Kipenzi Changu
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 59,734
- 140,476
Huyu naye kakosa kazi
Nimetoka kumwambia mjukuu wangu wa kike wa form 1 kuwa maisha yangu yaliyobaki sitarajii kuona tena numero uno wa TZ akiwa "ke", kaniambia yeye atakuja kuwa, nikamuhakikishia kuwa Watanzania wa kesho hawatakuwa wajinga tena kama wa leo, hilo halitowezekana.Tumeshagongwa na nyoka,hata Jani likitugusa tunashtuka!
Nadhani sitakuja kushuhudia Rais mwanamke Katika maisha yangu yaliyobaki!
Itachukua muda kufuta kumbukumbu ya Rais mwanamke wa kwanza na akawa na roho katili kushinda marais wote waliotangulia!
Ama kweli pata pesa au madaraka,tujue tabia Yako!
Hivi Tanzania hii kuna mtu anatamani tena kuja kuongozwa na maku? Hapana imetosha bwana!Natamani Waziri Dorothy Gwajima aje kuwa Rais baadae.
Dudubaya amesema hayo wakati wa mahojiano na ST Bongo, ambapo amemsifia Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima, kwa uchapakazi wake na ufuatiliaji wa masuala ya kijamii.
Aidha, Dudubaya amefika mbali zaidi kwa kueleza matamanio yake ya kumuona Waziri Gwajima akija kuwa Rais wa Tanzania siku za baadaye
Pia soma:
~ Waziri Gwajima aingilia hoja ya Mdau aliyedai mtuhumiwa aliyemfanyia ukatili mtoto anatamba mtaani
Bi ushungi kawaharibia Wanawake wengine ambao walikuwa wana ndoto ya kushika nafasi hiyo!Ukweli ni kwamba Dkt. Gwajima D mimi ni mmoja wa watu tunaoupenda sana uwajibikaji wako, naungana na MAMBA24 kukupongeza haswa kwenye kutoa mchango wa malezi katika makuzi ya vijana.
Ila niache pia kuwa mnafki huyo jamaa ameongea kwa muhemko tu utazani hajui kinachoendelea,Ni ngumu sana mwanamke kukalia kiti cha uongozi wa taifa hili baada ha 2030.Isipokuwa ninakuomba kama mama,usiache kuendelea kupambana katika uongozi wako,you born to be leader,pamoja sana Bi’mkubwa.
Mimi sijamaanisha hivyo mkuu🦅Bi ushungi kawaharibia Wanawake wengine ambao walikuwa wana ndoto ya kushika nafasi hiyo!
Hakuna chama kinaweza simamisha mwanamke kama kina Nia ya kushika madaraka!Labda baada ya hiki kizazi kufutika!