DSM : Alikiba alivyowakutanisha watu maarufu Afrika Mashariki

DSM : Alikiba alivyowakutanisha watu maarufu Afrika Mashariki

Hivi punde

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2017
Posts
2,554
Reaction score
8,587
Sherehe ya pili ya kuhitimisha harusi ya msanii maarufu wa muziki wa kizazi kipya, Ali Kiba imefanyika jana jijini Dar es Salaam, huku ikiwakutanisha watu maarufu katika nchi za Afrika Mashariki.

Watu hao ni pamoja na mke wa Rais mstaafu wa Awamu ya nne, Mama Salma Kikwete ambaye alihudhuria kama mama mlezi huku akidai kama si safari hata mumewe angekuwepo.
Mbali na mama Salma, wengine waliokuwepo ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu; Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Antony Mavunde; Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangalla na Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete.


Wengine waliohudhuria ni Gavana wa Mombasa nchini Kenya, Hassan Joho ambaye ni rafiki wa karibu na Kiba na hivyo kufanya wana Afrika Mashariki kukutana sehemu moja ambapo mara kwa mara walionekana wakizungumza.


Kwa upande wa wasanii walikuwepo wengi akiwemo Mwana FA, Christian Bella, Vanessa Mdee, MimiMars, Eshi Buheti, Idrissa Sultan na Ommy Dimpozi ambaye pia alikuwa ni mmoja wa wanakamati wa shughuli hiyo.

Wadau wa mpira pia hawakuwa nyuma, ambapo msemaji wa Timu ya Simba, Haji Manara alinogesha sherehe hizo ukizingatia aliingia ukumbini hapo akiwa ametoka uwanjani timu yake ikiwa imewashinda wahasimu wao, Yanga.
Nyota wa mpira wa miguu waliokuwepo ni pamoja Emmanuel Okwi anayekipiga Simba, wakati kwa upande wa Yanga waliwakalishwa na mchezaji Haroun Canavaro.

Pia walikuwepo watangazaji maarufu akiwemo Millard Ayo, Husna Dacota na Shadee wote wa Clouds Media, Angela Msangi wa TBC1 na Abdallah Chambua ’Dulla’ wa kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa kituo cha EATV.
Baadhi ya waalikwa hao walitoa nasaha zao ambapo kwa upande wa mama Salma aliwasihi wasanii hao kulinda ndoa zao na kuweka mambo ya umaarufu pembeni.

Wakati Dk Kigwangalla alitangaza kuwapa ofa Ali Kiba na mkewe kwenda kutembelea kivutio chochote cha utalii watakachoona kinawafaa katika fungate yao na kuahdi gharama zote kuzilipa yeye.
 
Kama ikiwekana kamba za mbuzi si jero tu unatafuta paa la nyumba tu
Sie maisha yanaendelea. Jinyonge mwenyewe ndugu yangu. Kwani zisingeibiwa zingekuwa mfukoni mwako sasa hivi?
 
Sie maisha yanaendelea. Jinyonge mwenyewe ndugu yangu. Kwani zisingeibiwa zingekuwa mfukoni mwako sasa hivi?
We si ndo umataka hayo ktk post zangu sijasema nataka kujinyonga mkuu mbona wanilisha maneno
 
ofisi zipo Dom watu wameamkia Dar kudadek
 
We si ndo umataka hayo ktk post zangu sijasema nataka kujinyonga mkuu mbona wanilisha maneno
Sijakulisha maneno mkuu. Nimewaza tu ni jinsi gani maisha yako yameingia huzuni kutokana na huo wizi.
 
Sie maisha yanaendelea. Jinyonge mwenyewe ndugu yangu. Kwani zisingeibiwa zingekuwa mfukoni mwako sasa hivi?


Dada yangu, watu wanakosa hata hiyo hela ya kununua kamba za kujinyonga. Usifanye masihara hali ni ngumu sana.
 
Dada yangu, watu wanakosa hata hiyo hela ya kununua kamba za kujinyonga. Usifanye masihara hali ni ngumu sana.
Ha haaaa. Sio lazima ununue..unaweza ukaiba. Au atumie shuka lake kujinyonga!
 
Back
Top Bottom