Jannatul Firdaus
JF-Expert Member
- Aug 4, 2026
- 446
- 1,113
Msanii wa muziki wa Rap nchini, Dudu Baya, ametoa shukrani za dhati kwa Watanzania na wasanii wenzake Madee, Babu Tale, na Fid Q baada ya kumsaidia kumlipia faini ya mahakamani.
Akizungumza kuhusu msaada huo, Dudu Baya ameeleza kuwa fedha kiasi cha Shilingi milioni tatu ambacho alikuwa ameshajiandaa kukitumia kulipia faini hiyo sasa atakitoa kama sadaka kuwasaidia watu wanaokabiliwa na changamoto za kiafya.
Katika mpango wake wa kutoa sadaka hiyo, Dudu Baya amebainisha kuwa atagawanya fedha hizo kwa watu watatu, ambapo kila mmoja atapokea Shilingi milioni moja.
Walengwa wa msaada huo ni pamoja na baba mzazi wa msanii Banana Zoro, Mzee Zahir Zoro; msanii na mbunge wa zamani, Professor Jay; pamoja na mama yake mzazi Dudu Baya mwenyewe, ambao wote wamekuwa wakiuguza maradhi kwa muda mrefu.
Hatua hii imekuja pia kama jibu kwa wakosoaji waliokuwa wakidai kuwa asingeweza kutimiza ahadi zake.