Dua Lipa ashtaki Samsung $15M kwa kutumia picha zake kwenye Maboksi ya TV

Dua Lipa ashtaki Samsung $15M kwa kutumia picha zake kwenye Maboksi ya TV

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Staa wa muziki wa Pop duniani, Dua Lipa, ameishtaki kampuni ya Samsung akidai fidia ya dola milioni 15 (takriban shilingi bilioni 40 za Kitanzania), akituhumu kampuni hiyo kutumia picha yake kwenye maboksi ya TV huko nchini Marekani bila ridhaa yake.

Katika kesi hiyo iliyofunguliwa kwenye Mahakama ya Wilaya ya California, Dua Lipa anadai kuwa Samsung walitumia picha ya tamasha lake la Austin City Limits la mwaka 2024 kutangaza mifano mbalimbali ya TV zao. Wanasheria wake wanasema kitendo hicho kililenga kutumia umaarufu wa msanii huyo kuongeza mauzo, jambo ambalo ni ukiukwaji wa haki miliki na matumizi mabaya ya taswira yake.

Inasemekana Dua Lipa aligundua jambo hilo mwezi Juni 2025 baada ya mashabiki wake kusambaza picha za maboksi hayo mtandaoni na kuyabatiza jina la “Dua Lipa TV Box.” Pamoja na malalamiko hayo, wanasheria wake wanadai kuwa Samsung walikaidi maombi ya mara kwa mara ya kutaka waache kutumia picha hiyo.

1778487879888.png


1778487731416.png


Source: Reuters
 
Back
Top Bottom