Setfree
JF-Expert Member
- Dec 25, 2024
- 6,238
- 8,194
Duh, kama hizi ndio faida za bia/pombe, basi akili zetu zinahitaji 'reforms'"
Kaa siti ya mbele, nikusimulie vituko na mikasa ya kweli iliyosababishwa na wanywa bia/pombe, halafu ujibu swali langu: "vituko na mikasa hii ndio faida za bia/pombe?"
SEHEMU YA KWANZA(I)
Visa na vituko vifuatavyo ni vya kweli kabisa, sio chai... majina halisi ya wahusika yamehifadhiwa.
Baba mmoja alikuwa mfanyakazi serikalini. Kila tarehe ya mshahara ikifika, baada ya kazi alikuwa akielekea moja kwa moja baa. Alikuwa anakunywa pombe mpaka usiku wa manane, huku akiwagawia makahaba pesa. Akirudi nyumbani, vijisenti vilivyobaki ndio anamkabidhi mke wake ambaye hakuwa na kazi. Maisha ya nyumbani yalikuwa ya tabu sana. Watoto wake walilala njaa mara kwa mara, wengine walishindwa kuendelea na shule kwa kukosa ada na mahitaji. Mtoto wake wa pili alijiua baada ya kudharauliwa na wenzake shuleni kwa kuvaa sare zilizochakaa.
==============
Kaka mmoja alifukuzwa kazi kwa sababu ya kulewa wakati wa kazi katika kampuni ya umeme aliyokuwa ameajiriwa. Huyu kaka alikuwa fundi mwenye kipaji kikubwa katika kampuni hiyo. Siku moja, walikuwa na hafla ya kampuni. Siku hiyo kaka huyo, alilewa sana na kufanya vituko mbele ya maboss wake wa kazi. Alitamka maneno ya aibu, na kutoa matusi hadharani. Asubuhi yake, alipofika kazini, alikuta barua ya kusimamishwa kazi ikimsubiri mezani. Hadi leo, hajapata kazi nyingine yenye mshahara mzuri kama ule. Amebaki anajuta.
==============
Babu mmoja aliua watoto watatu kwa kuendesha gari akiwa amelewa pombe. Huyo babu alikuwa na tabia ya kunywa pombe kisha anaendesha gari. Siku moja, akiwa amelewa chakari, aliigonga familia iliyokuwa inapita barabarani. Watoto watatu waliaga dunia papo hapo. Alikamatwa, akahukumiwa kifungo cha miaka mingi. Akiwa ndani ya gereza, anasema kila usiku anaota ndoto mbaya za wale watoto waliofariki.
==============
Kaka mmoja aliwapiga wazazi wake waliokataa kumpa pesa ya pombe. Kaka huyo alikuwa anategemea pesa za wazazi wake wastaafu ili akanywee pombe. Siku moja walipokataa kumpa hela ya pombe, aliwachapa hadi mama yake akavunjika mkono na baba yake alianguka kwa presha. Kaka huyo alikamatwa, lakini familia kwa huruma tu ilimuondolea mashtaka. Sasa anaishi kwa kujificha kwa aibu, huku majirani wakimchukulia kama mtu asiye na utu.
==============
Dada mmoja aliachwa na mumewe kwa sababu ya kulewa na kuzurula usiku. Huyo dada alianza kunywa pombe kidogo kidogo baada ya kazi. Lakini baadaye ikawa kawaida. Kila mara alirudi nyumbani usiku wa manane, akiwa amelewa. Kuna siku alishindwa hata kufungua mlango. Mumewe alivumilia sana hadi siku alipomkuta akiwa kwenye uhusiano na mlevi mwenzake. Mumewe alifungasha virago na kuondoka. Dada huyo sasa anaishi maisha ya kujuta, akilea watoto peke yake kwa tabu.
=============
Jamani, kama hizo ndio faida za bia/pombe, basi akili zetu zinahitaji "reforms."
Pombe inaharibu afya, inavuruga familia, kazi, ndoto za mtu na hata utu wa mtu. Wanywao pombe, wengi huishia kuwa walevi. Ulevi ni mzigo mzito. Ukiishaubeba mzigo huo ni vigumu sana kuutua. Utakukandamiza mpaka ushindwe hata kusimama wima!
Kama umelemewa na ulevi, Yesu anakuita leo. Atakupa nguvu ya kuachana na pombe/bia na kuanza maisha mapya yaliyojaa amani na heshima. Usingojee kesho. Chukua hatua leo: njoo kwa Yesu akuokoe na kukuondolea kiu ya bia/pombe. Yesu anasema: "Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha." (Mathayo 11:28). Ukitubu dhambi hiyo ya ulevi na kumpokea Yesu kwa imani moyoni mwako, ataikata kabisa kiu ya pombe/bia.
=============
KATIKA POSTS ZIJAZO NITAKULETEA HAPA HAPA, SEHEMU YA PILI YA HABARI ZA KWELI, VISA NA MIKASA YA AJABU ILIYOSABABISHWA NA UNYWAJI WA POMBE/BIA. SUBSCRIBE USIPITWE...