa mchezaji akiwa uwanjani acheze na sio kutafuta vikosa vidogo vidogo ili upewe penalt, kwanza tukiangalia Drogba alichemka mara ngapi na amekosesha timu yake ushindi kwa upuuuzi upuuzi wake ndani ya uwanja na kwenye nafasi nzuri tena sana tu.

hapo ni kuwa alikwenda kunzenguwa yule refa, kooote huko ni kuvuta watazamaji wote wajue ati alionewa kwa zile penalt huku akijua yeye ndie chanzo cha yote na kaizamisha timu yake.

pale hakuna cha mtu ati kaonewa kwasababu ya rangi wala nini ule ni mpira bwana na wote tuliuona live, kacheshemsha sana yule mshikaji wetu kwani ile ndio ilikuwa nafasi yake ya kung'ara sana. ila ndio ivyo imetokea sasa hatuna cha kufanya.

Mimi sioni sababu ya kumwondoa, na hilo ndio tataizo la wenzetu kwakuwa ana pesa basi hatufai wakati wanajua fika ni wapi pa kurekebisha ni wanataka kutupiana lawama tu.

Mimi ntasema kwamba hizo timu kubwa kubwa kama chelsea na Man U wao ni kununua wachezani kwa bei ya juu sana na kama vile wana unga unga au naweza sema wana assemble wachezaji na hili litawa cost sana na watkuwa na madeni mengi na garama kubwa za kuiendesha timu zao. wachukulie mfano mzuri kwa Arsenal system yao ya kuendesha timu ni mzuri sana ingawa hawapati makombe ila ukichunguza kwa makini utakuja gundua kwa nini wenga wame mwita professa timu haiendeshwi kwa hasara na inawafurahisha washabiki wote duniani kwa mpira unaopigwa pale.

Ila yote soka Je hapa kwetu tunajiweka vipi na Taifa star na wachezaji wa yanga na simba na kusahau mikoa mingine. Je huo si ubaguzi?

Roman Abramovich

 

Drobga alichofanya ni kumzongazonga mwamuzi na sidhani kama alimgusa. Kumzonga mwamuzi kwenye ile mechi karibu wachezaji wote wa Chelsea na Barca (kabla hawajapata bao) walifanya.

Mimi huwa siimbi kiitikio chanyimbo zinazoanzishwa na haya magazeti ya UK, huwa yanatengeneza mabifu na hii si mara ya kwanza. Na mara hii watampata huyu kwa sababu ya rangi yake.
 
hehehehe anajifanya anamachungu sana kuliko mwenywe timu ataenda Portsmouth sasa

Drogba ni hot cake na Waafrika inatupasa tujivunie kipaji cha mshkaji. Nimeskia Real Madrid wameshatenga kitita kumnyakua jamaa kabla hata ya ile gemu iliyojaa vimbwanga.
 
MBU unamchukia huyo jamaa sababu kila akicheza na Gunners anawapiga bao pamoja nayote aliyofanya jamaa anawabeba sana Chelsea
 

Heshima na nidhamu sio lazima viende sambamba na kuleta vikombe mkuu. Soma historia Giuseppe Meazza na maisha yake ya rock n roll lakini akija uwanjani anakipiga kama hana akili nzuri, na mpaka San Siro unaitwa kwa heshima yake. Mcheki Ronaldo the Brazilian, pamoja na makeke yake nje ya uwanja ndiye anayeshika rekodi ya kufunga mabao mengi kwenye World Cup na makombe na zawadi nyengine kibao. The list goes on..and on..

Hivyo hapo Chelsea kama wanataka kum-off-load Drogba wanachagua nidhamu over vikombe , thats good for them.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…