Drones ni game changer kwenye vita

Sasa nimeelewa kwa nini Armenia imesalimu amri kwa Azerbaijan. Zile target zote zilikuwa zinapondwa bila kukosea kwa kutumia drones. Kwa sasa zile mbinu za kale zimepitwa na wakati. Idadi ya Askari si hoja tena. Vita ya sasa ni ya kiteknolijia zaidi.
 
Mkuu naomba nifafanulie kidogo kuhusu hii vita ya Turkey na Armenia ni juu ya nini hasa? RTI
Wakati wa dola ya USSR , Azberzajan na Armenia yote yalikuwa kama majimbo tu ya Urusi ndani ya huo muungano wa Kisovieti. Lakini hata wakati huo hizo sehemu za Nagorno-Karabakh zilikuwa zinagombewa na ya haya majimbo. Hizi sehemu zipo ndani ya Arbezajan ila tu kwa vile wengi wa watu wanaoishi huko wana asili ya Armenia, basi Armenia inadai kuwa ni sehemu ya ardhi yake. Hizo nchi mbili zimekwisha pigana vita vingi kuhusiana na suala hili. Ila Umoja wa Mataifa unatambua kwamba sehemu zinazopiganiwa zipo upande wa Azberjan. Pitia Wikipedia ili kupata taarifa ya kutosha kuhusu sakata hili.
 
Asante sana mkuu.
 
Sisi bado tunafanya mazoezi kwa kutambaa chini ya senyenge. Yaani wenzetu kila kitu wanskirahisisha kupitia technology.

[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Ukitaka kujua msala wa Drone waulizeni Iran, Major General Qasim solomeni, Convoy yake ilikuwa attacked na drone tena iliyombali haswa Saivi drone nyingi zinakuwa na stealth technology ni ngumu kuwa visible kwenye Radar,
 
Sahihi
Bado 'man power' inahitajika kwenye majeshi mfano Kuna baadhi ya operation ya kijeshi ''man power' inahitajika mfano ulinzi wa amani, 'rescue operation' huwezi kutumia drone peke yake.

Sana sana hizo teknolojia zinarahisisha zaidi utendaji wa kazi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…