Dubai na ujenzi wa jengo mfano wa pete

Dubai na ujenzi wa jengo mfano wa pete

errymars

Member
Joined
Dec 17, 2019
Posts
98
Reaction score
285
Wakati dunia tuko mwaka 2022, Dubai wanataka kutonyesha kuwa wao wako mbele ya muda, wanaishi ‘future’ yetu.

Wataalamu wa mambo wanasema Dubai ni kama tayari wanaishi mwaka 3000, kwa maana Dubai wako mbele yetu kwa miaka 978.

Hivi karibuni Dubai wametangaza mpango kuwa, pale lilipo jengo liitwalo BURJI KHALIFA ambalo tangu 2009 ndio jengo la ghorofa refu zaidi duniani, Sasa mahala hapo kulizunguka ghorofa hilo la ajabu wanataka kujenga jengo lingine la duara mfano wa pete ambalo litakaa likielea angani kulizunguka BURJI GHALIFA (Ghorofa refu zaidi duniani lililoko pale Dubai).

Jengo hilo la duara mfano wa pete litakuwa ni kubwa kiasi urefu wake kwenda juu litakuwa na Meter 550, yaani viwanja vitano na nusu vya mpira wa miguu.

Na ukubwa wake litaweza kukaribia kuifunika Dubai yote, na ndani ya jengo hilo mfano pete linaloelea hewani kutakuwa na kila kitu, nyumba za makazi, Maofisi, Maduka makubwa, Bustani za kupumzika na mahitaji yote muhimu kwa mwanaadamu.

Wajenzi wa jengo hilo wanasema wanataka kui-challange dunia, na kuionyesha maarifa mapya ambayo hayakushubudiwa hivi karibuni.

Na pia Dubai wanaendelea kutekeleza miradi mikubwa zaidi ambayo ina duwaza walimwengu na kuwaacha midomo wazi

Wataalam wanasema dubai imeandaa miradi mikubwa ambayo ni sehemu moja ya kuhakikisha kua dubai inaendelea kua moja ya sehemu nzuri ya kustaajabisha na kuvutia zaidi na ikitarajia kufanya mageuzi makubwa ambayo hayajawahi kudhuhudiwa hapa dunia.

Sasa utajiuliza ni miradi gani wamepanga kuifungua,Jibu ni kwamba ipo zaidi ya miradi 11 ambayo inatarajiwa kufunguliwa ivii karibuni na miongoni mwa miradi hio ni

Mradi wa Atlantis, Royal
Hoteli ya Royal Atlantis Resort & Residencesambayo iko mbioni kufunguliwa baadaye mwaka huu. Mradi huo wenye thamani Dhs5.15 bilioni utakua na vyumba 231 vya kifahari, vyumba 693 vya hoteli na vyumba vin102.

Hoteli hiyo ya gorofa 43 pia itajumuisha mabwawa 90 ya kuogelea yaani swimming pool, ikiwa ni pamoja na bwawa la kustaajabisha la infinity ambalo litakua juu ya paa lililosimamishwa mita 96 juu ya kabisa.

Hoteli hii itahudumia migahawa inayoongozwa na wapishi mashuhuri wa kimataifa, ikiwa ni pamoja na Gastón Acurio, Costas Spiliadis, Ariana Bundy. Heston Blumenthal na Jose Andres.

Na Haito ishia hapo pia Dubai wanataka Kuonyesha ulimwengu kua wao ndio waanzilishi wa kujenga maduka makubwa na mazuri zaidi na hii ita ji dhihirisha kwa ujenzi wa Meydan One

Dubai itaimarishwa zaidi kwa kufunguliwa kwa Meydan One. Jumba hilo litakua katika Jiji la Mohammed Bin Rashid ambalo linatizamiwa kuvunja rekodi na kunyakua taji la chemchemi kubwa zaidi ya fountain dance duniani, ikiwa na maji yenye ukubwa wa mita za mraba 25,800.

Hata hivyo, ujenzi unaonekana kuwa upo katika hatua za awali, kwa hivyo huenda ikachukua muda kwaio usishangae siku za hivi karibuni ukiwa dubai ukapata kushuhudia Jengo la Meydan one.

Hakika kama Ni jeuri ya Pesa ndio inawafanya wawe na Kiburi hichi Basi dubai wao wamezidi ,Huenda usijue kwa jina Ila kwa picha na mifano utatambua tu hii ni Dubai.

