Dugange: Serikali inafanya tathmini kuona kama mikopo ya 10% inaweza kutolewa kwa mtu mmoja mmoja

Dugange: Serikali inafanya tathmini kuona kama mikopo ya 10% inaweza kutolewa kwa mtu mmoja mmoja

Mwanamwana

Platinum Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
9,604
Reaction score
22,722
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)akijibu maswali bungeni leo Juni 15, 2026, amesema Serikali inafanya tathmini ili kuona kama mtu mmoja mmoja anaweza kupata mikopo ya Halmashauri ambayo imekusudiwa kwa makundi

''Ni kweli kwamba mikopo hii inatolewa kwa vikundi vya watu watano na kuendelea. Lakini kumekuwa na mafanikio kwa baadhi ya vikundi ambavyo vinachukua mikopo, lakini kumekuwa na changamoto pia kubwa kukopa kwa vikundi.



Kwa hiyo, serikali inaendelea pia kufanya tathmini kuona uwezekano, ikiwa tutakuwa na mtu mmoja mwenye uwezo wa kuchukua mkopo na akaweza kuajiri watu wengine, vijana, wanawake na watu wenye ulemavu wengine, basi bado itakuwa dhamira ya mkopo huo inaendelea kutimia.

Hoja hiyo pia serikali inaendelea kuifanyia tathmini hivi sasa na kuona uwezekano wa kuelekea kwenye mikopo ya mtu mmoja mmoja."
 
Back
Top Bottom