Dudubaya adakwa LIVE kwa kuiba simu ya Papaa Mopao wa Twanga Pepeta

Dudubaya adakwa LIVE kwa kuiba simu ya Papaa Mopao wa Twanga Pepeta

Amalinze

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2012
Posts
6,780
Reaction score
5,305
DUDUBAYA.jpg
Msanii Dudubaya aka Kapafona aka Mapafu ya mbwa ameingia katika Skendo nyingine baada ya kushutumiwa kutaka kuiba simu ya mdau mkubwa wa Twanga pepeta ajulikanae kama Mapao ambae alikuwa amekaa naye meza moja pale Mango Garden huku Twanga Peteta wakiburudisha Tarehe 14 March.

Tukio hilo la fedheha lilitokea usiku wa Jumamosi kwenye ukumbi wa Mango Garden , Kinondoni Jijini Dar es Salaam , ambapo msanii huyo galacha licha ya kuwa mbabe lakini alijikuta akilainika na kuinamisha kichwa chini kutokana na kukutwa na simu ya ‘Pedeshee' Fredito Mopao.

Dudu Baya ambaye alikaribishwa kwenye meza ya Mopao na Mpambe mkubwa wa Mopao anayefahamika kwa jina la John Cena , alikaa hapo huku wote wakifurahia ofa zilizokuwa zikitolewa na Mopao lakini haikufahamika ni muda upi msanii huyo alikwapua simu.

Wakati Mopao alipotaka kuondoka ukumbini hapo ndipo aliposikika aking'aka simu yake aina ya Samsung Note4 iko wapi. Wakaanza kuulizana taratibu katika meza ile lakini hakupata jibu lililoeleweka akaanza kuchachamaa kuidai.

Wakati Mopao ‘akikoroma' ndipo mtu mmoja alimshuku msanii huyo na kusema wamsachi miguuni na ndipo simu hiyo ikakutwa imefichwa kwenye soksi.

Wadau mbalimbali na mashabiki pamoja na Mopao mwenyewe walitaka kumuangushia kichapo lakini wengine wakatumia busara na kumwacha msanii huyo akibaki kaduwaa kwa aibu.

Mkurugenzi Mtendaji wa bendi ya Twanga Pepeta Asha Baraka amesema amesikitishwa sana na kitendo hicho kwani Dudu Baya alipokelewa kwa heshima zote kama msanii.

"Dudu Baya ni msanii mkongwe hivyo hatukutarajia kabisa kama angeweza kufanya kitendo cha fadhaa kama kile, hii yote ni tamaa walizonazo wasanii inasikitisha, nina imani kubwa hata John Cena aliamua kumpeleka katika meza ile maalum ya Mopao kutokana na heshima yake na mchango mkubwa alioutoa katika muziki wa kizazi kipya katika sanaa lakini sasa amejiharibia" alisema Asha.
 
Kwani ukiishiwa lazima uibe au ni mwizi toka zamanii,huyu mziki ushamshinda bora awe baunsa wa club au auze biskuit stendi

Ni Aibu kubwa sana kitendo alichokifanya kapafona.
 
Wabongo hukawii kuwasikia hilo nalo ni kwa ajili ya Clouds FM kuwatia stress wasanii!!

Ilibaki kidogo jamaa wamchome moto
sema busara za wadau wanaomjua ilimsaidia
 
Duh! mjini pagumu kuishi kisanii kumewashinda kina msofe ushauri wa bure arudi kijijini ashike jembe sometimes life is not complicated ila tunajichanganya sisi wenyewe.
 
hivi dudu ndio kaisha namna hiyo juzi tu si alisema yeye ana hela za kutosha na kama kuna msanii kaishiwa aende akamuajili imekuaje mbona nouwma sana
 
hivi dudu ndio kaisha namna hiyo juzi tu si alisema yeye ana hela za kutosha na kama kuna msanii kaishiwa aende akamuajili imekuaje mbona nouwma sana

Labda anazungumzia pesa za malaya wake, c nasikia naye aliolewa kama Mziwanda, Gadner na Ezden
 
Samsung Galaxy Note 4 sio mchezo,namshauri Ze Dudu aende kwa Dogo Hamidu 26 Number ampe michongo....Wizi sio mzuri...
 
Maisha yasiyo na uhalisia sio mazuri mwaka jana kuna gazeti la udaku lilifanya naye mahojiano tukaandikiwa kuwa jamaa mambo safi na anamiliki machimbo/vitalu vya madini na picha tukaoneshwa
 
Maisha yasiyo na uhalisia sio mazuri mwaka jana kuna gazeti la udaku lilifanya naye mahojiano tukaandikiwa kuwa jamaa mambo safi na anamiliki machimbo/vitalu vya madini na picha tukaoneshwa

Duuuuhh leo hii anapiga Simu?
 
Back
Top Bottom