Droo ya raundi ya awali ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho Afrika

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Droo ya raundi ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) na Kombe la Shirikisho Afrika (CAFCC) msimu wa 2026/27 inatarajiwa kupangwa leo Agosti 6, 2026, katika makao makuu ya CAF jijini Cairo, Misri.

Droo ya Kombe la Shirikisho itaanza saa 8:00 mchana, ikifuatiwa na droo ya Ligi ya Mabingwa saa 9:00 alasiri, ambapo Simba na Yanga watafahamu wapinzani wao.

Malipo/Zawadi za Michuano:
  • Zawadi: Bingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) dola Milioni 6 (Tsh. Bilioni 15.9), huku bingwa wa Kombe la Shirikisho Afrika (CAFCC) akipata dola milioni 4 (Tsh. Bilioni 10.6).
  • Malipo ya Mshikamano: Klabu zitakazoondolewa katika raundi za awali zitapokea dola 100,000 (Tsh. Milioni 265.02).
1786002757730.png

​
Klabu ya Singida Black Stars imepangwa kukutana na Al-Ghazala SC Wau ya Sudan Kusini katika raundi ya kwanza ya awali ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF Confederation Cup) msimu wa 2026/27.

1786015533529.png

Wapinzani wa timu za Tanzania zinazoanzia hatua ya awali

Ligi ya Mabingwa

Mighty Wanderers FC vs Simba SC
Gaborone United SC vs Yanga SC

1786019298095.png

Droo ya raundi ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho Afrika imefanyika, huku Singida Black Stars ikipangwa kucheza dhidi ya Al Ghazala SC Wau ya Sudan Kusini katika raundi ya kwanza ya awali ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Singida itaanzia ugenini katika mchezo utakaochezwa kati ya Septemba 4-6, 2026, kabla ya kurudiana nyumbani kati ya Septemba 11-13, 2026.

Kwa upande wa Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba SC imepangwa kukutana na Mighty Wanderers FC ya Malawi katika raundi ya kwanza ya awali ya michuano hiyo.

Simba itaanzia ugenini kati ya Septemba 4-6, 2026, huku mchezo wa marudiano ukichezwa nyumbani kati ya Septemba 11-13, 2026.

Yanga SC nayo imepangwa kucheza dhidi ya Gaborone United SC ya Botswana katika raundi ya kwanza ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Kama ilivyo kwa Simba, Yanga itaanzia ugenini katika tarehe za Septemba 4-6, 2026, na kumalizia kazi nyumbani kwenye mchezo wa marudiano utakaochezwa kati ya Septemba 11-13, 2026.
 
Kwanini Azam hajaanzia raundi ya kwanza ya awali ..!!? Kwa kumbukumbu zangu hii ni mara ya pili Azam anaanzia raundi ya pili ya awali wakati kiuhalisia points za CAF alizonazo ni chache sana kulinganisha na wenzake
 
Amani complex patawaka moto
Simba Yanga Singida Kvz na Zimamoto bila kusahau Azam ⚽
 
Simba tulitakiwa tuwepo ndani ya Top 10.
Safari hii timu zinazoanzia raundi ya pili ni tatu tu. (Mamelodi Sundowns, Rs Berkane na Pyramids). Zilizobakia zote zinaanzia raundi ya kwanza. Wakati huo huo ukumbuke timu kama FAR Rabat, Al Ahly, Zamalek, na vigogo wengine wengi wanacheza Kombe la shirikisho aka Kombe la Luza.
 
Zamalek anacheza Klabu bingwa.
 
Back
Top Bottom