Dudu Baya: Kinachofanya Tanzania itulie tofauti na jirani zetu ni kuwa sisi tumenyimwa elimu ya haki zetu. Wenzetu wanayo

Dudu Baya: Kinachofanya Tanzania itulie tofauti na jirani zetu ni kuwa sisi tumenyimwa elimu ya haki zetu. Wenzetu wanayo

Akizungumza kwenye moja ya blog za mitandaoni msanii huyo mkongwe amesema kuwa inayoitwa amani tuliyonayo Tanzania ni kwa vile tu wananchi wamenyimwa elimu ya haki zao.

Amesema kwa mtanzania akiwasha runinga akaona kipindi kinaongelea mambo ya katiba anahamisha hiyo chanel haraka sana atatafuta mipira au mziki ama tamthilia ila kuongelea mambo yanayohusu mustakabali wa maisha yao wanaona hayawahusu.

Amesema hicho ndo tunatofautiana na jirani zetu kwa wenzetu asilimia kubwa ya raia wanaelewa haki zao hivyo ikitokea zinachezewa hawataki masihara kabisa.
Kwani huna akili? Haki, sio, lazima, upewe, au uambiwe hizi, ni, haki zako, unazaliwa, unazijua, swala, gumu ni kuzidai
 
Hajui sisi Watanzania tunaakili
Huwa hatupambanii mtu angie madrakani
Hao nirani zetu ni mazezeta tu
Uwezo wa kujua ya jayo hawana
Mm siwezi kuandamana eti mtu fulani awe kiongozi ni unwege
Wewe ndio hujaelewa mada kabisa kama ingekuwa ni mtihani wa shule ungepata 0% au 10%.
Tunapoongelea haki haina muingiliano na mambo ya chama.
Haki zako za msingi kama raia ni jambo lingine na chama cha siasa ni kitu kingine.
Kwa mfano kule Kenya linapotokea jambo lolote watakaloliona linakandamiza haki zao za msingi watajitokeza vijana kwa wazee kupinga jambo hilo bila kuita chama chochote.
Hao watu wa chama kama wataamua kujitokeza kupigania haki wapinga kwa muda wao wanavyojisikia ila raia kama raia huwa hawangoji chama kikawasemee wanaingia wenyewe mtaani kudai haki zao
 
Back
Top Bottom