Pia Dubai wana tizamia ku jenga na kupandisha One Za'abeel
Maghorofa mawili yaliyounganishwa na The link, chombo kirefu zaidi duniani cha cantilever. Ajabu ni kwamba usanifu huu wa majengo utaangazia orodha ya kawaida ya makazi ya kisasa ya hali ya juu,

lakini pia litajumuisha migahawa ya kiwango cha juu duniani, maduka ya wapishi ya watu mashuhuri,na mabwawa ya kifahari .Kweli hii ndo itakua One za Abeel

Pengine Dubai wao wanataka Kuonekana kua wao ndo wajuzi wa mambo Anyway mradi mwingine unao tizamiwa kufanywa ni ujenzi wa Abu Dhabi Rixos Marina Abu Dhabi hoteli ya kifahari ya Kufaana

hoteli ya Rixos Marina Abu Dhabi (hapo awali ilikuwa mali ya Fairmont) na Ilipata iconhood ya usanifu hata kabla ya kuzinduliwa, ambapo ilipangwa kuzinduliwa mwaka 2020, lakini hatimaye itawasili katika Q3 ya mwaka huu.

Ingawa hakuna taarifa rasmi kuhusu tarehe rasmi ya ufunguzi,lakini imepangwa kwa miezi michache ijayo huenda hoteli hii itazinduliwa, na tayari imeanzisha ukurasa wake wa Instagram - unao kwenda kwa jina la
@rixosmarinaabudhabi

Sio Tu kwenye Mahotel peke yake pia Dubai inatarajia kufungua makumbusho kubwa zaidi itakayo kwenda kwa jina la NATURAL HISTORY MUSEUM (Makumbusho ya Historia ya Asili) ambayo itafunguliwa kwenye Kisiwa cha Saadiyat mwaka wa 2025, Abu Dhabi inabahatika kupata Makumbusho ya Historia ya Asili.

Katika makumbusho hii Utapata Historia ya Asili ya miji inayozingatia tamaduni kote ulimwenguni. Na pia utapata historia ya dunia - na maonyesho ya kuvutia yanayoonyesha mabadiliko ya kibaolojia na kijiolojia.
Kumbuka kwamba dubai hivi karibuni walifungua jumba la kumbukumbu la Yin hadi Dubai lililofunguliwa hivi majuzi kuhusu Yang ya Baadaye.

Lakini Natural history museum)Makumbusho ya Historia ya Asili itakua na kila kitu kwanzia uundaji upya wa mifupa kamili ya viumbe vilivyotoweka kwa muda mrefu, kama vile jumba la makumbusho maarufu la London 'Dippy' (Diplodocus.
20220924_163800.jpg
 
Magu alikua na ukatili wake, ambao kimsingi ndivyo alivyokuta tokea akiwa waziri, alikua mtu wa misimamo, alikua mtu wa sifa, lakini pamoja na makandokando yoote, angefanyika daraja muhimu sana la mageuzi ya nchi yetu kuanza kuota Kwa mbali mambo makubwa kama taifa.

Katika ubaya wake wote, alikua na vichembechembe vya uzuri pia.
 
Ngoja waje vijana wa Arusha watakuja kufananisha Dubai na chuga.😅😅
 
Baadae wanakuja wamarekani na wangese wenzao wa nato wakishanyimwa mafuta wanakiwasha kinoma.panakuwa magofu.
 
Lakini Natural history museum)Makumbusho ya Historia ya Asili itakua na kila kitu kwanzia uundaji upya wa mifupa kamili ya viumbe vilivyotoweka kwa muda mrefu, kama vile jumba la makumbusho maarufu la London 'Dippy' (Diplodocus.View attachment 2377175
Namkubali sana Rashid Al Makhtoum
 
Magu alikua na ukatili wake, ambao kimsingi ndivyo alivyokuta tokea akiwa waziri, alikua mtu wa misimamo, alikua mtu wa sifa, lakini pamoja na makandokando yoote, angefanyika daraja muhimu sana la mageuzi ya nchi yetu kuanza kuota Kwa mbali mambo makubwa kama taifa.

Katika ubaya wake wote, alikua na vichembechembe vya uzuri pia.
Katika kipindi chake majengo yote yalisimama kujengwa akahamishia nguvu kwenye viwanda vya kwenye karatasi majengo yalitoa ukungu. MUNGU fundi sana alijua taifa linaangamia
 
Back
Top Bottom