Duh, kama hizi ndio faida za bia/pombe, basi akili zetu zinahitaji "reforms"

Hiyo ndo hali halisi,lkn jiandae kujibiwa kwa maneno ya karaha dada,au kutojibiwa.labda kwa umefungua huu uzi kabisa,mi uwa nawauliza kero na madhara wapatayo wanywao pombe,lkn wengi huwa hawanijibu,naambulia matusi tu,nasubiria majibu yao au maoni yao tu 😂😂🤭
 
Hayo maneno ni yakujifariji tu,ili a enjoy pombe lazima anywe alewe haswaa,kuandikiwa maneno ati kunywa kistaarabu ni danganya toto tu kwa wasomaji na hata wanywaji.nikuulize hivi mtu unaweza kunywa na usilewe???, Kama haulewi si bora tu unywe maji au juisi!?,.
 
Pombe ya kistaarabu ni nzuri na inajenga afya. Kuna jamaa alifanikiwa kwa mawazo anayopata katika vikao vya pombe. Kwenye vikao unapata mengi. Madili mengi yanasukwa wakati chupa za bia zipo mezani. Hata waandishi wa habari wengi wao wanapata habari kwenye hivyo vijiwe.
 
Guidelines recommend that if individuals choose to drink alcohol, they should limit consumption to one drink or less per day for women and two drinks or less per day for men. These limits are for days when alcohol is consumed and are not an average over time.
 
NB_1: Kunywa Pombe kupitiliza ni hatari kwa Afya na Uchumi wako.

NB_2: Kushika dini na Imani kupitiliza ni hatari kwa Afya, Uchumi na Usalama wako. Tafadhali Abudu kistrabu.
Kwa hizo NB mbili, kushika dini na imani kupitiliza ni hatari kuliko kunywa pombe kupitiliza.
 
Kulewa siyo tatizo, cha msingi ukilewa usiwe tatizo kwa wengine.

Upande wa pili watu wa dini wakilewa Imani wanaanza kupigia kelele watu sokoni, Wengine hujilipua na kuua sababu ya jina la Mungu.

Kwahiyo haya mambo yapo pande zote, na ustarabu unahitajika pote.
 
Mungu hajakataza kunywa pombe. Ameruhusu watu kumtolea sadaka kwa kunywa pombe hata na wachungaji wanaruhusiwa kunywa, ingawa hawa wachungaji wameekekezwa wasinywe sana (wasiuzoee ulevi). Setfree soma Kum 14:26-27 na 1 Tim 3:3 SUV

[26] na zile fedha zitumie kwa cho chote itakachotamani roho yako, ng’ombe, au kondoo, au divai, au kileo, au roho yako itakacho kwako cho chote; nawe utakula huko mbele za BWANA, Mungu wako; tena furahi, wewe na nyumba yako;
[27] na Mlawi aliye ndani ya malango yako usimwache, kwani hana fungu wala urithi pamoja nawe.
 
Waumini wanaofanya hivyo,wanakua hawajitambui au hawatambui dini yao,, maana dini haiyataki hayo na haitaki mihemko.,lkn pia pombe inachochea mtu kuingia kwenye madhara mengi sana.,kuliko imani.
 
Wakinitusi, mimi nahesabu wamenipulizia perfume. Nikirushiwa matusi najua kuwa ujumbe umepenya ndani kabisa ya moyo. Hivyo kwangu mimi hiyo ni "mission accomplished"
Si unakumbuka yaliyompata Stefano. Yeye alirushiwa mawe kabisa. Lakini akasema: "Naona mbingu zimefunguka" (Matendo 7:55-56)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…