Dua zetu Watanzania zinahitajika kwa Aston Villa

Dua zetu Watanzania zinahitajika kwa Aston Villa

Aston Villa walipiga mkwaju moja tu galini hadi mechi inaisha na kati ya mechi 10 walizobakiza nne watapambana na timu ambazo ziko top six kwa sasa.

Siioni Aston Villa wakibaki EPL msimu ujao, uwezekano wa kushuka daraja ni mkubwa sana.

Wachezaji wote wa Aston Villa akiwemo Samatta hawana kiwango cha kucheza EPL. Championship ndio size ya ligi ile ya Belgium aliyokuwa akichezea.
 
Washashuka daraja hao...

Samatta ajiandae kisaikolojia tu, na sijui nani alimshauri huyo nwana mdogo kupoteza muda wake kwenda Villa wakati timu nyingi tu za EPL zilionesha interest
 
Kusema ukweli jana ile machi nilishindwa kuendelea kutazama aisee sio kwa moto ule waliokuwa wanapelekewa na Lester City hawafai hata kwa kurumagia, ila naamini hata wakishuka Bridge Mshikaji wetu wa kuitwa Samagoal77 atapata timu ya kumchukua na yy kubaki ligi kuu
 
Hao kama uwezo wao ndio umefikia hapo basi itafaa zaidi kama wakishuka daraja. Wenye kuwapenda kwa ajili ya Samatta wawaombee tu japo maombezi bila jitihada uwanjani ni bure tu.
 
Itashuka lakini
Nakamba, samata na grealish watabaki epl kuchezea team zingine.
 
Aston Villa walipiga mkwaju moja tu galini hadi mechi inaisha na kati ya mechi 10 walizobakiza nne watapambana na timu ambazo ziko top six kwa sasa.

Siioni Aston Villa wakibaki EPL msimu ujao, uwezekano wa kushuka daraja ni mkubwa sana.

Wachezaji wote wa Aston Villa akiwemo Samatta hawana kiwango cha kucheza EPL. Championship ndio size ya ligi ile ya Belgium aliyokuwa akichezea.
Samatta kiwango anacho cha kucheza Epl useme timu ndiyo hana ,kwa kipindi kifupi amewafunga makipa wakubwa tu kwa sasa ktk soccer la ulaya,amemfunga Liverpool mara mbili ikiwemo ktk ligi ya ulaya na epl amewaweza mabeki bora ulaya na kufanikiwa kutikisa nyavu za timu zao zikiwamo pia Mancity,pamoja na ugeni wake...ki takwimu tayari amewatupa mbali mamia ya wachezaji ambao wamecheza msimu wote huu epl akiwamo Lingard
Tumpongeze kwa alichokionyesha hadi sasa na huenda akaiokoa Asvl isishuke mkabaki kushangaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukumbuke game yao ya kabla hii cjui ni fa wao walimpiga Leicester,na hawahawa tunaowabeza ndio walitinga finali wembley na mancity wiki jana!
Kwa hiyo mpira unabadilika ingawa ndio tunajua kuwa si wazuri ki hivyo
Kusema ukweli jana ile machi nilishindwa kuendelea kutazama aisee sio kwa moto ule waliokuwa wanapelekewa na Lester City hawafai hata kwa kurumagia, ila naamini hata wakishuka Bridge Mshikaji wetu wa kuitwa Samagoal77 atapata timu ya kumchukua na yy kubaki ligi kuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Baada ya kuangalia mechi kadhaa za timu pendwa Aston Villa, Ni dhahiri timu ya Aston Villa ina kila dalili ya kushuka dalaja. Kila utakapoangalia mechi ya Aston Villa, kuna baadhi ya vitu viko wazi. Ni timu ambayo ina beki mbovu, wachezaji wana uzembe mwingi, kuna lack of confidence kwa wachezaji wengi. Ni timu ambayo ni HOPELESS, ni vyema Samatta akaanza kujipanga kucheza Championship, Aston Villa kushuka daraja ni jambo lisiloepukika.

NAWASILISHA!.
Dalaja = daraja
 
Hamna cha dua wala sala hapo. Kama kiwango hamna ni hamna tu. Labda mumtafutie Samatta team ingine itakayobaki EPL la sivyo Championship itaanza kuonyeshwa mabanda ya mpira msimu ujao.
Azam wanaonyesha.
Kuna channel inaitwa ESPN na ESPN 2
 
Back
Top Bottom