Liverpool nao si wa kuwachukulia poa, nakumbuka mwaka 2005 Liverpool walisababisha wateja wote baa waondoke wakati wa half time baada ya kubugizwa mabao matatu bila na AC Millan huku mtangazaji akitia msumari wa moto kwa kusema haijawahi timu kuwa nyuma kwa mabao 3 halafu ikachukua kombe. Kipindi cha pili tuliangalia watu 2 tu, huku watu wote wakiwa wameondoka. Namkumbuka mzee Manyama alikuwa shabiki mkubwa wa Liver siku hiyo alitoa ofa za bia akiamini Liver watachukua kombe, ila alipotea katika mazingira ya kutatanisha, haijajulikana mpaka leo aliondoka saa ngapi pale baa na alipitia mlango gani. Kipindi cha pili Steven Gerrad aliongoza kiama cha Millan na Liver kuchukua kombe wakishangiliwa na watu wawili katika baa tuliyokuwamo.