Kwa hizo timu zote zilizopita hapo na kwa mpira anaocheza Liverpool, nampa nafasi kubwa sana ya kufika mbali akipangiwa na timu yoyote hapo.
Tumeuona mpira waliocheza Juventus umekuwa wa kujilinda sana hasa akipata goli.
Barca wako wepesi sana kama ukiwamiliki katikati ya uwanja, na ukimpita Umtiti tu hao wengine hawana jipya.
Bayern nao ugonjwa wao kama Barca tu.
Roma hana spidi sana ya kufanya maajabu mbele ya Liverpool.
Madrid timu yao haina maajabu zaidi ya bahati tu, mashambulizi ya kustukiza pamoja na ubora wa Ronaldo katika kufunga unawabebà sana.
Sevilla anaweza akamsumbua Liverpool ila safari hii kama wakikutana tena basi mwisho wa Sevilla ni hapo.
YNWA...
Tukutane fainali.