Dudubaya amesema hayo alipokuwa kwenye kipindi cha Planet bongo kinachorushwa na kituo cha Televisheni cha EATV na kudai hakuna mwanaume ambaye anaweza kutembea na mwanamke wake na kusisitiza kuwa yeye anajitambua
"Mimi sijaoa bali nimekuwa tu nikizaa na wanawake lakini hakuna mwanaume ambaye anaweza kutoka na mpenzi wangu sababu najitambua, lakini nikwambie tu kitu sijawahi kumuacha mwanamke asiwe kichaa au asilie, ndiyo maana wanakwenda mpaka kwenye vyombo vya habari wanaongea ongea huko, kwa hiyo mimi najiamini". Amesema Dudubaya
Dudubaya kwa sasa anafanya vyema na wimbo wake mpya 'Inama' ambao ameshirikiana msanii TID